Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 10,357
- 35,832
Baada ya wabunge wa viti maalum wa Chadema kuangushwa mahakamani siku ya leo na kujipanga kukata rufaa kupinga hukumu hiyo, je Spika Tulia ataendelea kuwatambua kama wabunge kwa kigezo kuwa mchakato wa kisheria dhidi yao bado haujakamilika kwa kuwa rufaa wanayojipanga kuikata bado haijasikilizwa?
Kuweka kumbukumbu sawa tu hapa JF, ni kuwa Spika Tulia toka awali aliweka msimamo wa kuwatambua kama wabunge halali, Halima Mdee na wenzake kwa kuwa walikata rufaa kwenye baraza kuu la chama chao kupinga uamuzi wa kuvuliwa uanachama wa CHADEMA uliofanywa na kamati kuu.
Hata baada ya baraza kuu la CHADEMA kubariki uamuzi wa kamati kuu wa kuwavua uanachama wa CHADEMA bado spika Tulia alisema kuwa ataendelea kuwatambua wabunge hao kwa kuwa walimweleza kuwa wanajipanga kupinga uamuzi wa CHADEMA mahakamani.
Sababu kuu ya Spika Tulia anayoitumia ni kuwa, mchakato wa kisheria dhidi ya wabunge hao bado haujakamilika.
Sasa watanzania wanasubiria tena kusikia kauli ya Spika Tulia kuendelea kuwakumbatia wakina Mdee, tofauti na hapo Spika Tulia ataoneka ni mnafiki.