Wachina sasa wahamia Msanga

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,792
287,994
Date::1/15/2010Wachina sasa wahamia Msanga
magogo.jpg

Wafanyabiashara ya Magogo na Mbao wakitayarisha bidhaa zao katika kijiji cha Msanga wilayani Kisarawe, tayari kwa kuzisafirisha kwenda Dar es Salaam
Julieth Ngarabali,Kisarawe

WIMBI la uvunaji hovyo wa miti, sasa limehamia katika miti ya mazao na katika Wilaya ya Kisarawe, mkoani Pwani, miti iliyokumbwa na hali hiyo ni minazi na miembe.

Maeneo yaliyokithiri kwa uvunaji wa miti hiyo ni pamona na vijiji Msanga, Sungwi na Maneromango.


Uchunguzi wa gazeti hili, umebaini kuwa magogo ya miti hiyo yamekuwa yakisafirishwa na kupelekwa katika kampuni zinazojishughulisha na utengenezaji wa vijiti vya meno na sabuni katika maeneo ya Tabata na Mwenge, jijini Dar es Salaam


Inadaiwa kuwa kampuni hizo zinamilikiwa na raia wa China.

Baadhi ya wananchi katika maeneo inakovunwa miti hiyo, waliliambia gazeti hili kuwa wamekuwa wakikata miti na kuiuza ili kujipatia fedha za kujikimu.


Kwa mujibu wa wananchi hao, kila mtu unauzwa kwa bei ya wastani wa kati ya Sh 50,000 na Sh 300,000 kulingana na ukubwa na ubora wa mti unaotakiwa.

Walisema hawaoni sababu ya kutouza miti yao wakati wakikabiliwa na hali ngumu ya maisha.


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Acquin Ndungwi, alithibitisha habari kuhusu ukataji hovyo wa miti katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo kongwe.

Alisema halmashauri yake imeyakamata magari matatu yaliyokuwa yanatumika kubebea magogo kutoka maeneo ya Msanga, Sungwi na Maneromango.
Ndungwi alisema watuhumiwa waliokutwa wakiwa na magari hayo walikabithiwa kwa maofisa wa Idara ya Maliasili, ili wachukue hatua za kisheria.
 
Hawa wachina sawa na siafu kilichobaki ni kupigwa marufuku tuu hii idara ya uhamiaji wako wapi hawa ni wabaya kuliko wazungu sawa na siafu hawana maana hata kidogo kwao wameruhusiwa kutoka na kwenda popote kwa wajinga kama tanzania kuzoa mali nakurudisha kwao ngoja tuliwe tutakapozinduka hatutakuwa na kitu kwa vizazi vijavyo
 
..Uchumi wa China unakuwa kwa kasi ya kutisha.

..ndiyo maana Wachina wapo kila mahali kutafuta vyanzo vya malighafi na nishati.
 
Hii stori imepindwa ili kuchochea chuki dhidi ya Wachina. Impression niliyoipata nilidhani labda Wachina wameenda kupiga kambi kwenye hifadhi fulani ya misitu na kuanza kuvuna kinyume cha sheria, kumbe not even close. Wao wanamiliki viwanda, na kumiliki kiwanda sio kosa wala kununua malighafi sio kosa. Tuache kuwanyanyasa na kuwasakama raia wa kigeni bila sababu za msingi. Hii haitotusaidia.

Awali ya yote hivi kuna ubaya gani wananchi wakauza rasilimali zao kama mazao ya shamba au miti? Serikali najua haikuwasaidia kwa lolote hivyo isijitie kimbelembele eti kulinda mazingira. Kila mtu atakula kwa urefu wa kamba yake, sasa wananchi huko walipo hawana njia nyingine ya kutokea, maana mmeshindwa kuwaongoza kuelekea tunu ya maendeleo.
 
watuuuuu piiiiiiipoooooooooooo nimerudi tena. wacha watu wale wqalichopanda na wachina Ongezekeni na mimi niwe na mtoto wa kichina awe mbunifu wa makombora oyeeeeee!!!! dua yangu.. " Ewe mola walete wachina wengi zaidi hapa bongo ili na sisi tuzae na wachina hao na wawe idadi sawa na wadanganyika" amen
 
ukitii na kuamini utakura mema ya nchi kwa nini wasire mema ya tanzania
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom