Waislamu wazindua Jukwaa la KATIBA

Prof Shivji na Baregu wameipinga hii sheria tangia mwanzo na ndiyo maana walionyesha hata ujasiri wa kuipinga live kwenye tv. Hawa mashehe nao waliipinga hiyo sheria? Laiti ungeona zile kanzu, baraghashia na hijabu zilivyokuwa zinashangilia JK alipokutana na wazee wa dar. Mimi binafsi zaidi ya wewe sijaona muislam mwingine akiipinga hii sheria kandamizi. Ndiyo maana watu wanahoji busara ya hawa viongozi wenu wa dini iko wapi maana wanataka kuvunja sheria waliyoishangilia .
Sweke acha Ujinga mkuu wangu umesoma kama unavyojiita.. Swala la Muswada ambalo JK ndiye aliwaita wazee wa Dar kuwezi kulilinganisha na Sheria iliyopitishwa. CCM ina wabunge wengi wakristu na ndio walioandika na waliopitisha muswada huo Bungeni wakiongozwa na Anna Makinda, sasa unataka nambia ilikuwa swala la Wakristu?..

Pili Kanzu ni vazi hata rais wa Nigeria huvaa kanzu kinakushanga kipi?..Mbowe alivaa kanzu siku ya Idd cha ajabu nini?...Kwani hiyo Katiba ni ya Waislaam au wazee wa Dar mbona mnazidi kuonyesha ujinga wenu jamani shule gani mlokwenda?

Halafu maswala ya Katiba sio maswala ya msikiti bali Masheikh wanachoweza kufanya ni hatua kama hii ambayo mawazo ya wananchi yanatakiwa. Kupinga ama kukataa kila mmoja ana maamuzi yake isipookuwa pale swala linahusu Institution ndipo Masheikh wanaweza kuingia... Ya kaizali tunamwachia yeye ila pale ya kiimani yanapotakiwa ndipo Masheikh huingilia.. Elimu nakupa uujue Uislaam ambao Yesu katufundisha...
 
katika vitu vinavyo nitia kichefu chefu ni kuona watu tukijadili udini zaidi katika kila swala. Yani sasa hivi watanzania badala ya kufikiria mambo kiundani zaidi tunafikiria kkuhusu udini na kila jambo tuna relate na dini.
Tunakoelekea siko tutaishia pigana mapanga huko mbeleni.
Rai yangu ni kwangu tubadilike jaman penye ukweli acha uwe ukweli.
 
mi najua hawatafanikiwa sababu ni moja tu...hawapo organized. makanisa yote yana viongozi wao wa juu na ambao wanaheshimika wanapotoa kauli na mara nyingi kauli zao hua ni majumuisho ya critical thinkers wa kanisa na mara nyingi kila baada ya tamko la hawa wakanisa hufatwa na la waislaam, maana yake ni nini?? maana yake ni kwamba wakristo ndio huibua hoja au hoja watoazo wao ndio hua mwiba mchungu kwao.

my suggestion: wajipange kwanza kiuongozi na wawe wanaheshim viongozi wao. sio makundi kila sehemu....wakristo huwa hawafanyi hii kitu wenyewe huwaachia maaskofu, na baraza lao hua lina watu 10 au 15 lakini hoja na mapendekezo yatokayo hapo hua ni nzito na zenye mantik.

kuna wakristo wengi hawana maaskofu, wakristo pia wana makundi mengi tu na sijawahi kusikia wametoa kauli yao ya jumla kama wakristo
 
Haki ya Kwanza, wapewe Jukwaa la Kukutana na Rais Ikulu kama "Wenzao" ili kusiwe na upendeleo!

This is a wrong approach.... siamini kama mashindano ndiyo njia sahihi.They need to be original wasiige kundi lolote katika kufanya yale wanayoona ni muhimu kwao.
 
hivi naomba niulize wakati Edward lowasa anasaini mkataba wa MOU wananchi au waislamu walipata nafasi ya kuulizwa kuhusu hayo makubaliano?na kama hawakupata nafasi ya kujadili kwanini wao wakipnga mambo yao munapinga?

