Wakati umefika sasa kwa uongozi mzima wa Simba ujiuzulu kupisha wengine

SAYVILLE

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
5,151
7,916
Kelele na malalamiko yamekuwa mengi kwenye klabu ya Simba. Kuanzia kwenye masuala ya usajili wa wachezaji, matokeo uwanjani, malalamiko ya kuonewa ndani na nje ya uwanja, hadi utendaji wa kila siku wa klabu kote huko malalamiko yamekuwa mengi mno.

Kwa muda sasa Simba imekuwa inahangaika huku na huko kutafuta viwanja vya kuchezea mechi zake na msimu huu pekee imebadili uwanja wake wa nyumbani si chini ya mara 4. Niliwahi kusema mara nyingi Simba imepoteza ushawishi ndani na nje ya uwanja na lawama zote zinaangukia kwa uongozi. Niliwahi kusema Simba inavyojipambanua kwa ukubwa wake, inatakiwa iweze kushinikiza kutumia uwanja wa Mkapa angalau kwa mechi chache za ligi, kuna watu wakanijibu wakifanya hivyo na timu nyingie itabidi zipewe ruhusa. Leo nimesikia mechi ya Azam vs Yanga imehamishiwa uwanja wa Mkapa wakati tuliambiwa uwanja umefungwa kwa mechi za ndani hadi October 2024 isipokuwa derby ya Simba vs Yanga pekee. Inakuwaje hili limewezekana? Ushawishi!

Naunga mkono hoja, twenzetu Rwanda ila tujiandae kufunguliwa kesi za uhujumu uchumi.
Simba imekaa kinyonge sana wakati mwingine. Hivi pamoja na kujipendekeza kote kwa wanasiasa, viongozi wameshindwa kushawishi mamlaka husika ili Simba iendelee kutumia uwanja wa Mkapa hata kipindi cha marekebisho?

Sasa hivi kumekuwa na kelele kuhusu ufadhili na ushawishi wa GSM kwa timu 6 za ligi lakini, jambo ambalo kuna wanaona linaweza kuashiria uwezekano wa upangaji wa matokeo kuisaidia Yanga. Haijalishi kama hilo jambo linaruhusiwa kisheria au ni kinyume cha sheria zilizopo, ila kama GSM wameweza kulifanya hilo ni kwamba wana ushawishi wa kutosha kwa mamlaka husika, hata kwa njia zisizo halali kuweza kulifanikisha. Ushawishi! Ushawishi! Kama mwenzio anafanya uhuni halafu na wewe una uwezo wa kufanya uhuni ila unajibalaguza, lazima itakula kwako tu.

Simba imejaribu kuiiga Yanga kwa kuweka ukaribu na wanasiasa mbalimbali. Kuna tukio kabisa lilifanyika la kufungua tawi la Simba Bungeni, klabu inaonekana kujipendekeza kwa hawa wanasiasa, hadi wakaweza kumualika Rais kwenye Simba Day. Haya yote yana faida gani kama mwisho wa siku klabu inaendelea kushuka viwango na kupoteza ushawishi nje ya uwanja? Inawezekana huu ukaribu kwa wanasiasa ndiyo unaivuruga timu maana inaonekana sasa kupata matokeo ya hovyo kimipango mipango tu.

Mimi nafikiri uongozi mzima kuanzia Management ya Imani Kajula, Bodi nzima chini ya Salim Abdallah na Mwenyekiti wa Klabu Murtaza Mangugu wote wanastahili kuachia ngazi ili watu wapya wenye maono na nguvu mpya waje kuokoa jahazi.
 
Nafasi ya simba na yanga kwenye siasa za nchi hii haziwezi kuzidiana hata kidogo na wala hutakuja ona serikali au wanasiasa wanaipendelea timu moja wapo eti kwa sababu ya ushawishi. Hili haliwezekani na ni unthinkable. Simba na yanga zinazidiana kuchezeana michezo michafu nje ya uwanja kwa mambo mengine eg kuibiana wachezaji, ushirikina, kutoleana siri kwa wapinzani nk, lakini sio kwa kuitumia serikali au wanasiasa. ila serikali inazitumia hizi timu kwenye mambo yao kila inapohitaji kufanya hivyo.
 
Hakuna kisingizio cha GSM wala siasa. Shida ipo kwenye uongozi Wa Simba. Wanasajili wachezaji wa kawaida mnoo. Hv Chilunda aliyeachwa na AZAM ndiye asajiliwe kuisaidia Simba? Kina Kapama, Kyombo ndo viongozi waliwaona wanaweza kuipa Simba ubingwa? Km ni GSM mbona na Sisi tulikula 5?
Hawa Jamaa kina Mangungu waondoke tu. Hawawezi kututoa tulipo. Tutakosa ubingwa ht mara 10 tukiendelea na hawa watu. Hawaoni aibu Wala uchungu na Simba yetu.
Hata ukimleta kocha mzuri vp, lkn km wachezaji wenyewe ndo wale, atafungwa Hadi achanganyikiwe. Ingekuwa kwa uwezo wangu, wachezaji wa kigeni nngebakiza 4 tu. Nyuma Che Malone na Inonga, Kati Chama na Ngoma Basi. Wengine wote timulia mbali..
 
Simba watu wa ajabu saba, kwa nini waliomwondoa CEO Barbra?

Sasa hivi timu hovyo hovyo kuanzia uongozi mpaka uwanjani.

Usajili wa hovyo, usimamizi mbovu, timu wamemuachia Ahmed Ally.
 
Yaani inatia uchungu sana. Sijui hata tufanyeje. Kila mechi timu inastruggle, uhakika Wa ushindi hakuna. Tutaaibika tena tutakapokutana na Utopolo. Siku hiyo mm uwanjani siendi. Nitasikilizia kwenye Radio. Ht Tv siangaliii. Ni ujinga mtupu.
 
Wameishiwa mbinu kabisa. Bahati mbaya wabongo huwa hawana mshipa wa aibu, kwa sababu ya kuwaza matumbo yao. Busara ni kuondoka, wasipofanya hivyo mashabiki tuungane tuwafukuze
 
Suala la uongozi pale Simba ni changamoto kubwa sana! Sijui viongozi kwanini wasitumie tu busara kuachia ngazi! Wana Simba wapo wengi ambao wanaweza kuongoza vizuri!

Timu inazidi kupoteza ushawishi kila msimu,matokeo yake timu itakuja kukosa wadhamini wa uhakika na hata wakijitokeza watakuwa ni wale wa kuweka pesa ndogo.

Ukitizama kwa sasa mashabiki wengi wameweka mgomo wa kwenda uwanjani! Na hata kwenye mitandao ya club trending ya wanaopitia mitandao ya club imeshuka sana na hata kwenye app ya club ni almost zero mapato ni kiduchu sana.

Kwa faida ya club ni vyema viongozi wote kuanzia management chini ya CEO aliefeli kabisa, ndugu Iman kajura na bodi chini ya bwana Muhene (try again) na uongozi wa wanachama ndugu Mangungu kuachia ngazi kwa kulinda heshima yao na manufaa ya club yetu.

Kwa mwekezaji wetu! Tunajua kabisa utoaji wake wa pesa ni wa kusuasua sana! mpaka abembelezwe sana! Ni vyema ajitafakali nia yake kuwekeza Simba ilikuwa ni nini?! Kama ilikuwa ni kutafuta sifa na fame kwake na makampuni yake!
Tunamwambia imetosha na kwakua mchakato haujakamilika kwa asilimia mia, ni bora ajitoe mapema kabla hatujaanza mgomo mkubwa dhidi yake.

Maana hata malkia wa nyuki alijitaidi sana kusajili wachezaji wazuri kuliko hawa ambao wanakuja,ambao hawana hata sifa ya kuchezea Kagera sukari. Hatuoni manufaa yeyote ya yeye kuwepo Simba kwa hali hii ya mpaka abembelezwe kutoa pesa.

Marehemu Zakaria Hanspope (RIP) hakuwa mwekezaji lakini kwenye masuala ya Simba alikuwa serious sana,ndio maana wanachama wengi walitaka hizo asilimia 49 za muekezaji wa sasa, zigawanywe kwa watu wawili kama serikali inavyotaka!

Watu walipendekeza Hanspope achukue 25% na muekezaji wa sasa achukue 24% ila watu wachache wakatusaliti,haya maujinga ya kunyenyekea mtu mmoja yasingekuwepo.
 
Wameishiwa mbinu kabisa. Bahati mbaya wabongo huwa hawana mshipa wa aibu, kwa sababu ya kuwaza matumbo yao. Busara ni kuondoka, wasipofanya hivyo mashabiki tuungane tuwafukuze
Hili lingewezekana kama mngekuwa na umoja. Hawa wazee wawili wanatafuta 10% tu Kila manunuzi na mauzo ya Wachezaji.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom