Wahaya kutoa tamko kuhusu kuonewa kielimu baada ya uhuru

Wahaya kwa kujimegea bwana hamjambo!
Ngoma nayo iliwamaliza sana otherwise mngekuwa mbali sana!
 
Baada ya uhuru tumeshuhudia mtaala wa elimu ukipandisha alama za ufaulu kuingia sekondari kwa wakazi wa mkoa wa Kagera kwa kile serikali ilichokiita eti ni sera ya kuleta usawa kielimu Tanzania nzima.Kwa mfano wakati huo mkazi wa Kagera alipaswa kuwa na alama za ufaulu 90,mkazi wa eneo jingine aliweza kuchaguliwa kujiunga na sekondari kwa alama 40.Hii ni kinyume cha haki za binadamu(right to education).Evidence zipo naomba ndugu zangu tupeleke kesi hii ICC ili tutendewe haki.
Half caste,you have touched a raw nerve,kweli kuna mlolongo wa matukio ambayo sisi wahaya yalitudhoofisha sana kielimu.Ngoja niongezee mi pweint:
1.Mhadhama Cardinal Rugambwa (RIP): Katik late 60's alihamishiwa Dares salaam katika mazingira ya utata.Through his immense influence ndo miradi mingi ya elimu Bukoba ilikuwa inatakata (kumbuka Rugambwa sec ilikuwa iendelezwe hadi university level),leo ndo tunahangaika na mradi wa tawi la SAUT pale Itahwa na Jokuco nshambya (almost 40 years later).Remember Ihungo shule ya kanisa ya miaka hiyo? Rutabo? Rubya?
2. Vyama vya ushirika: Unakumbuka BCU (for that matter na victoria federation ya mwanza na kncu ya moshi).BCU ilikuwa inasomesha watoto wa wakulima bure all over the world.Wahaya kibao degree zao (akiwemo mzee George Kahama) walizipata kwa sponsorship ya coop union.Kiko wapi baada ya vyama hivi kuvunjwa miaka ya sabini (tena kwa makusudi).
......nitaendelea,ngoja nile kwanza matoke (binamu ensholo) yanapoa....
 
Mambo ya namna hii yanahitaji utulivu kidogo katika kuyajadili na katika kukurupuka kuna vitu unaweza ukajikuta umepoteza,sasa katika hili naomba nieleweke binafsi naamini kilicholetwa kuwa na ukweli japo katika nini kifanyike ni muda sasa serikali ya JMT ikaomba msamaha kwa watanzania wakazi wa mkoa wa Kagera na hata kwingine ambako kumekuwa na michezo michafu ya hivi ili kuweka umoja na amani inayosemwa kweli mioyoni mwa watanzania na si hii ya leo ya kurazimishana ili tu baadae watu hawa wasije kudai kuwekwa bayana wao ni watu wa nchi gani hapa ulimwenguni

Mbali ya hili kuna jingine linalosemwa kwamba ilipitishwa kwamba kamwe makabila makubwa na wahaya wakiwemo hayatakuja kuonja ikulu,sasa tunajiuliza kwani makabila haya yako nchi gani ama watu hawa walifanya nini mpaka wakapata laana hii ya kutokuwa marais katika nchi yao,nchi ya babu zao?

Ili la kuongeza maksi si la kuhoji kwani hata leo tunaona kwa mfano katika kutengeneza ulinganifu wa wanafunzi shuleni jinsi wanaume tunavyoumizwa kwa kubakizwa eti kisa mie nalingana na msichana katika maksi za la7,4m 4,4m 6 kuingia chuo n.k...huu ni uonevu mkubwa sana ila inashangaza na viongozi wanaamua kufumba macho huku wakijua kabisa wanaume tunaumizwa,hatuwezi kuwa na harari inayotokana na haramu,njia hii ni haramu na kamwe kitakachozaliwa hakitakuja kuitwa harari na ipo siku shutuma hizi zitawaka moto zaidi ya ule wa tanuru

Kwahiyo natoa wito kama kuna data hebu tupeni tuzisome ili tuweke rekodi vizuri na serikali itoe tamko la sivyo wananchi hawa na makabila haya ya kitanzania ipo siku yatadai uhuru na naamini hapatatosha

Poleni ndugu zetu na wahanga wote wa mbinu hizi za kibaguzi na kikaburu kwa watanzania wasio huru ndani ya nchi yao iliyo huru tokea 1961

Rweye.
 
It was a good move kama walifanya hivyo. Wahaya wasomi bado ni wengi ukilinganisha na makabila mengine. Bravo serikali ya CCM.
 
Baada ya uhuru tumeshuhudia mtaala wa elimu ukipandisha alama za ufaulu kuingia sekondari kwa wakazi wa mkoa wa Kagera kwa kile serikali ilichokiita eti ni sera ya kuleta usawa kielimu Tanzania nzima.Kwa mfano wakati huo mkazi wa Kagera alipaswa kuwa na alama za ufaulu 90,mkazi wa eneo jingine aliweza kuchaguliwa kujiunga na sekondari kwa alama 40.Hii ni kinyume cha haki za binadamu(right to education).Evidence zipo naomba ndugu zangu tupeleke kesi hii ICC ili tutendewe haki.
Kumbe ndo maana wataalamu wamepungua!!!!!, kweli Wahaya tungeachwa katika speed yetu ile ile, Tanzania ingekuwa kisima cha Maendeleo kwa nyanja zote.
 
Mimi sio mhaya, lakini nilifanyia mtihani Kagera. Rafiki yangu ni mhaya, lakini alifanyia mtihani Mara. Sasa hii ni move ya Wahaya/wana Kagera AU ni move ya wahanga wote waliofanyia paper wakiwa Kagera?
 
