Wakili Pasco-A True Story of My Life: Nilitamani kuwa Wakili sababu ya Wakili Murtaza Lakha, sasa ni Wakili. Je, nitakuwa kama Lakha? Part III-Final

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,513
113,643
Wanabodi,
Mwendelezo
Screen Shot 2022-07-31 at 7.00.02 AM.png
Screen Shot 2022-07-31 at 7.00.17 AM.png

Kwa wasomaji wapya this is a true story of my life, nilitamani kuwa wakili kwa sababu ya Wakili Murtaza Lakha toka mwaka 1976, hatimaye sasa nimekuwa wakili, jee nitakuwa kama Lakha?.

Wiki iliyopita, tuliishia Baba Mzee Andrew Mayalla ni miongoni mwa washtakiwa wa Kesi ya Mauaji Mwanza, ilyowangoa madarakani kuanzia Makamo wa Pili wa Rais, Mawaziri 2, Mkuu wa mkoa, na maofisa waandamizi wa serikali mkoani Mwanza kushitakiwa, kufuatia vifo vya watuhumiwa wawili, Masaga Mahula Mazengenuka na Isaack Ngw’ana Nkog’oboko waliokufa mikononi mwa polisi muda mfupi baada ya mahojiano.

The Role of Mzee Mayalla.
Kwenye utekelezaji wa baadhi wa baadhi ya mambo ya baadhi ya idara za serikali, kuna watu wema, wanaolazimika kufanya evils in the line of duty, lakini dhamira zao ndizo zinazowasuta.

Vikao kazi ndivyo vilivyoamua ni mbinu gani zitatumika kuwahoji watuhumiwa, naomba nisizitaje humu, lakini kosa la Mzee Mayalla ni huruma ilimponza.

Baada ya watuhumiwa hao kuhojiwa walivyohojiwa, Mzee Mayalla akaingia huruma, kumbe kwenye Mkoa, RPC yuko chini RSO, hivyo Mzee akaamuru mahojiano ya wawili hao yasimame, kufuatia alivyowaona akaamua kujitolea kuwabeba kwenye gazi yake kwenda kuwakabidhi hospitali wapatiwe matibabu, kumbe wema unaponza.

Wakati wakiwa njiani, ndio wakamweleza mzee kuwa hawajala siku 4!. Mzee akaamua kusimama njiani wapate chochote, wakawa hawawezi kutembea!. Wakaagiziwa soda na keki wakaletewa hapo hapo kwenye gari, ile kunywa tuu, kidogo, ni walitapika damu na ku collapse hivyo kuwakimbiza Bugando.

Kule kwanza walikataliwa kupokelewa, mpaka polisi polisi watoe PF 3!. Polisi wakagoma kwa hoja kuwa ofisa huyo RSO amewaiba mahamusu na kuwasafirisha kwa gari binafsi bila movement order, hivyo if anything happens hawahusiki!.

Akampigia dakitari Mkuu wa Bugando, Dr. Nkulila, akimuita shemeji, wakati huo mama mdogo alikuwa mama wa Kinyiramba, Dr. akatoa amri, wapokelewe. Wakapokelewa na kupatiwa huduma ya kwanza. Mzee akarudi home. Kesho yake asubuhi, ilikuwa mimi natoka na baba kuni drop kwanza shule ndipo aende kazini, mimi ndio huwa wa kwanza kuingia kwenye gari, siku hiyo nikakuta seat yangu ya nyuma imetapakaa damu!. Nilikuwa nakalishwa nyuma hata kama mbele hakuna mtu.

Kumbe wale watuhumiwa wote wawili, kufika asubuhi, they were both no more!. (RIP Watuhumiwa).

Mzee akageiziwa kibao!.

