Wakili Pasco Mayalla - A True Story of My Life: Nilitamani kuwa Wakili sababu ya Wakili Murtaza Lakha, sasa ni Wakili. Je, nitakuwa kama Lakha? Part 1

Hongera sana wakili msomi P. Mayalla.
simulizi inavutia na inasisimua.

kamwe huwezi kufanikiwa kwenye maisha bila kupitia changamoto kwani changamoto ulizo pitia ni zinamchango mkubwa wa mafanikio ya leo.

Picha ninayo ipata enzi hizo utawala wa sheria haikuwepo bali ni mwendo wa ubabe, sheria kandamizi zilikuwa ni kikwazo cha maendeleo ya watu n.k.
 
Hongera sana Bro,nakukumbuka umepaki pikipiki yako nyeusi parking ya block F,ndani kuna Yule miss Tz nyuma ya Nancy sumari anatype assignment,ulimla!?
Mkuu red label, umenikumbusha mbali na swali lako limenichekesha!. Kuna kitu kunihusu mimi, naomba nikiseme na naomba uniamini, maana kwa mtu wa kawaida ni ngumu kuamini!.

Kwanza mimi nilijoin UDSM as a mature candidate, hivyo baadhi ya vitoto vingi vya chuo vilikuwa na umri wa binti yangu!.
Pili nilikuwa nikiishi Block F zile room za juu single.

Tatu, nilisoma kwa kujilipia, hivyo nilikuwa loaded, na kiukweli mademu wengi wa chuo walitegemea boom

Hivyo kwa hizo hoja tatu, ningetaka kuwatafuna!, ningewatafuna sana!, lakini huwezi amini, nimepiga miaka yote 4 bila kugusa mtoto yoyote wa chuo!. Week end nilikuwa narudi home, na kuwaachia madogo gheto yangu ambayo ndio waliifanya machinjio!. Majirani wakiona mizigo inapishana, walidhani ni mimi... kumbe ni madogo!.

Nikiwa kijana, nilikuwa hatari!, thanks God, nimejaaliwa very high self control, kujizuia kutafuna vifaranga nilivyosoma navyo!. Mimi nilikuwa ni mutu ya mizigo mikubwa!, and not at hostel bed!
P
 
Nawauliza mawakili wetu ambao wamekuwa msaada mkubwa wa kutetea Haki za wananchi, kwa nini huwa hawatumii Lugha yetu ya Kiswahili wakati wa kusikiliza kesi au hata wanapo andika hoja zao?!

kwa nini lugha ya kizungu ndio imeshika hatamu badala ya kiswahili?! na inaonekana au imezoeleka wakili anayeweza kutema kizungu basi ndio wakili bora na mweledi!!!

naomba ufafanuzi.
 
Hapa nadhani ni kukusubiri uiseme hoja yako ya msingi kwa nini unataka kuwa kama wakili Lakha?
Nimebahatika kumfuatilia Lakha enzi zile za kesi ya Uhaini na jinsi alivyokuwa akiwahenyesha mashahidi wa usiri kina X, Y nk waliokuwa maofisa usalama hadi ilileta raha ya kuitamani taaluma ya sheria.
Kesi ile ilichangia sana kufanya mapitio idara ya usalama wa taifa na kuigeuza muundo na kuwa TISS.
Sasa kabla ya kuchangia mada yako ngoja tusikie unataka kuwa kama Lakha kwa nini?
 
Back
Top Bottom