Wakazi wa Musoma Mjini wamuomba Prof Sospeter Muhongo kugombea ubunge

Wanabodi.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ambaye ni kada wa chama cha mapinduzi CCM ameombwa na wakazi Musoma Mjini kugombea ubunge jimboni humo mwaka 2015.

Profesa Sospeter Muhongo, ni msomi na mzaliwa wa Musoma Mjini wakazi wa mkoa Mara wanasema wakati umefika wa kumpa ubunge Profesa Muhongo, kutokana na elimu yake pamoja na uzoefu wake ili hawatumikie wananchi wa Mkoa wa Mara.

Jimbo la Musoma Mjini kwa sasa linaongozwa na chama cha Chadema kupitia mbunge wake Vicent Nyerere.

Wakazi wengi wa Musoma Mjini wanaoneka kumkubali zaidi Prof Muhongo, kutoka utendaji wake wake katika Wizara ya Nishati na Madini.
ungemuomba Mod Abadilishe heading na kuwa
[h=2]Waislam wa Musoma Mjini wamuomba Prof Sospeter Muhongo kugombea ubunge[/h]
Maana habari hii imekaa kama mawazo ya magaidi...

Huyo tayari ni mbunge...
 
Kwa kweli Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, ni mtu muhimu sana kwenye hiki kipindi wakazi wa Musoma Mjini lulu yenu hiyo.
 
Ritz bana anapima kuona CDM watareact vipi.........hasa kwa kugsa nyerere kuondoka. Haiwezekani. Mwana ukoo wa Nyerere ( Mkapa) atamlinda clan member mwenzake Vincent Nyerere
 
Wanabodi.
Profesa Sospeter Muhongo, ni msomi na mzaliwa wa Musoma Mjini wakazi wa mkoa Mara wanasema wakati umefika wa kumpa ubunge Profesa Muhongo, kutokana na elimu yake pamoja na uzoefu wake ili hawatumikie wananchi wa Mkoa wa Mara.

Wakazi wengi wa Musoma Mjini wanaoneka kumkubali zaidi Prof Muhongo, kutoka utendaji wake wake katika Wizara ya Nishati na Madini.

Mkuu Ritz, Yaani wammpe Ubunge kutokana na ELIMU YAKE, ili awatumikie?..by 2010 walikuwa hawajaliona hili, yaani walikuwa hawajamuona kuwa ni msomi?

-Kama wanamkubali, wameanza lini?
 
ungemuomba Mod Abadilishe heading na kuwa
[h=2]Waislam wa Musoma Mjini wamuomba Prof Sospeter Muhongo kugombea ubunge[/h]
Maana habari hii imekaa kama mawazo ya magaidi...

Huyo tayari ni mbunge...

Mambo ya udini yametoka wapi tena, jadili hoja.
 
Msiwe na tegemeo kuwa ataendelea kupata uwaziri baada ya kuwa mbunge wenu nyie wakurya; mfahamu kuwa baada ya katiba mpya kuanza kutumika baada ya uchaguzi wa 2015 ,mawaziri hawatatokana na wabunge tena!!! Huyu Muhongo ameweza kufanya anayofanya kwasababu hana bugudha za jimbo la uchaguzi!!!

Waweza kupoteza muda wako kusoma na kuamini yaliyoandikwa na ritz!
 
habari za gahawa hizi:flypig::flypig::flypig::flypig::flypig::flypig::flypig::flypig:
 
Kitiba mpya majimbo yawe ni ya kupokezana kam msoga bwagamoyo chalinze next time liwe chini ya CUF ngangari
 
Mkuu Ritz, Yaani wammpe Ubunge kutokana na ELIMU YAKE, ili awatumikie?..by 2010 walikuwa hawajaliona hili, yaani walikuwa hawajamuona kuwa ni msomi?

-Kama wanamkubali, wameanza lini?

Mkuu hippocratessocrates,
Sio elimu peke yake pamoja na utendaji wake wa kazi baada ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Nishati na Madini, alivyoibua madudu Tanesco, na sakata la Kampuni ya Puma Energy.

Alivyoweka wazi madudu ya Mhando, na madudu ya kamati ya madini.

Sidhani kama kuna ubaya wowote kwa wakazi wa Musoma Mjini kumuomba Prof. Sospeter Muhongo kugombea ubunge.
 
Last edited by a moderator:
Ni kweli nasikia muhongo aliahidiwa kuchaguliwa endapo atagombea ubunge,lakini kwa sharti moja tu.inasemekana mara baada ya kuteuliwa kuwa waziri,alienda musoma na kuwakusanya watu ambao ni maarufu.akawaambia alitaka wafahamiane na wajadili namna ya kusaidiana ili waiendeleze musoma.lakini aliulizwa kwa nini alijitokeza wakati huo kwani walikuwa hawamfahamu.alisema ameona arudi kuwatumikia baada ya kukaa nje ya musoma kwa muda sana akiitumikia nchi kwa ujumla.watu walipombana sana alikiri kuwa angeweza kugombea ubunge baadaye.wakamuahidi kumpa.."lakini siyo kupitia chama hicho unachotaka wewe"akajibu kuwa,"naomba msiangalie chama,angalieni uwezo wa mtu".akajibiwa kuwa,"hicho chama kinaharibu hata watu......"
 
Sisi ni wakazi wa Musoma mjini hayo maombi tuliyatoa lini kama siyo kufikilia kwa kutumia masaburi yako wewe ulieanzisha uzi wa kimajungu kama huu kwanza ana ubavu wa kupambana na Chadema Musoma mjini usidanganye watu na kumpa kichwa huyo Muhongo wako pili hali ya hapa kila mtu anaijua kuwa hii ni ngome ya M4C
 
Wanabodi.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ambaye ni kada wa chama cha mapinduzi CCM ameombwa na wakazi Musoma Mjini kugombea ubunge jimboni humo mwaka 2015.

Profesa Sospeter Muhongo, ni msomi na mzaliwa wa Musoma Mjini wakazi wa mkoa Mara wanasema wakati umefika wa kumpa ubunge Profesa Muhongo, kutokana na elimu yake pamoja na uzoefu wake ili hawatumikie wananchi wa Mkoa wa Mara.

Jimbo la Musoma Mjini kwa sasa linaongozwa na chama cha Chadema kupitia mbunge wake Vicent Nyerere.

Wakazi wengi wa Musoma Mjini wanaoneka kumkubali zaidi Prof Muhongo, kutoka utendaji wake wake katika Wizara ya Nishati na Madini.
wakati nchi inaingia mikataba mibovu wasomi kama muhongo walikuwepo,elimu si kigezo pekee cha uongozi,wasira na usomi wake analala bungeni,endrew chenge na mikataba hovyo ya madini,acha uongo na kutapika ovyo ritz ! shame on you gamba mkubwa,NASIKIA HALAFU GAMBA LAKO LIMESHIKAMANA NA NGOZI KABISA!
 
Alisema ye ni mtendaji siyo mwanasiasa so km anataka kuangukia pua aingie kwenye kinyanga'nyiro cha kugombea
 
Back
Top Bottom