Let me make the long story short, Mzee aliamua kuusema ukweli wote wa what really happened na ukizisikia hizo mbinu za mahojiano!, kiukweli it was shocking kujua binadamu wanaweza kuwafanya vile binadamu wenzao!. Mwisho wa siku kati washitakiwa wote, ni Mzee Mayalla tuu, ndie pekee the one and only aliyekutwa hana hatia na kuachiwa huru!. Watuhumiwa wengine wote walifungwa vifungo virefu!. Hili liliwezekana kwa sababu tuu ya umahiri na utetezi wa Wakili Murtaza Lakha. Ndipo mimi nikaamua nikiwa mkubwa lazima niwe wawili ili nitetee wanaoonewa!.

Maisha ya Mzee baada ya kesi hiyo, was never the same again!, kitu ambacho aliendelea kuwa nacho ni jicho la kuangazia warembo ambalo ni miongoni mwa urithi alioniachia!.

Nakumbuka siku moja Jumamosi, nikiwa darasa la 7 karibu na mtihani wa taifa, hivyo tunasoma tuition mpaka Jumamosi. Tuition yetu ilikuwa ni kwa Mwalimu mmoja anaitwa Mwalimu Ndii, tulikuwa tunasomea nyumbani kwa kina Daria Gwao, nyumbani kwa Mzee Mujengi Gwao, Daria na Carol Nyimbo, walitutangulia darasa moja, huku dada zake Fina na Dora wako sekondari, tuition tulikuwa tunasoma na mimi, Paul Macha, Stepha, Andrew na Emma Mwela, enzi hizo ni enzi za Nyerere, Watanzania wana moyo wa kujitolea, Mzee Gwao, Mbunge amejitolea bure dining room yake kutumika kwa tuition!. Wema wa hivi sijui siku hizi kama upo!.

Sasa siku hiyo ya Jumamosi, tukiwa wote kwa Mzee Kasanga, kuna jirani yetu Stefa, kaja home, tulikuwa tukiishi kizungu fulani, mtu kutembelewa na rafiki wa kike home was not a big deal, hivyo Stefa akaja kunipitia twende Tuition, Mzee Mayalla kumuona Stefa, akamtolea macho na akaninyooshea ishara ya dole gumba, kuwa unajua kuchagua!. Kumbe mimi na Stepha had nothing!, just friends. Baadae Dingi akaniuliza yule ndie mkamwana? nikamwambia no!. Akauliza why not?.

Kuanza kwa Safari Kuusaka Uwakili...
Wakati Baba akiwa kwenye kesi, kule Tabora, Mzee Kasanga pia alimhamisha bibi akaja Dar es Salaam, na mimi kuianza safari rasmi ya kuutafuta uwakili hivyo wote tukawa Dar es Salaam, nyumba ya Drive In ikawa haitoshi, Mzee Mayalla akakaa kwa baba yangu mkubwa Mzee Mfaume, Magomeni Mapipa, baadaye akapata kazi as a Chief Security Officer wa kampuni ya Wataliano ya Cogifer na kuhamia Zanzibar, sijui watu wa maeneo hayo kama walipona! Maana nina wadogo zangu lukuki kila mahali Mzee Mayalla alipokaa na hivyo ndivyo Wasukuma tulivyo!.

Tambaza Sekondari
Tambaza Sekondari tulisoma masomo yote, hadi form II, kuchagua combi, mimi kachagua Arts. Kulikuwa na mwalimu wetu mmja wa Tambaza ni jirani hapo Drive In, akaja kunishitakia nyumbani kuwa mtoto ana akili, lakini amechagua fani ya majinga!. Nikaitwa na Mzee K mbele ya mwalimu na kuulizwa kwanini nimechagua masomo ya wajinga?, nikajibu nataka kuwa kama Lakha!. Niligomewa, Mwalimu Kalunga akaambiwa nirudishwe masomo ya Sayansi, lazini niliamua kusoma yote Sayansi na Arts. Matokeo ya form IV nilipiga A moja ya Siasa, B ya Kiingereza na kutandika makarai yote yaliyobakia. Nika Opt kuchagua HGL, nikapangiwa Ilboru.

Nikiwa Tambaza, tulikuwa darasa moja na mtoto wa Ben Mkapa, na mtoto wa Nyerere, huyu Dr. Mwinyi wa Zanzibar na mtoto wa Malecela, tumesoma nao shule moja primary, wao walitutangulia, tukakuta Tambaza, sisi O-level wao A-level ni watu tunaongea nao sana tuu!. Nikiwa Chuo Kikuu, UDSM tumesoma sheria na Riz1 na ni rafiki!, Kwa Nyerere tunakwenda, kwa Mwinyi tunakwenda, kwa Mkapa ndio usiseme, mimi nimekwenda hadi akiwa US!. Lengo la kuwataja hao ni kuwajulisha tuu mimi ni well connected person, hivyo wanaodhani nanyemelea uteuzi wa ubwete!, are wrong about me, kama ni kutafuta uteuzi, ni uteuzi wa kugombea nafasi za uongozi, na nikitokea nikateuliwa kugombea, nitakuwa nimeteuliwa kwa sababu na deserve kwa sifa na vigezo na sio kwa kubebwa!.

Murtaza Lakha Aibuka Tena Nikiwa Tambaza!
Wakati nikiwa Tambaza. Nyumba yetu ni flat, imeungana na nyumba ya mtu aitwaye Banyikwa. Nyumba hii ndio kulifanyika mipango ya kumpindua Nyerere ile 1982, jirani zetu wawili Mzee George Banyikwa (Rip) na mkewe Zera Banyikwa (Rip), (Kabila ni Wahangaza na walikuwa na mabinti 4 bomba hao, balaa!), (mtoto wa Kisukuma kutoka kijijini, kuja mjini, unakaa next door kwa nyumba yenye warembo hivi!, we acha tuu!). Hawa jirani mtu na mkewe wote walishitakiwa kwenye ile kesi ya uhaini ya 1982, wakili Murtaza Lakha akaibuka tena kuwatetea Mshitakiwa wa kwanza na wa pili, na hapo sasa nikawa namsoma Lakha kwa nafasi.

Ilboru Sekondari Safari ya Uwakili Inaendelea... Nikapuliza Ili Kuisaka One!.
Nikajiunga Shule ya Sekondari ya Ilboru kufanya HGL. Nikiwa Tambaza kuna eneo kule juu linaitwa summit, wanafunzi walikuwa wanapanda huko na kupuliza ile ‘kitu’. Mimi nilikuwa naogopa kuipuliza kwa kuhofia nyumbani watajua. Wale jamaa wote waliokuwa wana puliza ile kitu, Tambaza walitoka na divisheni 1 kali~.Hivyo ili mtu ukasomee sheria chuo kikuu enzi hizo ni kimoja tuu cha Dar es Salaam, UDSM, ni lazima upate Division 1, hivyo nikaamua ili nipate Divisheni 1, na mimi sasa nitapuliza ile kitu ya Tambaza!. Nikapuliza ile kitu!... ile kupiga tuu pafu ya kwanza... la haula!, very unfortunately mimi ikanituma vibaya!. Wenzangu iliwatuma wasome sana, mimi ikanituma vitu vingine kabisa na huo ukawa ndio mwanzo wa kuharibikiwa!. Matokeo ya mwisho, nilikosa Divisheni 1, na ndoto ya uwakili na kuwa kama Lakha ikakatikia hapo!. Mwisho wa Hadithi yetu.

Baada ya ndoto hiyo kufa, ilikuwaje kuwaje sasa ni Wakili, hii ni hadithi nyingine inayojitegemea kwa siku zijazo, nitaiendeleza mdogo mdogo!.

Funzo la simulizi hii, ni kuna vitu wewe unavipanga kama Mungu hajakupangia haviwi, ila kama Mungu amekupangia, vinaweza kuja kutimia hata ukiwa na umri wa miaka 80 kama Mke wa Ibrahim alipomzaa Isaka akiwa na umri wa miaka 80!

Wasalaam

Paskali
 
PASKALI tuambie hapo, baba yako Mzee Mayalla alivyoenda Zanzibar kufanya kazi ya ulinzi kwenye hiyo kampuni uliendelea kuwasiliana naye?

