political monger senior
JF-Expert Member
- Nov 26, 2020
- 1,801
- 5,788
KUWA UPINZANI TANZANIA NI KUJIPA MAUMIVU TU.
Kwa muda sasa nimekuwa nikifuatilia jinsi Viongozi wa Upinzani Tanzania wanavyowatumia vibaya wanachama wao. Nimekuwa nikiangalia namna ambavyo baadhi ya Wanachama waliovipigania Vyama hivyo kwa machozi na Damu wanavyonekana hawana thamani yoyote.
Hivi Jiulize kwa Chama kama CHADEMA ambacho kwa zaidi ya Miaka 20 kimekuwa kikiongozwa kama kikundi cha familia fulani huku kuna baadhi ya wanachama ambao wamejitoa kwa machozi na damu kujenga vyama hivyo, Unahisi watu hawa wanajisikiaje?
Hivi jiulize ni maumivu kiasi gani unayojibebea kwa kuwa Shabiki wa Chama ambacho hakina uwezo wa Kuleta hoja zinazokugusa wewe kama mwananchi wa Kawaida zaid ya kukushawishi kutumika kuandamana na kuingia kwenye Mgogoro na Vyombo vya Ulinzi na Usalama?
Matamanio ya Vijana wengi katika Siasa za Upinzani Tanzania ilikuwa kupata Vyama vitakavyokuwa mstari wa Mbele kutetea maslahi yao na sio Vyama vya kuwatumia Kuandamana na Kutetea Agenda za Ushoga kwa misingi ya Kupata misaada na Fedha kutoka kwa wafadhili toka mataifa ya Kigeni.
Leo hii Vyama vya Upinzani Nchini Tanzania vimekuwa mstari wa mbele kujaribu kuwajaza jazba Vijana wa Tanzania ili waweze kutumika kama Ngao yao ya kutekeleza Vitendo vyao vya Uovu.
Mpaka sasa vijana wote makini wamewashtukia wahuni wa Vyama Vya upinzani na wameamua kutotumiwa kutafutia Misaada na ruzuku toka kwa mabeberu.
Vijana makini wameamua Kukataa Ushoga na Kuunga Mkono Maendeleo. Vijana makini wanaona umuhimu wa Kumuunga Mkono mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan.
Kuna wafanyabiashara apa Tanzania wametenga mabilioni ya fedha ili kuakikisha Bandari inakosa mwekezaji wa Uhakika ili waendelee kutajirika kutokana na mifumo yetu mibovu iliyojaa Rushwa na ufisadi wa kutosha.
NASIMAMA NA PRESIDENT SAMIA KWENYE ILI LA BANDARI WEWE JE?