Wakazi wa Musoma Mjini wamuomba Prof Sospeter Muhongo kugombea ubunge

kwani uzaliwa haki ya kugombea wewe huoni kuwa ni vitu viwili tofauti..wote tunajua kuwa ana haki ya kugombea..unafikiri yeye hana akili timamu hadi ajazwe ujinga na wazee wachache wenye njaa na matumbo yao ambao wanajua akishapata watakula naye? ..let see ila lazima ataumbuka akijaribu wewe huijui usoma wewe

Dr.Kafumu ni mzaliwa wa Igunga na ilikuwaje vile???
 
Acha ujuha wewe nani kamuomba kuwa mbunge wa musoma? watu wa musoma ni wanafiki hawana lolote wasitake kumchafua msomi wa watu kwan hapo alipo hawapati huduma yake?? mbona mnakuwa na low thinking nyie watu?
 
Mhe. Profesa Sospeter Muhongo, ni mzaliwa wa Musoma Mjini. Ana haki ya kugombea.

Mkuu Ritz, ana haki ya kugombea kama mzaliwa wa Musoma, tena Musoma Mjini pale karibu kabisa na Mwigobelo (Mwighobhelo). Lakini elewa kitu kimoja, siasa za Musoma hazitaki watu wanaokaa Dar maisha yao yote halafu wakati wa kuomba kura ndo waende, hii ni ngumu sana, na kama ataamua, atatumia msuli mkubwa ajabu. Pia, kwa taarifa yako, Prof. Muhongo kaondoka Musoma miaka mingi sana, na si mtu wa kwenda kwenda Musoma kwa maana hiyo, kwa vijana wa Musoma, jinsi walivyo atapata shida sana, na pia kwa taarifa yako, Prof. Musoma hata kwao hapajali! Hili litamwangusha sana. Mfano mwingine kwa hili ni huyu ndugu yetu Dr. Edmund Mndolwa ambae alikuwa pale Coopers, sasa hivi anaahangaika sana, na katika kinyang'anyiro cha sasa, anagombea na Mh. Stephen aka Maji Marefu ujumbe wa NEC kupitia Korogwe Vijijini, na pia wanagombea pamoja Nafasi ya Katibu Uchumi na Fedha Mkoa wa Tanga, na kwa taarifa za wadau hana uhakika wa kushinda, si unakumbuka walivyomtenda EALA?. Si rahisi hivyo Ritz!

Baada ya kutoka South Africa, alikuja na move ya kuanzisha Chuo Kikuu Cha Mwalimu Nyerere kitakachoshugulikia Kilimo, Uvuvi na Ufugaji kule Musoma na Kanda ya Ziwa, kupitia Kanisa la Mennonite, na walifanya mchakato kupitia Ikulu hapo ndipo Mh. Rais Kikwete akapata kumjua vizuri, lakini kwa siasa ni mweupe sana!
 
Wanabodi.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ambaye ni kada wa chama cha mapinduzi CCM ameombwa na wakazi Musoma Mjini kugombea ubunge jimboni humo mwaka 2015.

Profesa Sospeter Muhongo, ni msomi na mzaliwa wa Musoma Mjini wakazi wa mkoa Mara wanasema wakati umefika wa kumpa ubunge Profesa Muhongo, kutokana na elimu yake pamoja na uzoefu wake ili hawatumikie wananchi wa Mkoa wa Mara.

Jimbo la Musoma Mjini kwa sasa linaongozwa na chama cha Chadema kupitia mbunge wake Vicent Nyerere.

Wakazi wengi wa Musoma Mjini wanaoneka kumkubali zaidi Prof Muhongo, kutoka utendaji wake wake katika Wizara ya Nishati na Madini.
Akigombea ubunge tutampiga vijembe hadi akome. Maana leo ni waziri wa Nishati na madini lakini hajawawezesha kabisa wananchi wa Mara kufaidika na dhahabu ya North Mara..Ameshindwa hata fursa alopewa kutumia kodi zilizopendekezwa na kamati ya rais ya kina Zitto...Tunataka atuonyeshe uwezo wake na sio elimu ya darasani..
 
Ukiwa ccm tu ni laana we angalia tu pesa yote ya viwanja shekhe amri abed stadium na kirumba mwanza na maduka yake kuzunguka uwanja vimewashinda utafikiri ni vya miaka 200 kazi yao kula pesa tu ....pamoja na madigee na madoctor n maphd na ma vx.
Binafsi nimewachoka licha ya kuiba dawa mahospitalini hata dawa za vvu wanachakachuwa ccm bwana ni ballaaaa..

huyo muongo mpe muda tu si umesikia mikataba ya gesi ?
 
Huyu jamaa bwana, kila kwenye wabunge wa Chadema yeye yupo. Mara Kawe kwa Mdee, mara Ubungo kwa Mnyika mara watu wa Arumeru Mash wanaulizia bei ya sukari. Haya leo unakuja na ya Musoma mjini. Vipi, we ndio internal Vasco da Gama?
 
Acha ujuha wewe nani kamuomba kuwa mbunge wa musoma? watu wa musoma ni wanafiki hawana lolote wasitake kumchafua msomi wa watu kwan hapo alipo hawapati huduma yake?? mbona mnakuwa na low thinking nyie watu?

Mkuu, unamaanisha kuwa watu wa Musoma ni......................!
 
Wakuu acheni ndoto, juzi tu nilikuwa Musoma Mjini na wananchi wa jimbo hilo zuri waliniomba nami nigombee Ubunge mwaka 2015 na wananikubali kweli. Sasa hizi siasa za kutuma watu wakusemee humu JF inachekesha sana lakini hakuna tatizo nawakaribisha wagombea wote wanaotamani kunisindikiza. This time will be there to win!
 
Mhe. Profesa Sospeter Muhongo, ni mzaliwa wa Musoma Mjini. Ana haki ya kugombea.

Mkuu, ni sawa haki anayo na ungeeleza hivi tangu mwanzo tungekuelewa, lakini umeeleza kana kwamba ulikuwa huku likizo ama ulienda kufanya utafiti sasa unatupa matokeo ya utafiti wako. Kumbuka hata wewe ukiuliza watu wanasemaje juu yako kugombea nafasi kule unakotoka, watakwambia unafaa sana, sitegemei kama watakuwa na ujasiri wa kukukatalia. Kuzaliwa Musoma na kuishi Musoma vitu viwili tofauti, kuna sehemu nyingine jambo la kuzaliwa sehemu wameshalifuta wanaangalia kama unaaishi sehemu hiyo na unafahamu sehemu hiyo si kwa kuamabiwa bali unaishi pale na unaajua wananchi wa sehemu hiyo wanataka lipi. Mie nimezaliwa Mdaula, lakini hii haitoshi kunipa umaarufu wa kuchaguliwa na wananch wa maeneo hayo maana sikai huko. Tunashukuru kwa ripoti ya tafiti yako, ila Musoma hawapo hivyo kama aunavyofikiria.
 
ni wanafiki na wanaleta tabia za ubinafsi hata hapo mhongo anatoa huduma kwa taifa lake tanzania haipo tu musoma
 
Akigombea ubunge tutampiga vijembe hadi akome. Maana leo ni waziri wa Nishati na madini lakini hajawawezesha kabisa wananchi wa Mara kufaidika na dhahabu ya North Mara..Ameshindwa hata fursa alopewa kutumia kodi zilizopendekezwa na kamati ya rais ya kina Zitto...Tunataka atuonyeshe uwezo wake na sio elimu ya darasani..

Mpeni muda hata miezi sita hana toka rais amteue.
 
Musoma mjini ndio Jimbo la kwanza kutangaza matokeo ya Ubunge katika uchaguzi wa mwaka 2010. ukijuwa ni kwa nini Mbunge wa Musoma mjini ndio alikuwa wa kwanza kujulikana Tanzania nzima wala huwezi kuangaika na vithread uchwara kama hivi. wilaya ya Musoma si sehemu ya wa watu wanafki kama mleta mada anavyotaka kutuaminisha.
 
Wewe ni msemaji wa hao wakazi?? Hii habari imekaa kimajungu majungu sana.

Mkuu huyu jamaa thesis yake maji yashingo.....
Ulizania ungepata data so easily buddy...but at last you got to learn that...nothing so simple under the sun..bro
Rudi studio mkuu
 
Musoma Mjini maeneo ya Mkendo Kati.
una kila dalili ya kuwashwa, hakujawahi kuwa na mkutano , mwisenge, mkendo wala makoko sasa kama sio kuwashwa washwa anakosema mabumba ni nini?
 
Kama ni kweli huwa tunachagua viongozi sababu ya elimu zao basi leo umezidi kunithibishia kwamba 2005 Jakaya alitoroga.
 
Wanabodi.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ambaye ni kada wa chama cha mapinduzi CCM ameombwa na wakazi Musoma Mjini kugombea ubunge jimboni humo mwaka 2015.

Profesa Sospeter Muhongo, ni msomi na mzaliwa wa Musoma Mjini wakazi wa mkoa Mara wanasema wakati umefika wa kumpa ubunge Profesa Muhongo, kutokana na elimu yake pamoja na uzoefu wake ili hawatumikie wananchi wa Mkoa wa Mara.

Jimbo la Musoma Mjini kwa sasa linaongozwa na chama cha Chadema kupitia mbunge wake Vicent Nyerere.

Wakazi wengi wa Musoma Mjini wanaoneka kumkubali zaidi Prof Muhongo, kutoka utendaji wake wake katika Wizara ya Nishati na Madini.

CCM oyeeeeeeeeeeee.....!
 
Mpeni muda hata miezi sita hana toka rais amteue.
Hawezi kufanya lolote zuga tu...Kama mfanya kweli lazima angeanza na hili maana hoja zake siku zote ni kwamba madini hayawafaidishi wananchi. Sasa kama zipo kodi zilizokwisha pendekezwa anashindwa vipi kuanza na hizo ili wananchi wafaidike halafu ndipo anakwenda kwenye kuitazama mikataba feki..
 
Wana ccm wa musoma wame muomba profesa muhongo kugombea ubunge!
 
Back
Top Bottom