Wahaya kutoa tamko kuhusu kuonewa kielimu baada ya uhuru

Ni system iliyowagusa wanyakyusa wahaya na wachaga kwa imani kuwa walikua juu kielimu and afta that quota system wachagga waliamua ku invest kwnye private schools and thats y in chaggaland shule zipo nyingi kule zaidi ya mkoa mwngine wowote.
 
Baada ya uhuru tumeshuhudia mtaala wa elimu ukipandisha alama za ufaulu kuingia sekondari kwa wakazi wa mkoa wa Kagera kwa kile serikali ilichokiita eti ni sera ya kuleta usawa kielimu Tanzania nzima.Kwa mfano wakati huo mkazi wa Kagera alipaswa kuwa na alama za ufaulu 90,mkazi wa eneo jingine aliweza kuchaguliwa kujiunga na sekondari kwa alama 40.Hii ni kinyume cha haki za binadamu(right to education).Evidence zipo naomba ndugu zangu tupeleke kesi hii ICC ili tutendewe haki.

Inasikitisha sana kama hii habari ni kweli! Mkuu ebu leta ushahidi kuhusu jambo hili. So sad!!!!
 
Ni kweli Wahaya waligandamizwa kutafuta usawa! Kuna kipindi wavulana nao waligandamizwa ili kuleta usawa kijinsia!
 
Tupe evidence mkuu, tuanze kuwashughulikia hao waliotubagua. Sikuwahi kuisikia popote hii kitu. Kama kweli patachimbika. Usishangae wahaya wakataka uhuru wao. Hata hivyo ziwa victoria lilishawawekea mipaka.
 
of course na sisi wahaya we have our problems.....wachaga wanashindana maendelea flan kajenga nyumba nzuri let me build a bigger and better house......mhaya ukipanda wahaya wenzio ndo bize kuku pull down,wenyewe wanasema...'wabilima tobilye'...tutafika kweli???
 
Ushirikiano wa wahaya naona uko zaidi katika uongeaji lugha yao,ila si katika maendeleo!!
 
This is fact 100%...mfano Bwiru boys was considered as a special school ambapo watu waliokua wanachaguliwa walipaswa kua na marks za juu sana na atleast kwenye hesabu upate 45/50 ndo uende pale na ilikua inachagua wanafunzi wa kanda ya ziwa mpaka Tabora..cha ajabu wanafunzi asilmia kubwa walikua ni wahaya tu mpaka staff nzima yani sisi ambao hatukua wahaya du kazi kweli kwani jamaa walikua wanadiscuss mpaka kwa kihaya na still nafasi zote za juu zilikua zao ata mtihani wa taifa yalipasua sana haya majamaa...mie nadhani serikali ilitumia busara kidooooogo manake wasingefanya hivyo ingekua nchi yao kwani nafasi zote nyeti zingekua zao...ata sasa check vyuo vikuu vyote wakufunzi wengi ni wao.....ila haikua haki kwa wale waliofelishwa makusudi
 
Si kihivyo; kwani wahaya wote wameisha????, we sema tu tulikandamizwa na tunaendelea kukandamizwa bila kujitambua: just imagine; mtu anayemaliza kidato cha 4 Kagera mwenye Div.4 akija Dar akarudia paper anatisha si mchezo; wapo wengi wamehitu Engineering na Sheria na wanafanya vizuri ktk soko la ajira.
Mkuu wangu tatizo hapo ni walimu wazuri,vifaa na mazingira mazuri ya kujisomea. Ndugu zetu Wachagga walipitia katika madhila kama yetu,lakini wao walijatambua na sasa wanazidi kusonga mbele kwa kasi,sisi tumebakia kulalamika! Tunapaswa kujitambua kwanza ndipo tuelewa uwezo mkubwa tulionao! Tumejaza wasomi,matajiri na watu wenye vipaji wengi waliotapakaa Dunia nzima. Viongozi wetu mfano wabunge wanawashirikisha vipi kuchochea maendeleo ya Bukoba? Leo nimeangalia Fund raising ya CDM ktk Startv Live toka Arusha. Nimejiuliza sisi kama Wahaya tunashiriki vipi ktk ukombozi wa pili wa nchi yetu? Tumebakia kulalamika bila kuchukua hatua! Wenzetu Kilimanjaro wabunge wao wanaulizwa na wapiga kura kula wao maji safi ya bomba na barabara za lami! Elimu,Hospitali,Umeme na Mawasiliano ya simu walikwisha maliza! Sisi wabunge wetu wanafanya nini? Kama siyo kuzinzia na kugonga meza?
 
Kama mnawachagua akina karamagi mnategemea nini?
 
Back
Top Bottom