Wadau, hivi mwenendo wa soko la ajira la Tanzania mnauonaje?

Imruu

Member
Nov 4, 2023
12
15
Hebu nipeni mawazo yenu wakuu; hii trend ya upatikanaji wa ajira kwa upande wenu mnaionaje? Ukiangalia miaka kumi iliyopita, idadi ya fursa za ajira zilizokuwepo na idadi ya wataalamu huru waliokuwepo (wahitimu). Ukiangalia idadi ya fursa za ajira zilizokuwepo hivi sasa na idadi ya wataalamu huru waliokuwepo (wahitimu).

Kwa miaka 10 ijayo tunahisi hali ya upatikanaji wa ajira utakua vipi? Je, fursa zitakuwepo? Elimu yetu watanzania itakua na thamani tena au wasomi watakua wamejazana mitaani tu?

Hebu changia mawazo yako mkuu.
 
haya maisha majirani zetu wa Kenya walishayaanza muda sana, kwetu ndo tunayaanza baadae watu watazoea na kuamua kujiongeza na mengine kama wa nigeria tu,,,,,hii ni shida kwa nchi nyingi za kiafrika sababu walikua wanafata mfumo wa elimu na ajira wa kikoloni ,,,kuna kipindi lazima ubume hasa wasomi wakiwa wengi huku ajira zinazozalishwa ni chache,,,,,ajira zinaweza kubaki kwa wenye connection au iwe bahati tu kama kubet
 
Tunakoelekea ndo hatari, kwa elimu yetu hii mbovu zaidi ya 40% ya kozi zinazotolewa elimu ya juu zitakua hazina maana wala fursa.

Automation inakuja na mavitu kama Artificial intelligence, Industrial automation, Robotics, collaborative robots nk.

Miaka ya 2030 na kuendelea hali itakuwa mbaya sana mtaani kwa elimu hii na Kasi ya vijana kukimbilia masomo kukariri ngoni migration
 
Liko vizuri Sana na Nchi inafunguka,tafuta mtaji ,tafuta fursa maisha ni mapambano.

Msikiloze Gwaji Boy utaelewa kwamba tatizo sio Ajira ila tatizo ni kichwa chako
 
Hakuna ajira bongo,serikali iingie ubia TU na nchi zingine ulaya au uarabuni wakitaka wafanyakazi watangae kupitia wizara ya kazi hata za vibarua vya mda wakafanye nje wapate angalau mitaji
Shida ni kwamba mitaala yetu ya elimu haipo standard kuendana na soko la ajira la kimataifa, yani degree ya tanzania ni aghalabu sana ukaajiriwa nchi za wenzetu huko
 
haya maisha majirani zetu wa Kenya walishayaanza muda sana, kwetu ndo tunayaanza baadae watu watazoea na kuamua kujiongeza na mengine kama wa nigeria tu,,,,,hii ni shida kwa nchi nyingi za kiafrika sababu walikua wanafata mfumo wa elimu na ajira wa kikoloni ,,,kuna kipindi lazima ubume hasa wasomi wakiwa wengi huku ajira zinazozalishwa ni chache,,,,,ajira zinaweza kubaki kwa wenye connection au iwe bahati tu kama kubet
Nakuunga mkono mkuu🤝
 
Tunakoelekea ndo hatari, kwa elimu yetu hii mbovu zaidi ya 40% ya kozi zinazotolewa elimu ya juu zitakua hazina maana wala fursa.

Automation inakuja na mavitu kama Artificial intelligence, Industrial automation, Robotics, collaborative robots nk.

Miaka ya 2030 na kuendelea hali itakuwa mbaya sana mtaani kwa elimu hii na Kasi ya vijana kukimbilia masomo kukariri ngoni migration
😂😂 Ama kweli inabidi tujiongeze na tubadili mindset zetu sisi vijana kwanza then tushajihishe mabadiliko huko juu
 
Liko vizuri Sana na Nchi inafunguka,tafuta mtaji ,tafuta fursa maisha ni mapambano.

Msikiloze Gwaji Boy utaelewa kwamba tatizo sio Ajira ila tatizo ni kichwa chako
Umezungumzia swala la ubunifu na upambanaji wa mtu binafsi lakini topic inazungumzia soko la ajira ambalo liko governed na nchi na linategemea taaluma rasmi ambayo inasmamiwa na nchi vilevile, elewa topic kisha wasilisha maoni yako
 
Zama za kusubiria Nchi na kutegemea vyeti zimepita.
 
Soko la ajira lipi sasa? Uchumi ukivuruga soko la ajira usitegemee muujiza...maisha ni ya kubahatisha sana kwa vijana hasa wanaotoka shule.

Kada kama ualimu na afya wapo mtaani wana bet wakati hatukuzoea hali hiyo. Mahitaji ni makubwa ya hao watu hospitalini na shuleni ila hatuna pesa ya kuwalipa unapowaingiza kwenye payroll ya URT.
 
Aiseee ni shida kwelikweli! Hakuna uwiano mzuri kati ya wasomi na ajira zilizopo. Kuna baadhi ya kozi unakuta kwa kila wahitimu 1000 nafasi ya ajira ni moja.

Sekta ambayo naona inaweza kubeba watu wengi ni kilimo na mifugo iwapo changamoto mbalimbali zinazozikabi zitatatuliwa hususani masoko.

Kwa miaka kumi ijayo hali itakuwa mbaya sana aisee

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
Soko la ajira lipi sasa? Uchumi ukivuruga soko la ajira usitegemee muujiza...maisha ni ya kubahatisha sana kwa vijana hasa wanaotoka shule.

Kada kama ualimu na afya wapo mtaani wana bet wakati hatukuzoea hali hiyo. Mahitaji ni makubwa ya hao watu hospitalini na shuleni ila hatuna pesa ya kuwalipa unapowaingiza kwenye payroll ya URT.

walimu wapo mitaan shule hazina walimu.shule ina wanafunzi 600 na walimu wawili ref.itv habar jana. wanaomba waongezewe walimu
 
Back
Top Bottom