Au aliwahi kurudi nyumbani kuwasalimia? Au ndio ulikuwa mwisho wake na hukutaka kufuatilia kwa bosi/wafanyakazi, au mzee Kasanga uliyekuwa ukiishi kwake kama alikuwa akiwasiliana na baba yako?
 
Nimependa history yako na unavyopangilia lakini pia mtoto wa polisi huwa haishiwi vituko kwa kuwa ana utetezi kutoka kwa baba. Kwa uliosoma nao waliofanikiwa ni Mwinyi tu naye alikuwa akisogezwa taratibu na baba yake akimwongoza vizuri.

Mwinyi JR upole na utulivu umemsaidia sana. Wewe unakosa teuzi kwa kuwa huaminiki saba. Kuna siku unaipinga serikali hadi inakukwepa kwenye mahojiano

Kuna siku unaibuka unawatetea. Hivyo umekuwa mtu wa kuogopwa.
 
Daah...ni story moja kali sana hii braza Pascal Mayalla . Inavutia, imeandikwa kwa lugha yenye imagery na inasomo zuri la kuwapa moyo wale wanaokata tamaa kutaka kufikia yale waliyoyatamania wakiwa wadogo lakini yalikatishwa kwa sababu mbali mbali na sasa wanaumri mkubwa. As long as tupo hai, tusikate tamaa kupambana.

Pia nimejifunza kuwa katika maisha yetu wanadamu kuna watu wanaroho mbaya sana. Kwa Maelezo yako, Mzee Mayala asingekuwa na Wakili mzuri angepotea kwenye kesi ile ya wale mahabusu.

Mwisho nikupongeze kufikia malengo yako 'Wakili Msomi P. Mayalla
 
Sawa, ila kitendo cha wewe kujipambanua kuwa mwana CCM ndio kinachokwaza zaidi. Hicho chama kinawaumiza zaidi raia wa tz. Ushahidi ni uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na uchaguzi Mkuu 2020. Pia, upandaji kiholela wa bidhaa na mengine mengi.
Mimi ni raia wa TZ, sijaumizwa na kitendo cha pasikali kuwa mwana ccm, ila sipendi wewe kuwa wanasaccos wa aboubakar..
 
Kamwe hutokuja kuwa Wakili wa kutetea watu wanao onewa huku ukiwa ni kada wa ccm! Chama kilichopo madarakani!

Hata wale akina Peter Kibatala wangekuwa ccm, muda huu tungekuwa tunaongea mengine. Na mfano mzuri tu mchunguze Albert Msando wa zamani, na huyu wa sasa! Then utapata majibu.

Unatakiwa uchague upande mmoja. Nje ya hapo, utaishi maisha magumu na ya kinafiki sana ndugu wakili msomi, na kada wa ccm.
 
Namkumbuka mzee mmoja aliwahi kusema usifanye urafiki na polisi.

Hata awe mwanao ipo siku atakugeuka atakuchoma tu.

Mheshimiwa (you're blessed name), umewataja wakubwa fulani fulani hapo juu, japo umetoa na sababu zako, hivi kuna umuhimu wa kuwataja ?

Huku nikiamini Ben hakuwa na mtoto lakini umemtaja was he a real mtoto wake?

Natamani siku moja nikupe kesi yangu.

Kazi njema Mheshimiwa.
 
Mkuu
Asante umenifunza kitu!"kama Mungu hajapanga haiwi Kama amepanga hata ukiwa mzee wa miaka 80 inakuwa"!

Nashukuru Sana

Lakini unaogopa nini kama upo well of na hutafuti uteuzi wowote kama ungeandika sentensi hii chini ya bandiko lako!?unaodhani utafukuzwa uanachama!?hata Mimi ni mwanachama lakini nadiriki kuandika hivi;-

"Rasimu ya Warioba irudi mezani Sasa iwe Katiba Mpya"!
 
Back
Top Bottom