Kama unataka pia waweza kuuliza hivi: Wakati Jakaya Mrisho Kikwete anawataka Waislam nao wapeleke ombi kusaini MoU yao, aliwauliza wananchi? Kwanza hilo takwa la kuulizwa unalitoa wapi? Ukipeleka ombi lako serikalini ni hiari serikali kukubali au kukataa.Siyo lazima serikali ikuulize wewe au mtu yeyote au kikundi chochote.

Ningependa kujua ni kwanini hadi sasa Waislam hawajachukua hatua hadi leo hii kusaini MoU yao na serikali?
Ni kikwazo gani kinawafanya wasipeleke document yao kusaini na serikali na badala yake wanalalamika tu na kutaka MoU ifutwe? Kuna nia njema kweli?
 
Mou kama ile ya Kanisa na serikali ni kinyume cha Katiba, Si vyema hata kwa waislamu kuingia Mou ya aina ile na serikali.
 
Mou kama ile ya Kanisa na serikali ni kinyume cha Katiba, Si vyema hata kwa waislamu kuingia Mou ya aina ile na serikali.

Mkuu badala ya kuongea tu kwa hisia, hebu fafanua. Ni kipengele gani hicho cha Katiba?
 
Hii thread imekula vichwa vya watu wengi sana..........jana ilikuwa moto na naona pages zimepunguzwa na MODS
 
wacha unafiki ulivyokuwa na kiherere cha kuvamia mambo usiyo yajua eti mahakama ya kazi usivamie mambo soma kwanza mambo yaliyoandikwa kabla yakuvamia mambo usiyo yajua wacha ushabiki hapa hayazungumzwi mambo ya simba na yanga
 
wacha unafiki ulivyokuwa na kiherere cha kuvamia mambo usiyo yajua eti mahakama ya kazi usivamie mambo soma kwanza mambo yaliyoandikwa kabla yakuvamia mambo usiyo yajua wacha ushabiki hapa hayazungumzwi mambo ya simba na yanga

Kama unataka pia waweza kuuliza hivi: Wakati Jakaya Mrisho Kikwete anawataka Waislam nao wapeleke ombi kusaini MoU yao, aliwauliza wananchi? Kwanza hilo takwa la kuulizwa unalitoa wapi? Ukipeleka ombi lako serikalini ni hiari serikali kukubali au kukataa.Siyo lazima serikali ikuulize wewe au mtu yeyote au kikundi chochote.

Ningependa kujua ni kwanini hadi sasa Waislam hawajachukua hatua hadi leo hii kusaini MoU yao na serikali?
Ni kikwazo gani kinawafanya wasipeleke document yao kusaini na serikali na badala yake wanalalamika tu na kutaka MoU ifutwe? Kuna nia njema kweli?
Hivi wewe unadhani JK ana say yoyote pale alipo huo ni mfumo ambao yeye ameukuta kwahiyo hana uwezo wowote wakuutoa na uliyeuwekea supa glue huo mfumo alishatangulia huko kwenye haki ya ukweli hapa ameacha vibaraka wake ambao wanamtunukia cheo cha mwenye heri kwasababu amewaeka juu na siku zote ukimkuta mbwa juu ya mti ujue kapandishwa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Mou kama ile ya Kanisa na serikali ni kinyume cha Katiba, Si vyema hata kwa waislamu kuingia Mou ya aina ile na serikali.

Kifungu gani hebu tujuze!
Wakristo kuingia MoU hawakuingia ili kulinufanisha kanisa bali kuwanufaisha watanzania bila kuwabagua kwa dini zao.Kwa msingi huu hakuna DINI.Nyie mnachotaka ni mambo yenu ya dini yenu yanayowabagua watu wa dini nyingine ,yaingizwe kwenye mifumo ya serikali isiyo na dini!
 
