Je, Serikali ina mpango gani na ongezeko la ajira nchini Tanzania?

Utawala2025

JF-Expert Member
Oct 20, 2023
329
1,059
Habari.

Kwanza Tuanze kumshukuru mwenyezi Mungu kwa kuweza kutupa uhai tena hilo ni jambo Jena la kumahukuru Mungu.

Kwa upande wa mada iliyo mezani Serikali imejipanga vipi na ongezeko la ukosefu wa ajira nchini?

Nchi yeyote inachangia asilimia kadhaa ya kuzalisha ajira katika nchi yake na mara zote sio asilimia 100,
Kwa upande wa Tanzania uzalishaji wa ajira kwa upande wa umma umekuwa ukiongezeka na kubosreshwa kadri ya siku zinavyoenda.

Ongezeko pia la wahitimu wanaoingia katika utafutaji wa ajira katika soko nchini ni mkubwa pia.

Uzalishaji wa watalaamu hao umesababishwa na ongezeko la vyuo vikuu na vya kati nchini.
Mwamko wa wazazi katika kusomesha watoto tofauti na miaka ya zamani. Ongezeko la shule za sekondari ya awali na juu. Ongezeko pia la idadi ya watu.

Kama Wananchi Tunafurahi kuona ongezeko hili la watalaamu na wasomi katika nchi ya Tanzania na linaleta faida nyingi chants.

Swali langu Je serikali imejipangaje kwa ongezeko hili la ukosefu wa ajira nchini kwetu nikimaanisha.

(1) Je, Wameeandaa mtaala maalum ambao utaweza kuwasaidia wahitimu wakiingia mtaani waweze kujiajiri.

(2)Je, kuna mifumo mizuri imeundwa ambayo unaweza kupelekea vijana wakaweza kujiajiri kama kuwawezesha kupata mikopo ya riba nafuu,utoaji wa maeneo ambayo vijana wanaweza kufanya shughuli za kilimo.

(3) Je, Ajira za kutosha zimeendelea kuzalishwa ukiachana na siasa za makaratasi.

(4) Je, michakato ya ajira upande wa sekta binafsi na serikali ni ya wazi pasipo kuweka shaka lolote la watafuta ajira kuwa na wasiwasi wowote.

(5) Viongozi wa kiserikali kuanzia ngazj ya jua hadi chini wanejiandaa Kaunda Sera bora za Ajira nchini.

Namalizia.

Je, Serikali imejipangaje na ONGEZEKO LA AJIRA NCHINI?
 
Serikali haina mpango wowote na upungufu wa ajira sababu wao ndio waliotengeza hilo tatizo. Hadi yeboyebo unaagiza nje, migodi yote umeuza, yaani kila kitu umeuza, bandari etc.

Vyuo vipo kukusanya hela kupitia control namba,FUNGUKA!!
 
Serikali haina mpango wowote na upungufu wa ajira sababu wao ndio waliotengeza hilo tatizo. Hadi yeboyebo unaagiza nje, migodi yote umeuza, yaani kila kitu umeuza, bandari etc.

Vyuo vipo kukusanya hela kupitia control namba,FUNGUKA!!
Una uhakika?
 
Hizi ndizo ajira za uhakika
Bodaboda, mama ntilie, wapiga debe stendi, watembeza maji
 
Back
Top Bottom