ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 44,321
- 51,061
Baadhi ya maoni ya wadau mbalimbali wa masuala ya kiuchumi yameeleza kuwa nchi inapota kukua zaidi kiuchumi basi uwekezaji katika bandari ni muhimu zaidi katika manufaa hayo.
Wakati haijulikani nini kinahitajika kufanyika hadi sasa tangu kuibuka kwa suala la uwekezaji katika Bandari ya Dar es Salaam kupitia mwekezaji kutoka Falme za Kiarabu (UAE), uchumi wa nchi bado unahitaji kukua.
Kwa nyakati tofauti takwimu zimeonyesha namba zisizoridhisha kiutendaji katika bandari nchini ukilinganishwa na uhalisia wa eneo la Tanzania linavyoweza kunufaika kupitia sekta ya bandari baharini na ziwani.
Hata hivyo, bado baadhi ya watu wanaamini kila uwekezaji ni wizi kwa mali ya umma. Bila kuangalia hali halisi kwa nchi zinazoendelea ikiwemo Marekani na Uchina zinavyoruhusu kwa kasi ya ajabu uwekezaji kutoka nje.
Mwaka 1961 baada ya Uhuru wa Tanganyika, bandari zote nchini zilikuwa chini ya wazalendo wakati huo Serikali ikiongozwa na Rais Julius Kambarage Nyerere. Wakati huo ushindani ulikuwa mkubwa na mataifa jirani yenye bandari ikiwemo Kenya na Msumbiji.
Lakini kijiografia Bandari ya Dar es Salaam imekaa sehemu nzuri kupokea na kupeleka mizigo katika nchi kama Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia, Zimbabwe, Malawi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na hata baadhi ya maeneo ya Kenya kutokana na ukaribu wake.
Mbali ya kuwepo fursa hiyo na ukubwa wa eneo lililopo kwa Bandari ya Dar es Salaam, bado haifui dafu kwa bandari za Afrika.
Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Mrisho Mrisho alipata kueleza kuhusu ongezeko la watumiaji wa bandari hiyo kwa kila mwaka ikiwemo Nchi jirani na za maziwa makuu ambazo hupitisha magari kwa asilimia 60.
Takwimu kama hizo zinaonyesha kuwa nu ni muda muafaka kwa Serikali kuingia ubia na Mwekezaji ili kuongeza tija na ufanisi wa kiutendaji katika Bandari hiyo ili kuongeza pato la Taifa.
Unapozungumzia ufanisi wa bandari katika viwango vya kimataifa ni pamoja na kupunguza muda wa meli kusubiri nje ya bandari, kupunguza muda wa malori unaotumiwa ndani ya bandari, kuongeza idadi ya mizunguko ya mashine ya kupakua na kupakia makasha.
My Take
Chadomo na Mwambukusi tafuteni kazi ya kufanya, uzushi wa Bandari imeshawakata.
View: https://twitter.com/RashdaZunde/status/1715372180169433248?t=7pqswVonU9ECpnb4bgDN6A&s=19