mshikachuma
JF-Expert Member
- Dec 2, 2010
- 2,853
- 626
- Thread starter
- #21
Mkuu Spencer, ahsante kwa uchambuzi wako ulioenda shule! hakika nimekuelewa vizuri sana kuelekea kwenye mageuzi ya kweli.GreatThinkers,
Tatizo la Dar ni lile kundi linaloyumbishwa na Si Si Em.
Hilo kundi halina, lakini pia njaa kwa watu Dar imezidi.
Watu hawajifikirii unaishi kwa kutafuta nauli na kula tu, ila unangoja dili la wizi ndio ujenge au ufanye kitu xha maendeleo.
Nimekaa Dar miaka 15 naijua vizuri sana Temeke walianza Temeke miaka ie Mrema akawa Mbunge baada ya hapo ikawa kimya hadi hivi majuzi.
Mnamkumbuka Kitwana Kondo 'KK' aliwatukana wanakigamboni kuwa niliwapa Pilau langu baada ya hapo Kigamboni ikamchagua Mbunge wa CUF?
Tatizo la Dar ni njaa na watu kuwa Bize wakizani watapata unafuu wa Maisha, Maisha haya hayawezi kuwa nafuu bila huu mfumo wa kulindana kuuondoa.
Niwape mfano mdogo: Hapa Mwanza kivuko cha Busisi Mkuu wa wilaya ya Geita ndiye aliyepewa tenda ya kuwa mama Ntilie ndani zile Feri mbili za Serikali?, Je, Mnafahamu nani kawakusanyia ushuru hapo Dar akiwa na Kampuni Tanzania Parking Solutions "TPS" ahaa Kinguge, na Je- wajua kwanini UDA imepigwa mnada, Je unadhani kuna nini wanataka kule kurasini? Yard Ya Makontena ili kina Masaburi wale Mihela!
Siwalaumu, ila ngoja tutwasaidia kuwaondoa hawa wezi. Vijana tuliosoma baadhi tumerudi Kanda ya ziwa tuna mkakati wa kutosha kuiondoa Si Si Em na itaondoka 2015.
2015 Wataiba kura lakini hazitatosha.
Wilaya karibu zote za Shinyanga Si SI Em haina chake ispokuwa kuna sehemu moja inatatizo, nalo tumeshaliona Dawa yake inaandaliwa ili tuanze na uchaguzi wa mitaa kwanza.
Tumewasukuma vya kutosha na sasa tumefika Igunga, huo ni koa wa Tabora ambao haujawahi kuwa na Mbunge wa Upinzani, Hivi majuzi it was neck to neck, Si Si Em mbinu yao tushaipata.
Lakini wewe kwa mtizamo wako wakazi kama wa jimbo la Ilala wanaweza kubadilika kweli? maana Ilala yule mbunge wao ZUNGU wanamuona
kama mungu mtu! yaani wanamtukuza huyo Zungu kushinda hata nyerere!. Wewe unafikiri kifanyike nini ili kuwaamusha wakazi wa Ilala?