Naona uanze kuwatetea dada zako wanao dhalilishwa kule Temeke Sokota, Buguruni na Tandale (bwengas) halafu ndo ufunge safari ya ICC! Wahaya bana kwa kupenda sifa!, hapa anataka kuonyesha kuwa wao wana akili zaidi!!

akili wanazo,unabisha?
Subiri nifike nyumbani nikuoneshe jinsi walivyo na akili sana..
 
Kumbe ndo maana wataalamu wamepungua!!!!!, kweli Wahaya tungeachwa katika speed yetu ile ile, Tanzania ingekuwa kisima cha Maendeleo kwa nyanja zote.

Wachaga they are smart,baada yakuona hakieleweki wakaamua kukusanya nguvu zaowenyewe wasomeshe watoto wao,wahaya tukabweteka.
Leo nendamachame,uru,marangu,kibosho narombo uone quality ya praimari na sekondari za vijiji na kata,you will be amazed.Matokeo yake sisi wahaya tunabwabwaja eti wachaga wamejaa treasury,TRA na kwingine,kaone CV zao ni high quality na wanastahili nafasi zao.wahaya amkeni tujenge uhayani.Majuzi tu sekondari ya Kadea kanyigo ilikuwa hoi,wana kanyigo waishio dar walipoamua kushikamana na kufufua look at the number of div1 walizopata vijana mwaka jana,very impressive!
 
Nakubaliana na wewe mkuu!
 
Unajua nini mkuu, ndugu zetu hawa waliamua kubadilisha majina yao ya asili na kutumia majina ya kizungu ili waweze kuchaguliwa,

1.mfano JOHN NDIBALEMA,alipaswa kubadili jina na kujiitabulisha kama JOHN PROTASE,HAMIS KAGASHEKI,aliweza kutumia HAMIS MOHAMED.ili afiche ubini aweze kwenda secondary

2.Wengine waliweza kuhama Mkoa na kuingia Mikoa mingine ili waweze kuchaguliwa.

Ni sawa walitumia mbinu hizo eventuary baada ya kuchoshwa na ubaguzi wa kijinga, hila mkuu baadhi ya majina uliyo quote siyakusadikika yana wenyewe, kwa mfano jina la Barozi "Khamisi Kagasheki", sikumbuki kumsikia kabadilisha jina lake tangu anasoma shule ya msingi, O-level, A-level, Vyuo vikuu - amewahi kuishi Merikani na Ulaya. Hakuwahi kujulikana kwa jina lingine zaidi ya Hamisi Kagasheki, juzi juzi tu ndio ndiyo nilisikia watu wanamuita jina lake la kitoto "Kasibante".
 
Half caste,you have touched a raw nerve,kweli kuna mlolongo wa matukio ambayo sisi wahaya yalitudhoofisha sana kielimu.Ngoja niongezee mi pweint:
1.Mhadhama Cardinal Rugambwa (RIP): Katik late 60's alihamishiwa Dares salaam katika mazingira ya utata.Through his immense influence ndo miradi mingi ya elimu Bukoba ilikuwa inatakata (kumbuka Rugambwa sec ilikuwa iendelezwe hadi university level),leo ndo tunahangaika na mradi wa tawi la SAUT pale Itahwa na Jokuco nshambya (almost 40 years later).Remember Ihungo shule ya kanisa ya miaka hiyo? Rutabo? Rubya?
2. Vyama vya ushirika: Unakumbuka BCU (for that matter na victoria federation ya mwanza na kncu ya moshi).BCU ilikuwa inasomesha watoto wa wakulima bure all over the world.Wahaya kibao degree zao (akiwemo mzee George Kahama) walizipata kwa sponsorship ya coop union.Kiko wapi baada ya vyama hivi kuvunjwa miaka ya sabini (tena kwa makusudi).
......nitaendelea,ngoja nile kwanza matoke (binamu ensholo) yanapoa....
Mkuu Bishanga kuhamishwa kwa Rugambwa hakuwezi kuwa sababu ya kulaumu utawala wa Nyerere. Hayo ni mambo ya Kanisa Katoliki. Rugambwa alipandishwa madaraka ikabidi ahamie ktk Jimbo Kuu ambalo lilikua ni Dsm. Kukwama kwa miradi aliyoanzisha akiwa Bkb aulizwe Askofu aliyechukua nafasi ya Rugambwa. Kuhusu Vyama vya Ushirika nakubaliana na wewe kwa asilimia mia!
 
Mkuu wataalamu wengi wa Kihaya walimalizwa na Ukimwi.
Si kihivyo; kwani wahaya wote wameisha????, we sema tu tulikandamizwa na tunaendelea kukandamizwa bila kujitambua: just imagine; mtu anayemaliza kidato cha 4 Kagera mwenye Div.4 akija Dar akarudia paper anatisha si mchezo; wapo wengi wamehitu Engineering na Sheria na wanafanya vizuri ktk soko la ajira.
 
Mkuu Bishanga kuhamishwa kwa Rugambwa hakuwezi kuwa sababu ya kulaumu utawala wa Nyerere. Hayo ni mambo ya Kanisa Katoliki. Rugambwa alipandishwa madaraka ikabidi ahamie ktk Jimbo Kuu ambalo lilikua ni Dsm. Kukwama kwa miradi aliyoanzisha akiwa Bkb aulizwe Askofu aliyechukua nafasi ya Rugambwa. Kuhusu Vyama vya Ushirika nakubaliana na wewe kwa asilimia mia!
mwaka 1974 kwa nini Askofu Nkaranga ali resign voluntarily?
 
Back
Top Bottom