Ni muda mrefu sasa tangu spika wa bunge letu tukufu alipoanza kuhusishwa na tuhuma mbali mbali, wana Jf wengi walijitokeza bila kusahau vyombo mbali mbali vya habari kumtetea SS! sakata linaloendelea mjini Dodoma kwa sasa katika Bunge ni kielelezo tosha kuwa SS si muadilifu kiasi ambacho wengi tungependa tuamini.
kamati ya maridhiano ambayo imekuwa ikiongozwa na Mzee Mwinyi mambo mengi yameibuka ikiwa ni pamoja na SS kuhusishwa moja kwa moja na ujio wa kampuni tata ya Richmond!
taarifa ambazo zimepatikana siku chache zilizopita ni kuwa Mh SS akiwa TIC ndiye aliyebariki ujio na kutoa maelekezo anuai ili wahusika wa Rich mond waweze kupewa msaada pindi ambapo wangehitaji, hiyo haitoshi lakini SS amethibitika kutembelea ofisi za Richmond oversees na hata kupiga picha ya pamoja na mohamed Gire mtuhumiwa mkuu wa Richmond lakini kama hayo haya toshi ni siku chache zilizopita TAKUKURU ilianza kuwahoji baadhi ya wabunge kwa tuhuma za posho mbili! SS kama mpambanaji wa ufisadi kama ambavyo angependa tudanganyike hivyo, akaja juu na kuwa mithili ya Nyati alijeruhiwa kwa risasi kwa ku tetea eti wabunge wasihojiwe NOSENSE! wengine wakadiriki kusema kuwa wanao wahoji wabunge lengo lao ni kuwa ziba midomo wapambanaji bandia wa ufisadi, hoja hii haina mashiko kabisa.
Nimalizie kwa kuwaomba wote waliokuwa mstari wa mbele kumtetea mnafiki, mwenye wivu wa kukosa Uwaziri mkuu SS waje hapa jamvini na watueleze kwa kiasi gani wamekuwa wafuasi wa SS, na kwa kiwango wamekuwa wakimtetea Sita pasipo kuwa na ushadi yakinifu zaidi ya upambe na ulipyoto!
Tunawaomba jamvini hapa na kama ni waungwana mkiri kuwa mlipotoka kumtetea Sita mimi na wengine wengi tupo tayari kuwasamehe endapo nafsi zitawaagiza kufanya hivyo