BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,020
Date::1/15/2010Wachina sasa wahamia Msanga
Wafanyabiashara ya Magogo na Mbao wakitayarisha bidhaa zao katika kijiji cha Msanga wilayani Kisarawe, tayari kwa kuzisafirisha kwenda Dar es Salaam
Julieth Ngarabali,Kisarawe
WIMBI la uvunaji hovyo wa miti, sasa limehamia katika miti ya mazao na katika Wilaya ya Kisarawe, mkoani Pwani, miti iliyokumbwa na hali hiyo ni minazi na miembe.
Maeneo yaliyokithiri kwa uvunaji wa miti hiyo ni pamona na vijiji Msanga, Sungwi na Maneromango.
Uchunguzi wa gazeti hili, umebaini kuwa magogo ya miti hiyo yamekuwa yakisafirishwa na kupelekwa katika kampuni zinazojishughulisha na utengenezaji wa vijiti vya meno na sabuni katika maeneo ya Tabata na Mwenge, jijini Dar es Salaam
Inadaiwa kuwa kampuni hizo zinamilikiwa na raia wa China.
Baadhi ya wananchi katika maeneo inakovunwa miti hiyo, waliliambia gazeti hili kuwa wamekuwa wakikata miti na kuiuza ili kujipatia fedha za kujikimu.
Kwa mujibu wa wananchi hao, kila mtu unauzwa kwa bei ya wastani wa kati ya Sh 50,000 na Sh 300,000 kulingana na ukubwa na ubora wa mti unaotakiwa.
Walisema hawaoni sababu ya kutouza miti yao wakati wakikabiliwa na hali ngumu ya maisha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Acquin Ndungwi, alithibitisha habari kuhusu ukataji hovyo wa miti katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo kongwe.
Alisema halmashauri yake imeyakamata magari matatu yaliyokuwa yanatumika kubebea magogo kutoka maeneo ya Msanga, Sungwi na Maneromango.
Ndungwi alisema watuhumiwa waliokutwa wakiwa na magari hayo walikabithiwa kwa maofisa wa Idara ya Maliasili, ili wachukue hatua za kisheria.