Naibu Waziri Khamis Chilo Ahimiza Utoaji Elimu ya Mazingira

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,906
945

Naibu Waziri Khamis Chilo Ahimiza Utoaji Elimu ya Mazingira

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis amewahimiza maafisa mazingira nchini kuongeza kasi ya utoaji elimu ya utunzaji wa mazingira kwa wananchi ili kuepusha athari za mabadiliko ya tabianchi.

Ametoa wito huo wakati akizungumza na viongozi pamoja na watumishi wa Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma wakati wa ziara yake ya kikazi ya kufuatilia utekelezaji wa Mradi wa Hifadhi ya Ardhi ya Bonde la Ziwa Nyasa.

Naibu Waziri Khamis amewataka wataalamu hao kusimamia vyema sheria na taratibu za hifadhi ya mazigira ikiwemo utunzaji wa vyanzo vya maji na kusimamia maelekezo ya Serikali ya kupanda miti milioni 1.5 kwa kila halmashauri.

Aidha, amepongeza halmashauri hiyo kwa upandaji wa miti akihimiza lengo la idadi ya miti lililowekwa na Serikali pamoja na kujenga majiko banifu 60 yanayopunguza kasi ya ukataji wa miti kwa ajili ya kuni na mkaa.

Mhe. Khamis pia amewapongeza viongozi na wataalamu hao kwa kuusimamia vyema Mradi wa Hifadhi ya Ardhi ya Bonde la Ziwa Nyasa unaoratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.

“Ninamini miradi hii imeashaanza kuwanufaisha wananchi na target (lengo) ya Serikali iwafikie wananchi kwa wakati na kwa ubora, na hapa nimeona kwenye taarifa yenu imeanza kuwanufaisha wananchi, hongereni sana,“ amesema.

Awali akizungumza, Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mhe. Filberto Sanga amesema anatambua kazi inayofanywa na Serikali hususan katika ujenzi wa miundombinu.

Amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuidhinisha fedha za miradi mbalimbali ikiwemo ya mazingira elimu, maji, afya, umeme, mawasiliano na utalii.

Akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Bw Khalid Khalif amesema utasaidia kupunguza uharibifu wa mazingira kwani wananchi watafanya shughuli za kujipatia kipato.

Ametaja faida ya kijamii inayopatikana ni pamoja na kuongeza usalama wa chakula na kipato kwa kaya kwa kupunguza uharibifu wa ardhi na uharibifu wa Bonde la Ziwa Nyasa.

Bw. Khalif ameongeza kuwa halmashauri imepanda miti 3,500 kwenye vyanzo vya maji katika Kijiji cha Lundo na vijiji jirani sanjari na kukarabati majiko banifu katika maeneo mbalimbali ambayo yatasaidia kupunguza matumizi ya kuni na mkaa.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-10-22 at 18.10.56(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-10-22 at 18.10.56(1).jpeg
    33.8 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-10-22 at 18.10.56.jpeg
    WhatsApp Image 2023-10-22 at 18.10.56.jpeg
    27.6 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-10-22 at 18.10.55.jpeg
    WhatsApp Image 2023-10-22 at 18.10.55.jpeg
    52.2 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-10-22 at 18.10.54(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-10-22 at 18.10.54(1).jpeg
    42.4 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-10-22 at 18.10.53(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-10-22 at 18.10.53(2).jpeg
    25.4 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-10-22 at 18.10.53.jpeg
    WhatsApp Image 2023-10-22 at 18.10.53.jpeg
    52.2 KB · Views: 1
Washajilipa Per diem basi..
Maisha yanasonga.

Si anatuletea kelele tu🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom