dudus
JF-Expert Member
- Feb 28, 2011
- 22,126
- 49,385
- Thread starter
- #21
"Chombo hicho ambacho tumekubaliana kitaitwa Jukwaa la Katiba la Waislamu, kitakuwa na jukumu la kuhakikisha Waislamu kote nchini wanakuwa na kauli moja juu ya masuala yanayohusu dini na maisha yao ambayo wangependa yawemo kwenye katiba mpya", alisema.
Hapo kwenye red inanipa tabu:-
Chombo hicho kitaitwa JUKWAA LA KATIBA LA WAISLAMU
Kitahakikisha Waislamu wanakuwa na kauli moja juu ya masuala yanyohusu DINI ambayo wangependa YAWEPO KWENYE KATIBA
Kitahakikisha Waislamu wanakuwa na kauli moja juu ya masuala yanyohusu MAISHA YAO ambayo wangependa YAWEPO KWENYE KATIBA
KATIBA inayozungumziwa hapa sio ya BAKWATA au Taasisi nyinge ya Kiislamu bali KATIBA YA NCHI. Ni lazima kuwa makini baadhi yetu wanapoanza kutaka DINI ZAO ziwepo kwenye KATIBA.
Kwenye suala la MAISHA kila mtu anahitaji maisha bora kwanini mjadala usijikite kwenye MAISHA YA WANANCHI WOTE badala ya MAISHA YA WAISLAMU TU? Nashindwa kuwaelewa hawa jamaa.