Wahuni Jeshini Wadhibitiwe haraka, Wanajeshi wafundishwe nidhamu ya kuishi na raia

Rashidi Jololo

JF-Expert Member
Sep 21, 2022
1,492
2,367
Kitendo cha serikali ya CCM kufumbia macho WAHUNI Jeshini waliojichukulia sheria mkononi na kupiga, kujeruhi na kuua raia wasio na hatia HAKIKUBALIKI asilani.

Tunafahamu ni kwa muda mrefu sasa majeshi yetu yote (Jeshi la wananchi, Polisi,Magereze n.k) yamekuwa yakitumika na serikali hii ya CCM kufanya vitendo vya KIHARAMIA dhidi ya wananchi hasa katika nyakati za Uchaguzi Mkuu, na pia kwenye UHUNI mwingine uliobatizwa kwa majina ya VIKOSI KAZI, OPERATIONS n.k Na hii ndio sababu serikali hii iliyoko madarakani kinyume na matakwa ya wengi imekua ikisua sua kuchukulia hatua WAHUNI wa namna hii katika Majeshi yetu yote.

Tunaitaka serikali ya CCM ichukue hatua haraka dhidi ya WAHUNI hawa haraka na pasipo kuchelewa, vinginevyo ukimya huu ukiendelea kutamalaki basi na ieleweke kwamba siku tutakapo anza kuishi kama WANAMGAMBO WA PALESTINA dhidi ya ISLAEL atakayetufikisha hapo ni hii serikali ya CCM.

Chuki iliyopandikizwa kutoka na vitendo vya hawa Wanajeshi WAHUNI ni kubwa sana, serikali ya CCM isijidanganye kwamba HUU NI UPEPO NA KWAMBA UTAPITA TU... Serikali ya CCM na mamlaka zake wachukue hatua haraka kabla wananchi hawajapata UJASIRI WA KUJIHAMI na WAHUNI hawa kutoka Jeshini, na hatimaye kusababisha mauaji ya wanaovalia sare za jeshiwanajeshi kuwa ni jambo la kusherehekewa na wengi.

Matendo ya ukosefu wa amani na utulivu katika nchi nyingi ni matokeo ya SERIKALI ZAO KUSHUPAZA SHINGO na kufumbia macho vitendo vya uonevu na kihalifu kama hivi.
 
Hii story ina mambo mengi sana nyuma ya pazia
Inaweza kuwa exaggerated sana
Kama ni kweli nashauri viongozi wakuu wa jeshi wakae na wananchi kawe kwa ajili ya ku solve hii ishu
 
Kitendo cha serikali ya CCM kufumbia macho WAHUNI Jeshini waliojichukulia sheria mkononi na kupiga, kujeruhi na kuua raia wasio na hatia HAKIKUBALIKI asilani.

Tunafahamu ni kwa muda mrefu sasa majeshi yetu yote (Jeshi la wananchi, Polisi,Magereze n.k) yamekuwa yakitumika na serikali hii ya CCM kufanya vitendo vya KIHARAMIA dhidi ya wananchi hasa katika nyakati za Uchaguzi Mkuu, na pia kwenye UHUNI mwingine uliobatizwa kwa majina ya VIKOSI KAZI, OPERATIONS n.k Na hii ndio sababu serikali hii iliyoko madarakani kinyume na matakwa ya wengi imekua ikisua sua kuchukulia hatua WAHUNI wa namna hii katika Majeshi yetu yote.

Tunaitaka serikali ya CCM ichukue hatua haraka dhidi ya WAHUNI hawa haraka na pasipo kuchelewa, vinginevyo ukimya huu ukiendelea kutamalaki basi na ieleweke kwamba siku tutakapo anza kuishi kama WANAMGAMBO WA PALESTINA dhidi ya ISLAEL atakayetufikisha hapo ni hii serikali ya CCM.

Chuki iliyopandikizwa kutoka na vitendo vya hawa Wanajeshi WAHUNI ni kubwa sana, serikali ya CCM isijidanganye kwamba HUU NI UPEPO NA KWAMBA UTAPITA TU... Serikali ya CCM na mamlaka zake wachukue hatua haraka kabla wananchi hawajapata UJASIRI WA KUJIHAMI na WAHUNI hawa kutoka Jeshini, na hatimaye kusababisha mauaji ya wanaovalia sare za jeshiwanajeshi kuwa ni jambo la kusherehekewa na wengi.

Matendo ya ukosefu wa amani na utulivu katika nchi nyingi ni matokeo ya SERIKALI ZAO KUSHUPAZA SHINGO na kufumbia macho vitendo vya uonevu na kihalifu kama hivi.
Vijana wa Ufipa mda wenu huu hampitwi na jambo
 
Ukweli lazima usemwe ndugu, serikali ya CCM imeyalea haya MAGENGE kwa maslahi yake binafsi. Siku matendo ya wananchi ya KUJIHAMI dhidi ya WAHUNI hawa yatakaposhamiri ASIWEPO mpuuzi yoyote wa kulaani huo mrejesho wake
 
Si Amir Mkuu wa Majeshi au CCM wanaoweza kulisemea hii hasa hasa hiki kipindi ambacho tunakaribia uchaguzi wa 2025!
Unajua tena bila Jeshi hakuna tena!
Kwa hiyo raia waendelee kuugulia maumivu tu,Mungu awasaidie!
 
Back
Top Bottom