Mbona unamtukana Rais wetu tena Muislam jamani???
Hivi kama mna mtizamo huu, kuna kitu mtapata? Je angekuwa rais mkristo mngesemaje?
Acheni kujiweka nafasi ya VICTIM kila siku.

Sweke acha Ujinga mkuu wangu umesoma kama unavyojiita.. Swala la Muswada ambalo JK ndiye aliwaita wazee wa Dar kuwezi kulilinganisha na Sheria iliyopitishwa. CCM ina wabunge wengi wakristu na ndio walioandika na waliopitisha muswada huo Bungeni wakiongozwa na Anna Makinda, sasa unataka nambia ilikuwa swala la Wakristu?..

Pili Kanzu ni vazi hata rais wa Nigeria huvaa kanzu kinakushanga kipi?..Mbowe alivaa kanzu siku ya Idd cha ajabu nini?...Kwani hiyo Katiba ni ya Waislaam au wazee wa Dar mbona mnazidi kuonyesha ujinga wenu jamani shule gani mlokwenda?

Halafu maswala ya Katiba sio maswala ya msikiti bali Masheikh wanachoweza kufanya ni hatua kama hii ambayo mawazo ya wananchi yanatakiwa. Kupinga ama kukataa kila mmoja ana maamuzi yake isipookuwa pale swala linahusu Institution ndipo Masheikh wanaweza kuingia... Ya kaizali tunamwachia yeye ila pale ya kiimani yanapotakiwa ndipo Masheikh huingilia.. Elimu nakupa uujue Uislaam ambao Yesu katufundisha...
Kwanza sijawahi kujiita nimesoma...ila nina uelewa na exposure ya kutosha kuweza kufuatilia mijadala na kuelewa mijadala mingi(japo si yote) humu jamvini. Bado nina safari ndefu mpaka niweze kujiita mwenyewe msomi.
Suala la muswada nalifananisha na sheria kwa sababu JK aliutetea huku akishangiliwa na alionesha nia yake ya kwenda kuusaini huo muswada. Wabunge waliopitisha muswada ni wa CCM - CUF (wakristo,waislam n.k) kwa maslahi yao wenyewe siyo ya watanzania wote. Sawa kila mtu ana haki ya kupinga au kukubali lakini mkuu utakuwa ni mjinga sana kama hautakubali kuwa waislamu wanatumika kupunguza nguvu ya kuipinga hii sheria kandamizi. Ni wewe Mkandara ndiyo huwa unashangaa waislamu wenzako wanaopinga mfumo kristo lakini ni haohao ndiyo wa kwanza kuichagua na kuitetea serikali inayoendeshwa na mfumo kristo eti kwa sababu rais ni muislam. Kwenye hili la sheria kandamizi waislam wanatumika tu kama kule Igunga kupitisha mambo ya CCM. Siyo wewe mkandara uliokuwa unabishana na akina Topical waliokuwa hawaoni ubaya wa huu muswada/sheria? Ndiyo ma ana nilishasema huko nyuma kuwa waislam wanahitaji viongozi wa kiroho wenye elewa na msimamo kama wewe siyo hawa jamaa tunaowaona vijiweni wasiokuwa na elimu dunia ya kutosha. Ukiondoa suala kiimani, waislamu wengi wameshindwa kupata busara kama hizi zako kutoka kwa viongozi wao wa dini badala yake wanaambiwa 'uislam kwanza' na matokeo yake ni kusupport kila kila kitu kinachotoka kwa muislam hata kama kitawaumiza na wenyewe pia. Ukiwauliza waislam kwanini Cardinal Pengo alisikitika Kikwete aliposaini huu muswada ,watakuambia kwasababu JK ni muislam. Hawajiulizi kwanini Pengo anapinga sheria inayohakikisha serikali inayoendeshwa na Kanisa(mfumo kristo) itawale milele..! Anyway...tusubiri yatakayojiri kwenye kongamano hilo..! Nimeandikia simu , samahani kama sitasomeka vizuri.
 
