Wahafidhina wa CHADEMA na CCM wahaha kuwakwamisha Rais Samia na Mbowe

Wanajikwamisha wenyewe na washakwama....hakuna tena Ccm wala chadema....Act chama kinaongozwa na kajamaa kanafiki sana.
 
Inadaiwa kuna kundi la Wahafidhina kutoka Chadema na CCM ambao wamedhamiria kukwamisha Maridhiano ya mh Rais Samia na Mwenyekiti wa Chadema mh Mbowe

Kundi hilo la Wahafidhina wamo Mawaziri, Wabunge, Wajumbe wa kamati kuu za Chadema na CCM nk

Source: Gazeti la Raia Mwema
Chadema ni chama cha demokrasia kinaruhusu mawazo mbadala kupanua wigo wa uhuru wa maoni kusukuma gurudumu la maendeleo.
Kwa habari ya ccm sijui wao wakoje kwa wenye mawazo tofauti.
Kimsingi maridhiano ndio mlango uliofungua siasa za kukamiaana na kuwaweka huru wafungwa wa kisiasa waliobambikwa kesi na kufungwa gerezabi kwa husuda.
Tunataka siasa za kitaarabu zenye kuheshimu utu na maoni huru katika tofauti za watu.
Kigezo hiki ndicho kilichosukuma maendeleo kwa nchi zilizoendelea na kuweka misingi ya maendeleo endelevu.
 
Wakijaribu wakashindwa mwisho wa siku na wao wataona ili wafanikiwe kumkwamisha Rais na Mbowe nao watafanya maridhiano🙏😅
 
Inadaiwa kuna kundi la Wahafidhina kutoka Chadema na CCM ambao wamedhamiria kukwamisha Maridhiano ya mh Rais Samia na Mwenyekiti wa Chadema mh Mbowe

Kundi hilo la Wahafidhina wamo Mawaziri, Wabunge, Wajumbe wa kamati kuu za Chadema na CCM nk

Chanzo: Gazeti la Raia Mwema
Mkuu johnthebaptist hii makala ni ya kiwango cha chini sana kuwekwa na wewe. Hivi kweli inaingia akilini mwako kuwa Waziri anayeteuliwa na Samia mwenyewe ahusike kukwamisha maridhiano? Kwanza anakuwa na nia gani? Pili atafanya consipiracy hiyo na nani?
 
Labda kama Siasa za CCM umezisahau bwashee!

Hao Wajumbe wa Chadema wanaburuzwa tu CCM ndio kuna dhamira mbalimbali!
 
Inadaiwa kuna kundi la Wahafidhina kutoka Chadema na CCM ambao wamedhamiria kukwamisha Maridhiano ya mh Rais Samia na Mwenyekiti wa Chadema mh Mbowe

Kundi hilo la Wahafidhina wamo Mawaziri, Wabunge, Wajumbe wa kamati kuu za Chadema na CCM nk

Chanzo: Gazeti la Raia Mwema
Wahafidhina wa CCM, huwezi kuwakosa, Masatu Wasira, na Mzee Pinda na johnthebaptist

Sent from my Infinix X658E using JamiiForums mobile app
 
Hivi unajua CDM wameingizwa mkenge ?
Kama kuingizwa mkenge ni kuruhusu uhuru wa maoni na mikutano ya kisiasa na pia kuwaachia huru wafungwa wa kisiasa, napendekeza waingizwe mkenge zaidi. Mwisho wa siku tunachokitaka ni uhuru na furaha ya moyo. Mtoa wa mada umesukumwa na chuki zako dhidi ya maridhiano yanayoendelea, hilo halina shaka kabisa. Zama hizo zimepita.
 
Inadaiwa kuna kundi la Wahafidhina kutoka Chadema na CCM ambao wamedhamiria kukwamisha Maridhiano ya mh Rais Samia na Mwenyekiti wa Chadema mh Mbowe

Kundi hilo la Wahafidhina wamo Mawaziri, Wabunge, Wajumbe wa kamati kuu za Chadema na CCM nk

Chanzo: Gazeti la Raia Mwema
Kama wakikwamisha wakwamishe tu maana hata hayo maridhiano hayana tija kwa nchi sababu shida za wananchi ziko pale pale. Bidhaa mbalimbali bado ziko juu mfano maharage 1Kg Kenya bei ni Tshs 2800 wakati Tanzania 1 Kg ni 4500 lakini sasa hivi Wakenya wapo barabarani wakidai bei ishuke wakati Watz akiwepo huyo Mbowe anasifu na kuabudu bethidei ya miaka 2 ya Rais wake madarakani ili tu aendelee kunenepesha tumbo lake na familia yake kwa kutumia kivuli cha maridhiano ya kisiasa. Kalambishwa asali hapo white house kawa mpole kama mtu aliyekalia sindano.

Ukifuatilia kwa makini sasa hivi utagundua kuwa CHADEMA haina ajenda zozote zenye manufaa kwa wananchi kama ilivyokuwa enzi za Dr. Slaa. Ni bla bla nyingi zinazohusu mambo binafsi na kuelezea wananchi ubaya wa serikali iliyopita badala ya ''ku-address'' mambo yanayoathiri jamii kwa sasa hasa wa kipato cha chini na kipi kifanyike kupunguza makali ya ugumu wa maisha. Namshauri Mbowe aache kujinufaisha kwa kutumia mgongo wa maridhiano.
 
Kama kuingizwa mkenge ni kuruhusu uhuru wa maoni na mikutano ya kisiasa na pia kuwaachia huru wafungwa wa kisiasa, napendekeza waingizwe mkenge zaidi. Mwisho wa siku tunachokitaka ni uhuru na furaha ya moyo. Mtoa wa mada umesukumwa na chuki zako dhidi ya maridhiano yanayoendelea, hilo halina shaka kabisa. Zama hizo zimepita.
Wewe utakua ulikua fisadi ndio maana ulijiona huna uhuru sisi wengine tumekua huru siku zote kwako wewe mbowe lema na genge lake ndio wamekuletea uhuru?
 
Back
Top Bottom