Wakazi wa DAR, tumelogwa na CCM? Kulikoni?

hiki kitu mkuu mshika chuma nimekuwa najiuliza kila siku! yani dar ambako wanajiita wameelimika ndowanatuangusha!
njoo arusha mkuu uwambie machalii ishu kuhusu ccm wanaweza kukupiga kabisa! juzi nilikuwa pale benki vijana wote wanaongea kuhusu kuipoteza ccm
lakini nyie bado mnakomaa nao nenda hata mwanza hadi watoto wa shule za msingi hawataki ccm! ila nyie ambao kuna vyuo vingi shule nyingi media nyingi bado mnakomaa na ccm tu! vijana wa dar wengi kazi kujisifu tu wakija mikoani! hawana lolote!
 
Yaani mkuu hujakosea kabisa! cha ajabu magazeti karibu yote yanatokea Dar,Radio nyingi ziko Dar na vituo vya Television vingi viko Dar....lakini
cha kushangaza bado wabongo wanaichagua ccm! shame on us kwakweli!
 
Tatizo vijana wa Dar ni kujiandikisha kwenye daftari wengi hawajajiandikisha pili wakina mama wauswazi wengi wanashabikia CCM ila ndo choka mbaya pia vijana wa Dar usharobaro mwingi lakini dhiki ndo zimewajaa sasa upinzani kutoka inakuwa ishu
Sawa mkuu....sasa wewe unaona kifanyike kitu gani kuwabadilisha hawa watu wa Dar akiwemo Dada Faiza Fox and com.?
 
Soma post#1 halafu fuatilia Igunga, halafu fuatilia nyuzi iliyoanzishwa na Regia uone anvyoidhihaki hijab. Halafu utajuwa namaanisha nini.
Mmh! hapa naona kuna harufu ya mambo ya udini....sasa haya mambo ya hijabu yametokea wapi tena? Dada Faiza huwezi kuongelea kitu bila hisia
za kidini? Ama kweli nakubali watu wa Dar tunamatatizo kumkichwa.....Faiza karibu hapa mtaa wa sikuu na kariakoo tule chipsi kuku if u dont mind pls!
 
Jamani tunachagua viongozi wetu baada ya kusikiliza sera, hivi ndivyo elimu ya uraia inavyosema na wala aisemi kuwa ni lazima kutoichagua CCM. Hata mfano wako unaweza ukawa unakubana maana hata vyama vilivyoangushwa madarakani kwa njia ya Demokrasia sio kama vinakosa kabisa uwakilishi katika bunge hivyo ni dhana yako yakiushabiki ndio inakutesa. Naweza Pia Kukusaidia Kuwa Imetokea Mara Nyingi tu ukakuta Diwani Na Mbunge Ktk Majimbo Tofauti Wakawa Sio Wa Chama Kimoja Jiulize Kwanini? Kinachotakiwa ni sera makini sio Uchama.
 
Mmh! hapa naona kuna harufu ya mambo ya udini....sasa haya mambo ya hijabu yametokea wapi tena? Dada Faiza huwezi kuongelea kitu bila hisia
za kidini? Ama kweli nakubali watu wa Dar tunamatatizo kumkichwa.....Faiza karibu hapa mtaa wa sikuu na kariakoo tule chipsi kuku if u dont mind pls!

Hizo wanakula wakuja (wasiokuwa na kwao Kariakoo) na wavivu wa kupika na walevi wanaorudi kujirusha saa tisa za usiku. Nani akale chipsi za Dulla, aaahhh babu nyumbani nna jiko spesho la kukaanga chipsi bila mafuta, zinatoka nyeupeeee, mambo ya "steaming" ukizibandika wee sahau, ingia JF kalumbane huko na kina Regia ukipumzika unazikuta tayari, kavuu, jiko limejizima na moto zinajipasha. Halafu ile kechap yao ya rangi ya pinki? Khaaa, usinchafuwe roho. Kama sina kechap si bora nijikatie katie nyanya freesh (hapo hapo ukifika Mkunguni na Sikukuu si unaona mboga mboga zinapatikana saa 24) kuliko kula hiyo mi kechap ya kwa Dulla.

Haaaa nna kwetu babu wee, utansameh sana lakini hapo sili, Unanchekesha!
 
Tatizo watu wa dar wanajifanya wako bize sana eti hawana muda na siasa ,mi wananiniboa sana.Lakini sehemu za Uswazi ndo zinaturudisha nyuma kwa hapa Dar maana ndo sehemu CCm wanaposhinda sana.
 
Tatizo watu wa dar wanajifanya wako bize sana eti hawana muda na siasa ,mi wananiniboa sana.Lakini sehemu za Uswazi ndo zinaturudisha nyuma kwa hapa Dar maana ndo sehemu CCm wanaposhinda sana.
Mkuu wewe ni mtu kama wa kumi hivi kwenye post unaongea the same thing kuwa mtaji wa ccm hapa Dar ni watu wa uswahilini.
Lakini inakuwaje watu kama hao na maisha yao ni magumu sana wanaichagua ccm tena? tatizo ni nini hapo?
 
Hizo wanakula wakuja (wasiokuwa na kwao Kariakoo) na wavivu wa kupika na walevi wanaorudi kujirusha saa tisa za usiku. Nani akale chipsi za Dulla, aaahhh babu nyumbani nna jiko spesho la kukaanga chipsi bila mafuta, zinatoka nyeupeeee, mambo ya "steaming" ukizibandika wee sahau, ingia JF kalumbane huko na kina Regia ukipumzika unazikuta tayari, kavuu, jiko limejizima na moto zinajipasha. Halafu ile kechap yao ya rangi ya pinki? Khaaa, usinchafuwe roho. Kama sina kechap si bora nijikatie katie nyanya freesh (hapo hapo ukifika Mkunguni na Sikukuu si unaona mboga mboga zinapatikana saa 24) kuliko kula hiyo mi kechap ya kwa Dulla.

Haaaa nna kwetu babu wee, utansameh sana lakini hapo sili, Unanchekesha!
Mmmh....Dada Faiza unamipasho wewe! khaaa! yaani unasound kama wale wamama wanaoishadidia ccm huku wakiwa kwenye rangi za njano
na kijani.....anywayz sisi wengine tuko single thatz'y tunakula hapa kwa Dulla....na washikaji waliowengi kuanzia mitaa ya msimbazi,Amani,Living
stone,Udowe,Kariakoo,Mafia,Swahili,Tandamti,Mkunguni na Aggrey karibia wote walikuwa CCM, lakini kwa kuja kwangu kula kila siku hapa kwa Dulla
nimefanikiwa kuwashawishi kwa hoja mzito kuhusu madudu ya ccm....nashukuru wote wamenielewa na hivi tuko mbioni kuanzisha shina la chama
fulani hapa mtaa wa Sikukuu na Mafia
 
Hatudanganyiki hii thread yakufikiria kwa njia za Masaburi. Dar yetu imetulia na katu chama pinzani hakiwezi igusa dar kwani wanajua ni moto.

Kama unataka mageuzi hama Dar yetu na nenda uko utakako na watu km ww Dar hii mmehamia tu sio wakazi wa mji huu, ondokeni Dar mrudi makwenu.

Nahisi wewe ni kichaa kwani ubungo na kawe sio Dar? mbona wanatawala CDM?
 
Inaonysha marafiki zako wanapata shida sana na sidhani kama una rafiki ambaye unaweza kuongea nae akakuelewa. Watu wa kaskazini sio wenzio wale wameenda shule na wamekaa darasani sio kama wewe mawazo yako yapo kwenye pilau.

Na ndio maana wasomi hao wa st st wakajiunga pamoja kuanzia Chadema Co Ltd na baadae kuisajili kama chama cha siasa lakini kikiwa na malengo yale yale.

nakupa pole.
 
hiki kitu mkuu mshika chuma nimekuwa najiuliza kila siku! yani dar ambako wanajiita wameelimika ndowanatuangusha!
njoo arusha mkuu uwambie machalii ishu kuhusu ccm wanaweza kukupiga kabisa! juzi nilikuwa pale benki vijana wote wanaongea kuhusu kuipoteza ccm
lakini nyie bado mnakomaa nao nenda hata mwanza hadi watoto wa shule za msingi hawataki ccm! ila nyie ambao kuna vyuo vingi shule nyingi media nyingi bado mnakomaa na ccm tu! vijana wa dar wengi kazi kujisifu tu wakija mikoani! hawana lolote!

Kwani walioenda shule wote ni Chadema? Na katika mkoa wa Arusha ni majimbo mangapi ya uchaguzi Chadema wamechukua mpaka useme Arusha wote ni chadema?

Fikiri kabla kuropoka barazani.
 
Na ndio maana wasomi hao wa st st wakajiunga pamoja kuanzia Chadema Co Ltd na baadae kuisajili kama chama cha siasa lakini kikiwa na malengo yale yale.

nakupa pole.
Barubaru, ninawasiwasi na mfumo mzima wa akili yako!.....hivi unajiona uko sawa kumkichwa?
 
Tatizo watu wa dar wanajifanya wako bize sana eti hawana muda na siasa ,mi wananiniboa sana.Lakini sehemu za Uswazi ndo zinaturudisha nyuma kwa hapa Dar maana ndo sehemu CCm wanaposhinda sana.

Ni kweli hayo unayosema watu wa dar wengi vilaza,wanachowaza kujirusha kwa sasa vilio kila kona hapa maisha mgumu
 
Sometime huwanawaza kwanini wakazi wa Dar-es-salaam tusiwe chachu ya mabadiliko tunayoyataka? Maana utakuta tunapiga
keleleweeee lakini mwisho wa siku tunaichagua ccm! Hasa wakazi wa ILALA na KINONDONI' kwanini jamani? Tumelogwa? Hakika
haiingii akilini tunazidiwa na hata watu wa mikoani na vijijini?

Tena huko watu ndiyo wamelala na hawana mwamko au mtazamo kama sisi wakazi wa Dar....iweje watu wanaokaa nje kidogo tu ya jiji letu kama Kawe, Ubungo na hata Tabata Segerea hawataki kusikia kitu kinachoitwa CCM, sasa inakuwaje sisi wakazi tunaoishi majimbo ya katikati ya mji (Ilala na Kinondoni) tumeichagua CCM kwenye ucha guzi uliyopita?

Yaani nadiliki kusema hata kesho itokee uchaguzi wa ghafla Kinondoni au Ilala kama ilivyotokea Igunga basi utaona watu wanaichagua
ccm kwa kura za kishindo!. jamani tatizo ni nini? tumelogwa na ccm hii iliyotunyonya kwa miaka 50 na kutulaza na giza kila siku?

Hebu tazama wakazi wa Mwanza,Mbeya,Arusha,Shinyanga mjini,Iringa, Lindi mjini,Moshi mjini na vijijini,Singida vijijini,Mbozi nk huko
kote hawataki tena kusikia kitu kinachoitwa ccm. Sasa iweje sisi tunaojiita wajanja wa mjini (wabongo) kila uchaguzi tunaichagua ccm?

Makao makuu ya Chadema yako jimbo la kinondoni lakini cha ajabu ccm ndiyo inatawala hapo. Makao makuu ya NCCR yapo Ilala lakini
cha ajabu ccm ndiyo inatawala hapo. Makao makuu ya CUF yapo Buguruni lakini cha ajabu ccm ndiyo inatawala hapo. Jamani kulikoni?

Yaani makao makuu ya vyama vyetu yapo milangoni kwetu na tunaona kabisa hawa viongozi wetu wa vyama vya upinzani jinsi wana
vyopambana na kutuelimisha....lakini bado mwisho wa siku tunaichagua ccm. Jamani wabongo tuna nini kwenye vichwa vyetu?

Mageuzi ya kuindoa KANU yalianzia Nairobi, mageuzi ya kumuondoa Keneth Kaunda na sasa Rupia Banda yalianzia Lusaka, mageuzi ya
kumuondoa Ghabo wa Ivory coast yalianzia Abdijani, mageuzi ya kumuondoa rais wa Tunisia yalianzia Tunisia, mageuzi ya kumuondoa
Mubarak wa Egypti yalianzia Cairo na mageuzi ya kumuondoa Gaddafi wa Libya yalianzia Tripoli na baadae Beghazi.

So kuna waliotoka kwa sanduku la kura na kunawaliotoka kwa kufukuzwa na wananchi. So all in all mageuzi yalianzia miji mikuu na kusambaa miji midogo.

Lakini kwa hapa Tanzania mambo ni tofauti kabisa! watu wa mji mkuu wamelala usingizi mfano wa pono....yaani wanatushinda hata wakazi
wa mikoani na vijijini? Hebu angalia kilichotokea Igunga' CCM imetokea kwenye tundu la sindano, chupu chupu ing'oke!

Yaani ilikuwa tia maji tia maji mtu (ccm) isikate roho pale Igunga. Je wakazi wa jiji la Dar ukiondoa Kawe na Ubungo, tuna matatizo gani? tumelogwa na CCM? Au kunatatizo ambalo limejificha mie sijui? Kwa nini tusiwe kioo cha mageuzi kwa faida ya watanzania wote?.

- Nawasilisha
Wanapiga kura kama vipofu, halafu wanalalama kama vichaa!
 
Mkuu mimi nipo jimbo la Ilala....tena city center kariakoo na kuna miundombinu mibovu usipime! maji yanatoka kwa wiki mara moja tena ni usiku
lakini watu wanaipenda ccm maeneo haya usipime! hata huwaelimishe vipi hawasikii!

Wajanja wa mjini hawadanganyiki.....TMK tulishawahi kuichagua NCCR, baadae tukawachagua CUF(Kigamboni), lakini wote wakatuzingua tu!!
 
Ni kweli hayo unayosema watu wa dar wengi vilaza,wanachowaza kujirusha kwa sasa vilio kila kona hapa maisha mgumu

Nini dar kama dar bwana; hebu niambie wewe......hivi karatu kwa baba enu slaa na maji matitu (mbagala ndani ndani) ni heri ya wapi?
 
Kwani walioenda shule wote ni Chadema? Na katika mkoa wa Arusha ni majimbo mangapi ya uchaguzi Chadema wamechukua mpaka useme Arusha wote ni chadema?

Fikiri kabla kuropoka barazani.

Tatizo la wapwa, hata kata moja ikichukuliwa na CDM, basi wao watasema mkoa mzima CDM inatisha. Arusha ni mkoa mkubwa sana; lakini mbwembe za CDM zinaishia pale town na karatu pekee!!! Na siku Slaa akija kukengeuka na kuhamia chama kingine; karatu nayo itafuata the same direction.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom