Wadau: Uwekezaji Bandari ya Dar es Salaam hauepukiki, nchi itanufaika

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,128
49,850
Baadhi ya maoni ya wadau mbalimbali wa masuala ya kiuchumi yameeleza kuwa nchi inapota kukua zaidi kiuchumi basi uwekezaji katika bandari ni muhimu zaidi katika manufaa hayo.

Wakati haijulikani nini kinahitajika kufanyika hadi sasa tangu kuibuka kwa suala la uwekezaji katika Bandari ya Dar es Salaam kupitia mwekezaji kutoka Falme za Kiarabu (UAE), uchumi wa nchi bado unahitaji kukua.

Kwa nyakati tofauti takwimu zimeonyesha namba zisizoridhisha kiutendaji katika bandari nchini ukilinganishwa na uhalisia wa eneo la Tanzania linavyoweza kunufaika kupitia sekta ya bandari baharini na ziwani.

Hata hivyo, bado baadhi ya watu wanaamini kila uwekezaji ni wizi kwa mali ya umma. Bila kuangalia hali halisi kwa nchi zinazoendelea ikiwemo Marekani na Uchina zinavyoruhusu kwa kasi ya ajabu uwekezaji kutoka nje.

Mwaka 1961 baada ya Uhuru wa Tanganyika, bandari zote nchini zilikuwa chini ya wazalendo wakati huo Serikali ikiongozwa na Rais Julius Kambarage Nyerere. Wakati huo ushindani ulikuwa mkubwa na mataifa jirani yenye bandari ikiwemo Kenya na Msumbiji.

Lakini kijiografia Bandari ya Dar es Salaam imekaa sehemu nzuri kupokea na kupeleka mizigo katika nchi kama Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia, Zimbabwe, Malawi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na hata baadhi ya maeneo ya Kenya kutokana na ukaribu wake.

Mbali ya kuwepo fursa hiyo na ukubwa wa eneo lililopo kwa Bandari ya Dar es Salaam, bado haifui dafu kwa bandari za Afrika.

Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Mrisho Mrisho alipata kueleza kuhusu ongezeko la watumiaji wa bandari hiyo kwa kila mwaka ikiwemo Nchi jirani na za maziwa makuu ambazo hupitisha magari kwa asilimia 60.

Takwimu kama hizo zinaonyesha kuwa nu ni muda muafaka kwa Serikali kuingia ubia na Mwekezaji ili kuongeza tija na ufanisi wa kiutendaji katika Bandari hiyo ili kuongeza pato la Taifa.

Unapozungumzia ufanisi wa bandari katika viwango vya kimataifa ni pamoja na kupunguza muda wa meli kusubiri nje ya bandari, kupunguza muda wa malori unaotumiwa ndani ya bandari, kuongeza idadi ya mizunguko ya mashine ya kupakua na kupakia makasha.

My Take
Chadomo na Mwambukusi tafuteni kazi ya kufanya, uzushi wa Bandari imeshawakata.

View: https://twitter.com/RashdaZunde/status/1715372180169433248?t=7pqswVonU9ECpnb4bgDN6A&s=19
 
Mmeona tu bandarini ndo wanatafuna umeona zile daraja za m200+ na la B17 huko hawatafuni Hela ee
 
Tatizo letu tunapoiongelea bandari vichwani tunakuwa na akili zile zile za kijamaa na hata lile wazo kwamba Bandari iingizwe kwenye sheria ya utunzaji wa rasilimali za nchi msingi wake ni ujamaa huo huo. Kwamba tunalinda rasilimali za nchi.

Hatujiulizi mabadiliko ya uendeshaji wa dunia wa sekta ya bandari kulinganisha na namna tunavyoiendesha bandari yetu kama tunaenda nayo sambamba au tumeshachelewa.

Ujamaa una kawaida ya kudanganya watu ili wabakie katika ile ile comfort zone ya miaka yote bila kuangalia uhalisia wa dunia upo vipi.

Ujamaa unapofusha macho yenye kutakiwa kuona mbele pamekaa vipi kiuchumi. Sio kwamba anakuja DP World peke yake kuna waendeshaji wengine wanakwenda kupewa bandari za Bagamoyo na ile ya Tanga.

Pale TPA kutakuwa na waendeshaji watatu mahiri, DP World na mwingine pamoja na TPA mwenyeji, lengo hapo ni kukuza tija na kuhakikisha mchango wa bandari kiuchumi unapatikana wote ikiwezekana.
 
Chawa Aliyeshiba Damu Kwenye Viwango Vyake

Unaambiwa Kila Siku Hakuna Mtu Anayekataa Uwekezaji

Namna Dubai Port World Ilivyoletwa Na Ule Umilele Ndiyo Watu Hawakubali
 
Hebu muacheni Hangaya atulie jamani sakata la DP WORLD limepoa mnataka mama akose usingizi tena?
 
Wengi wetu hatuwezi kuona namna meli zinavyochelewa kushushwa kwamba ni utaratibu unaochelewesha sana uchumi wa nchi kukua kwa haraka.

Wengi wetu hatuwezi kuongea kwa niaba ya wafanyabiashara wanaoagiza vitu na kupeleka nje tunaongea tukiongozwa na roho mbaya tu tukidhani kuwa baadhi yetu wanakwenda kupata riziki nono hivyo eti tuwazibie!.
Sina hakika kama kuna Mtanzania mwenye akili anaekataa Uwekezaji ktk bandari zetu. Shida ni aina ya mikataba ya kifisadi kama ule wa Waarabu wa Dubai. Ndiyo kuna mapungufu makubwa ya uendeshaji wa bandari zetu, lakini hiyo hisitufanye tukubaliane na ulaghai wa hao wawekezaji kwa kushirikiana na wenye mamlaka nchini kuhujumu na kujineemesha kupitia bandari zetu.
 
Huo mkataba unaosema ni mbovu baada ya kuaminishwa unaweza kutaja kifungu kipi ni kibaya kwetu sisi na kwa sababu zipi haswa?

Tunaweza kuaminishwa na waraka wa maaskofu kwamba mkataba ni mbaya na unatufunga kiasi cha kushindwa kuendeleza bandari lakini TPA wanaendelea kutangaza zabuni za uendeshaji wa bandari zetu, hapo ndio pa kujiuliza. Kama mkataba ni mbaya na wa kifisadi hizi barua za kualika waendeshaji wengine zinaweza vipi kuendelea kuwekwa mitandaoni?

Maarifa ni tatizo la nchi yetu.
 
Chawa Aliyeshiba Damu Kwenye Viwango Vyake

Unaambiwa Kila Siku Hakuna Mtu Anayekataa Uwekezaji
Namna Dubai Port World Ilivyoletwa Na Ule Umilele Ndiyo Watu Hawakubali
DP World alipewa tender moja kwa moja kutokana na uwezo wa kampuni yake kikazi na kutakana na ukweli kwamba ni mmiliki wa biashara nyingi za kule Rwanda na DRC.

Hawa wazabuni wengine wa magati namba nane mpaka kumi na moja imebidi watangazwe kwa mfumo ule ule wa zamani kwa sababu hawana sifa kama zile za DPW.
 
Huo mkataba unaosema ni mbovu baada ya kuaminishwa unaweza kutaja kifungu kipi ni kibaya kwetu sisi na kwa sababu zipi haswa?.

Tunaweza kuaminishwa na waraka wa maaskofu kwamba mkataba ni mbaya na unatufunga kiasi cha kushindwa kuendeleza bandari lakini TPA wanaendelea kutangaza zabuni za uendeshaji wa bandari zetu, hapo ndio pa kujiuliza. Kama mkataba ni mbaya na wa kifisadi hizi barua za kualika waendeshaji wengine zinaweza vipi kuendelea kuwekwa mitandaoni?.

Maarifa ni tatizo la nchi yetu.
Steve, naona wewe ndiye uliyehamishwa vibaya. Achana na TEC, ww binafsi hukuuona mkataba na kuusoma? Mbona hiyo IGA ya DPW ilisambaa kila kona hasa mitandaoni?. Kama huna uwezo wa kusoma, kutafasili na kuelewa kilichoandikwa, iweje uilaumu TEC na wadau wengine waliojitokeza kupinga kwa hoja na kuelemisha wale wasiojua kutafasili hiyo IGA? Sakata zima hakuna hata siku moja serikali ilishaweza kujibu hoja zozote zinazolalamikiwa hisipokuwa imekuwa ikijikanyaga kanyaga kwa majibu ya jumlajumla ambayo hayamo kwenye mkataba wenyewe.

Kwa kifupi ule haukuwa mkataba wa uwekezaji hisipokuwa umilikishwaji wa bandari zetu kwa Waarabu.
 
Sawa, tunahitaji mwekezaji lakini mwenye manufaa. Katika maelezo yako sijaona wapi unasemea mapato tutakaopata baada ya kumpa huyo mwekezaji .
Pili, hausemi kwa sasa, tunapata kiasi gani kwa mwaka ili tulinganishe na mwekezaji huyo atakachotupa.

Kila Mtanzania , anahamu ya kuona tunapata zaidi kuliko tunachopata kwa sasa.

Pia, lazima mwekezaji, asipewe bandari milele. Lazima mkataba useme ni miaka mingapi na tukishindwana tunaachanaje, Hata akipewa kwa miaka 20 au 30 n.k haina neno.
Hayo yalishaelezwa sana ila wewe umechagua Utapeli wa kina Mwambukusi
 
Steve, naona wewe ndiye uliyehamishwa vibaya. Achana na TEC, ww binafsi hukuuona mkataba na kuusoma? Mbona hiyo IGA ya DPW ilisambaa kila kona hasa mitandaoni?. Kama huna uwezo wa kusoma, kutafasili na kuelewa kilichoandikwa, iweje uilaumu TEC na wadau wengine waliojitokeza kupinga kwa hoja na kuelemisha wale wasiojua kutafasili hiyo IGA? Sakata zima hakuna hata siku moja serikali ilishaweza kujibu hoja zozote zinazolalamikiwa hisipokuwa imekuwa ikijikanyaga kanyaga kwa majibu ya jumlajumla ambayo hayamo kwenye mkataba wenyewe.

Kwa kifupi ule haukuwa mkataba wa uwekezaji hisipokuwa umilikishwaji wa bandari zetu kwa Waarabu.
Kama ule ni umilikishwaji wa bandari yetu hao hao TPA wanapata wapi mamlaka ya kutangaza tender za uendeshaji wa magati namba 8 mpaka 11?. Wanapata wapi mamlaka ya kutangaza tender ya uendeshwaji wa bandari ya Mbegani Bagamoyo?.

TEC wanastahili lawama kwani wameingiza siasa kwenye suala la kiuchumi, wanadhani wanafanya uzalendo kumbe ndio wamewachanganya na kuwakwaza wasomi wanaosali makanisani ambao pia ni wataalam wa serikali.

TEC waliingia mkenge wa kufikiria kama wewe unavyofikiri kwamba mkataba unaiuza nchi, ungekuwa unaiuza nchi hizi tender za kutafuta waendeshaji zingeweza vipi kuwekwa kwenye magazeti na mitandaoni?.

Watu wangu wanateketea kwa ukosefu wa maarifa - Biblia.
 
Steve, inaelekea una mgogoro wa wivu na kiimani kwa TEC. Swala la IGA kati ya serikali na DPW halikupigiwa kelele na TEC pekee bali na wadau wengi waliousoma, kuuelewa na kuutafasili ule mkataba. Ni mkataba wa hovyo ambao ulilenga kugawa bandari bure kwa Waarabu. Sitaki niingie ndani kueleza uhovyo wa ule mkataba kwasababu unajulikana, hasiyeujua ni yule hasiyejua kusoma au aliyehamua kwasababu zake kujitoa ufahamu.. Mkataba uko wazi kwenye mitandao na mengi yamefafanuliwa na wanasheria.

Kukataliwa kwa mkataba wa DPW hakuzuhii kuendelea kutafuta wawekezaji wengine. Sasa unapouliza kwa nini TPA inatangaza tenda sikuelewi. Kwa mawazo yako unafikiri wawekezaji kwenye bandari ni hao Waarabu pekee?

Shida haikuwa Waarabu kuwekeza kwenye bandari zetu kilichogomba ni aina ya mkataba wenyewe.
 
Steve, inaelekea una mgogoro wa wivu na kiimani kwa TEC. Swala la IGA kati ya serikali na DPW halikupigiwa kelele na TEC pekee bali na wadau wengi waliousoma, kuuelewa na kuutafasili ule mkataba. Ni mkataba wa hovyo ambao ulilenga kugawa bandari bure kwa Waar00abu. Sitaki niingie ndani kueleza uhovyo wa ule mkataba kwasababu unajulikana, hasiyeujua ni yule hasiyejua kusoma au aliyehamua kwasababu zake kujitoa ufahamu.. Mkataba uko wazi kwenye mitandao na mengi yamefafanuliwa na wanasheria.

Kukataliwa kwa mkataba wa DPW hakuzuhii kuendelea kutafuta wawekezaji wengine. Sasa unapouliza kwa nini TPA inatangaza tenda sikuelewi. Kwa mawazo yako unafikiri wawekezaji kwenye bandari ni hao Waarabu pekee?

Shida haikuwa Waarabu kuwekeza kwenye bandari zetu kilichogomba ni aina ya mkataba wenyewe.
Novemba mwaka huu DP World anaanza kazi hapo bandarini kwa mkataba huo huo uliopigiwa kelele na watu wasio na uelewa wa mikataba ya sheria za kimataifa.

Kupigiwa kelele na watu wengi haina maana wote hao wapo sawa, wanaweza kuwa na tatizo la uelewa pia, wengine ni watu wanaotumiwa na mafisadi wanaofaidika na hiyo bandari kubakia kama ilivyo.

Huo mkataba unaosema ni mbovu umetolewa ufafanuzi kila mahali na hauna ubovu wowote. Ungekuwa ni mbovu kama tunavyodanganyana TPA wangepata vipi uwezo wa kutangaza tender za magati namba nane mpaka kumi na moja?, wangeweza vipi kutangaza tender ya Mbegani Bagamoyo?.

Pia bandari ya Tanga inakwenda kutangaziwa tender ya uendeshaji, nchi zetu za kiafrika zimejaa wapigaji wa kila aina, kuna watu wa hovyo sana na hao ndio wanaipotosha jamii kwamba mkataba ni mbovu na eti nchi itauzwa!, mbona wanatafutwa waendeshaji wengine wa TPA bila ya nchi kuuzwa?.

TICTS amekaa pale TPA kwa miaka 22 na nchi haijauzwa. Swissport ambaye zamani aliitwa DAHACO yupo pale airport tangu miaka ya 90 mwanzoni na nchi haijauzwa mpaka leo.
 
Back
Top Bottom