Kaka Mkubwa
Senior Member
- Oct 10, 2008
- 154
- 10
Unaweza kukopi na kupaste hapa?
SAKATA la ununuzi wa viungo vya ulemavu wa gozi 'albino' jijini limechukua sura mpya baada ya wafanyabiashara maarufu jijini kunaswa na Polisi kwa tuhuma za kujihusisha na biashara hiyo akiwemo mganga wa kienyeji na kufanya idadi ya waliokamatwa kuwa watano.
Sakata hilo la kunusurika kutekwa watoto wawili wa familia moja Irine Stanclaus (10) na Gerald Stanclaus (4) wakazi wa Kipawa, jijini ambapo walinusurikwa kupelekwa kusikojulikana na watu wawili waliokamatwa ambao ni Juma Anthony Ndaigwa (26), mkazi wa Magomeni Makuti na Juma Mgai (21) 'Juma Chibuku', mkazi wa Msasani Macho.
Watuhumiwa hao walikiri kushiriki kwenye matukio mbalimbali ya mauaji yaliyotokea ufukweni mwa habari ya Hindi, Morogoro, Kigamboni na Tandale.
Watuhumiwa wengine wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi ni mganga wa kienyeji, Kulwa Herman mkazi wa Mbezi Matangini, Dar es Salaam, wafanyabiashara maarufu wanaofahamika kwa majina Ndama Mtoto wa ng'ombe na Juma Ally 'Kizaizai'.
Kukamatwa kwa watuhumiwa hao ni kutokana na juhudi za polisi kufanya msako mkali kutokana na watuhumiwa kuwataja wanaoshirikiana nao kwenye suala la biashara ya viungo vya albino.
Habari kutoka vyanzo vyetu zinaeleza kuwa, hadi sasa idadi ya waliokamatwa kuhusiana na tuhuma za kushiriki kwenye biashara hiyo ni watano.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile alisema juzi kuwa, jeshi lake linaendelea na juhudi za kuhakikisha kuwa wale wote wanaojihusisha na biashara hiyo wanakamatwa.
Alisema kazi ya kuwakamata watuhumiwa imekuwa ngumu kutokana na watuhumiwa kukimbia nyumba zao hata hivyo juhudi zinafanywa kwa kushirikiana na wasamaria wema ili kuweza kupata taarifa walipokimbilia.
"Biashara hiyo imeingia Dar es Salaam hivyo tutashirikiana kuhakikisha wale wote wanaojihusisha na biashara hiyo wanakamatwa, " alisema Shilogile.
Mama wa watoto hao Evodia Stanclaus alisema alipata taarifa za watoto wake kuwindwa na watu wawili waliokuwa wakirandaranda katika maeneo ya nyumbani kwake wakijifanya kutafuta simu ya mkononi yenye kamera.
Hata hivyo kwa ushirikiano na wananchi waliweza kuwakamata watuhumiwa hao baada ya jirani yake kusikia njama hizo zikipangwa kwenye simu ya mkononi na vijana hao kupitia dirishani na kutoa taarifa za siri kwa majirani wenzake.
Baada ya kuwekwa chini ya ulinzi na kupata kipigo kikali vijana hao waliweza kuokolewa na polisi waliofika eneo la tukio.
Katika operesheni hiyo tayari mfanyabiashara anayesadikiwa kuwa ni raia wa Burundi mwenye asili ya Kiarabu anashikiliwa na polisi wakiwemo watu wengine watatu kutoka maeneo ya Kimara, Ubungo na Magomeni jijini.