Diwani Viti Maalumu Moshi matatani, ni kwa tuhuma za kumtumikisha mwanafunzi Baa

Jul 30, 2018
13
12
DIWANI wa Viti maalumu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Manispaa ya Moshi anatajwa kuingia matatani baada ya kudaiwa kumtumikisha kama mhudumu wa baa mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya Sekondari Longido, iliyopo mkoani Arusha.

Mwanafunzi huyo anatajwa kutoweka kwa zaidi ya siku 30 alikutwa akitumikishwa kama mhudumu wa baa kwenye moja ya baa maarufu iliyopo eneo la Soweto mjini Moshi ,baa inayotajwa kumilikiwa na Diwani huyo.

Mwanafunzi wa jinsia ya kiume anatajwa kutoweka nyumbani kwao Kwa Moromboo, jijini Arusha Septemba 19, mwaka huu na hakuonekana shuleni alipotakiwa kuripoti hata hivyo badae wazazi wa kijana huyo walipata taarifa kwamba mwanafunzi huyo hakuripoti shuleni hapo.

Taarifa zinaeleza kuwa awali Wazazi baada ya kubaini kuwa mwanafunzi huyo hajulikani alipo na hakuripoti shuleni ,walifanya uamuzi wa kutoa taarifa kituo cha polisi cha Murieti kilichopo wilaya ya Arusha na kufungua jalada lililopewa namba, MRT/RB/4900/2023 na kuanza kumfuatilia mwanafunzi huyo alipo.

Baba mkubwa wa mwanafunzi huyo aliyejitamburisha kwa jina la Philibert Mshanga amesema baada ya mwanafunzi huyo baada ya kuaga nyumbani kwao kwamba anenda shuleni hakuonekana kwa zaidi ya mwenzi mmoja hadi alipokutwa Oktoba 19 akifanya kazi kwenye baa inayoaminika kuwa ya diwani .

"Novemba 18 mwaka huu ambapo ndio siku shule zilifunguliwa mtoto aliondoka nyumbani muda wa saa nne asubuhi kwenda shuleni Longido na ana desturi akifika shuleni anatoa taarifa kwa wazazi kwamba amefika, sasa zikawa zimepita siku kadhaa hajatoa taarifa,"

"Wazazi wakajiuliza mbona hajatoa taarifa ya kufika shuleni? wazazi wakapiga simu shuleni, wakaelezwa ana vipindi vitatu hajaonekana darasani, ikabidi wazazi wafike pale shuleni kupata taarifa zaidi, walipofika ni kweli hakuonekana ikabidi waende kituo cha polisi kwenda kutoa taarifa,"

Mshanga anasema baada ya kupewa namba ya jalada (RB ) waliendelea kumtafuta mwanafunzi huyo pamoja na kutuma taarifa za kumtafuta mtoto huyo kwenye makundi mablimbali ya mtandao wa Whats App ambapo siku chache baadaye ilitumwa meseji kwenye simu ya mama yake ikieleza kwamba"njoo nichukue nateseka"

"Baada ya mama yake kupata ujumbe huo, alipiga simu ambayo ilituma ule ujumbe na ikapokelewa na mwanamke mmoja, akamuuliza wewe ni nani akamwambia kuna ujumbe umetuma kwenye simu yangu…ikieleza njoo nichukue nateseka,"

Alisema baadaye polisi walifuatilia mawasiliano ya namba iliyotuma ujumbe kwenye simu ya mama wa mwanafunzi huyo ambayo ilifanikisha kumpata mwanafunzi huyo akiwa kwenye baa hiyo eneo la Soweto Manispaa ya Moshi.

Taarifa zinaeleza kuwa Maofisa wa Polisi wanaotajwa kutoka kituo kikuu cha Polisi jijini Arusha walifika Moshi na kumshikilia Diwani huyo katika kituo cha polisi cha kati mjini Moshi ambapo baadae inadaiwa alipewa dhamana kwa msaada wa Diwani mwenzake kwa sharti la kuripoti kituoni hapo.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo alipotafutwa kuzungumzia juu ya tukio hilo alisema apewe muda anafuatilia tukio hilo na kwamba atalitolea taarifa baadaye huku kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Simon Maigwa akiomba muda zaidi ili aweze kufuatilia undani wa tukio hilo.

Tumemtafuta Diwani huyo na kufanikiwa kuonana nae akiwa kituo cha Polisi cha kati mjini Moshi na kumuuliza utayari wake wa kuzungumzia tuhuma hizo hata hivyo alijibu kwa kifupi kwamba kwa sasa hawezi kuzungumzia suala hilo .
 
Back
Top Bottom