Waislam Dar wakutana Kidongo Chekundu, kulaani filamu ya kumkashifu MTUME

Status
Not open for further replies.

Bajabiri

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
9,730
1,201
Mchana huu waislam watakutana uwanja wa kidongo chekundu, kwa ajili ya kuonyesha hisia zao za kulaani kitendo cha wamarekan kuandaa filamu ya kumkashifu mtume.

Ikumbukwe kuwa haya si maandamano,ila waislam baada ya sala ya ijumaa watakua pale.

NB:
Katika ulimwengu wa kidemokrasia UVUMILIVU ni msingi muhim sana, kukashfu dini ya mtu si jambo jema, tujadili hoja kwa hoja.
 
katika hiyo filamu kashfa ipo wapi au kitu gani kinaonyesha kuwa Muddy amekashifiwa?. Kama hakuna jibu juu ya hilo maana yake ni kwamba kila kitu ukweli ndani ya filamu hiyo ila mnataka kuleta ulalamishi usio na maana. Waitazame kwanza hiyo filamu sio kukurupuka tu, halafu hayo maandamano wakafanyie huko waliporekodi huo mkanda.
 
............unaposemma waislamu wote unamaanisha kutoka katika kila mkoa au? Hapo kidonge chekundu eneo lake lina ukubwa gani??
 
nahisi sio wote wameona hiyo film, hapo mkumbo lazima uwepo ,ila tuwatakie kila la kheri kwenye dua na wakumbuke kusamehe pia sio kulaani tu!
maandano mema ndugu zangu!
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Wanabodi,

Nipo maeneo ya barabara ya Lumumba naona makundi ya Waislam wakielekea katika viwanja vya Kidogo chekundu huku gari za polisi wakiwa tayari kupambana na waandamanaji.

Hali sio ya kawaida tusubiri kitakachotokea.
 
wapambane nao kwa nn?
Wamewanyima wasifanyie jangwani hivyo wakaamisha eneo, sasa tatizo liko wapi?
 
Wanalaani filamu ambayo hawajaiona na imetengenezwa Califonia USA kuwa inakashifu dini yao.Jioni haohao ndio wanaopanda jukwaani kwenye mihadhara yao na kuweka maspika makubwa na kukashifu dini za wenzao.Tena sio kwa kuigiza kama filamu bali kwa viapo vya dini yao.Ajabu sana hii
 
Wanabodi,

Nipo maeneo ya barabara ya Lumumba naona makundi ya Waislam wakielekea katika viwanja vya Kidogo chekundu huku gari za polisi wakiwa tayari kupambana na waandamanaji.

Hali sio ya kawaida tusubiri kitakachotokea.

Kwa taarifa tu baadhi ya balozi zimetoa tahadhari kwa raia wake kuelekea maeneo ya mjini leo! sijui kunani kwakweli.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom