Mkuu wa Wilaya ya Mlele (Katavi) amewataka wavamizi katika Milima ya Lyamba Lyamfipa kuondoka haraka

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
Mkuu wa Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi amewataka Wananchi wanaofanya shughuli za Kibinadamu katika Milima ya Lyamba Lyamfipa kuondoka haraka kwani milima hiyo ndio yenye uoto wa asili na kutunza vyanzo vya maji.

Kauli hiyo ya Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Majid Mwanga imetolewa katika Kata ya Kasanda Halmashauri ya Mpimbwe Mkoani himo mara baada ya kuona shughuli za Kibinadamu zinafanyika katika milima hiyo ambayo ni muhimu kwa kutunza vyanzo vya maji ambapo amepiga marufuku kufanyoka shughuli za kibinadamu na kuwataka kuondoka haraka.

Shamimu Mwariko ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mpimbwe amesema upandaji wa miti kati milima hiyo na vyanzo vya maji ni muhimu kwa faida ya upatikanaji uoto wa asili pamoja na maji.

Silas Ilumba ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo amesisitiza Serikali kuwaondoa Wananchi wote wanaofanya shughili katika milima hiyo huku Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Joshua Mbwana amesema fedha zote zinazotolewa na serikali zisimamiwe ipasavyo katika kutekeleza miradi ya wananchi.
 
Back
Top Bottom