Singida: 6 Wakamatwa kwa tuhuma za Mauaji na Kufukua Makaburi

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,379
8,123
WATU sita wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Singida wakihusishwa na mauaji ya watu, ufukuaji wa makaburi na kuchukua viungo, baadhi ya vitu vya maiti katika maeneo tofauti wilayani Manyoni.

Imeelezwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Stella Mutabihirwa, leo Machi 28, 2023 kuwa hatua hiyo imefuatia msako uliofanywa na Jeshi hilo, kati ya Machi 16 na 24 Mwaka huu.

“Msako ulifanyika kwenye maeneo tofauti ya Wilaya ya Manyoni na vijiji vya jirani vilivyopo Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora,” amesema Kamanda Mutabihirwa.

HABARI LEO
 
Sasa wakipelekwa rumande wakaingizwa gerezani hatasababisha taharuki ndani ya selo kama watajitambulisha kwa makosa waliyopekwa nayo huko? Maana manyampara yana utaratibu wa kutambulisha wageni huku wageni wakitaja makosa yao ndani ya selo wakisikilizwa na wa wafungwa na mahabusu. Nani atakubali kulala jirani na washirikina, je wakifanya ushirikina wa kutishia askari na wafungwa huko gerezani si waleta taharuki?
 
Back
Top Bottom