Wadiz
JF-Expert Member
- Nov 10, 2022
- 5,417
- 11,083
Hello family,
Mods please tupeni fursa tuseme kweli, kweli inaponya.
Let speak the truth, the truth be told. Hakika nasema katika kweli hasira na chuki hasa katika mawanda ya ndoa si bure kuna chanzo, wengi wa wanaokataa ndoa na kuoa ni wahanga wa kuumizwa kihisia na kuharibiwa malengo hasa dhamira ya dhati ya kuwa na wenza wao au wapenzi wao katika kusudi la kudumu. Hivyo basi kuishia kupoteza tumaini na Imani ya kweli katika kupata mtu wa kweli na aliye sahihi kuishi nae kwa lengo la kudumu kama mke na mume.
Baadhi yetu tuliachwa na kusemwa vibaya kwa kejeli, matusi, dharau, wengine katika kadamnasi, heshima ilikufa kabisa.
Katika Hali ya kukosa tiba ya vidonda hivyo mbalimbali kwa vyanzo na matukio mbalimbali tumejikuta ni watu katili sana sana kihisia hatuogopi kuwa peke yetu, hatujali chochote kitu, na hasa pale unapokuwa na fimbo ya pesa ya kufanya chochote ni balaa.
Nawahusia vijana, mabinti, wanawake kwa wanaume weka akiba kwa kila jambo, timiza wqjibu mfahamu mpenzi wako kwa historia kila alipopita muulize ongea nae. Ipo siku atabadirika je wewe utakuwaje umejiandaa vipi kupokea kuachwa au kuachika.
Mapenzi ni amani, mapenzi ni chuki, mapenzi ni furaha, mapenzi ni hudhuni, kuna hisia, kuona na kusikia vyote vyetu.
Niwakaribishe kwenye ushuhuda na simulizi.
karibuni
wadiz a.k.a Baharia