Mkuu ndivyo nilivyofundishwa mimi kuwa karibu na watu hawa ili niwape elimu maana hata dini zimepelekwa kwa wajinga.. Kama ingekuwa kwa jinsi unavyofikiria wewe basi hata huo Uislaam usingefika Afrika au Tanzania maana sisi wote tulikuwa makunguru, wakaja majoroe kutufundisha kuimba na kujenga viota..Leo Alhamdulillah Uislaam umefika.

Mkandara
Asikuumize mtu kichwa Uislamu ni dini ambayo haina shaka yeyote na wala hakuna atayeiondoa, kila mtu ana imani yake ukiona mtu anakashifu dini ya mwenzake basi jua fika hata hiyo yake haijui. Ukimsikia limbukeni anaihusisha Chadema na Ukristo huyo bahau achana naye; tangu lini dini na siasa vikajichangana?

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Mou kama ile ya Kanisa na serikali ni kinyume cha Katiba, Si vyema hata kwa waislamu kuingia Mou ya aina ile na serikali.

Sawia kabisa.
Huo ni ufisadi mwingine tena huu ni mbaya zaidi kwani unahusisha imani za kidini. Ni khatari kubwa sana kwa mustakabali wa nchi yenu.

Kwani kazi za imani za kidini ni kukemea na sio kuongoza katika maovu.
 
Kifungu gani hebu tujuze!
Wakristo kuingia MoU hawakuingia ili kulinufanisha kanisa bali kuwanufaisha watanzania bila kuwabagua kwa dini zao.Kwa msingi huu hakuna DINI.Nyie mnachotaka ni mambo yenu ya dini yenu yanayowabagua watu wa dini nyingine ,yaingizwe kwenye mifumo ya serikali isiyo na dini!

Je una uhakika wa unachokisema.
Je unaijua Mou yenyewe na unajua kanisa linakwapua kiasi gani toka katika Serikali masikini ya Tanganyika.

MOU ya Kanisa na Serikali ilifungwa mwaka 1992 na Fisadi EL. Kila mwaka makanisa yenu yanapata Billioni 60 (sasa hivi yanapata Billioni 91) .

Toka 1992- 2011 ni miaka 19= 60,000,000,000 x 18 + 91,000,000,000= Trilioni 1.17 or Trilioni 1.2. Kutoka katika kodi za WATANZANIA.

Jiulize kama Serikali ingekuwa kila mwaka kutokana na pesa hizo ingekuwa inajenga hospitali 2 na labda chuo kimoja na secondari 3. Je sasa ingekuwa imefikia wapi?

Kwanini wazidi kukodi kwa kanisa? Kwa mwenye akili timamu atajiuliza kama kanisa waliweza kujenga kwanini washindwe kuviendeleza?

Kazi ya JK hiyo udini unashika kasi! yani mchezo mchezo hivi hivi tutaanza kutwangana waislamu kwa wakristo JK na familia yake haoooo oman na mali zetu walizopora! chonde chonde ninyi mashekh wapenda tende na wali hayo mnayoyafanya siyo dini inavyotaka kwa sababu Uislam ni utawala uliokamilika... hauhitaji mfumu mwingine toka nje yake ili utawale vizuri i!! hizo ni njaa zinawasumbua na Kwa haki mnacheza na adhabu ya ALLAH! muda wa toba ni sasa rejeeni katika dini acheni huu utwahut!!
 
Hivi wewe unadhani JK ana say yoyote pale alipo huo ni mfumo ambao yeye ameukuta kwahiyo hana uwezo wowote wakuutoa na uliyeuwekea supa glue huo mfumo alishatangulia huko kwenye haki ya ukweli hapa ameacha vibaraka wake ambao wanamtunukia cheo cha mwenye heri kwasababu amewaeka juu na siku zote ukimkuta mbwa juu ya mti ujue kapandishwa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Fikra mfu hii!! daah!! Mbona nafasi ya kufanya hivyo anayo kubwa tuu! si ameanzisha mchakato wa katiba kiaina!! sasa hii si ndo njia pekee ya kurekebisha hali hiyo!! we vipi??
 
Back
Top Bottom