kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,319
- 12,622
Simba moyo unataka kucheza nusu finali lakini quality yao inakataa katakata na wana mashaka nayo. Tumaini lao kuu huwa wanalielekeza kwa kocha Benchikha kwakuwa anao uzoefu mkubwa wa kucheza hizi za robo, nusu na finali za caf champions, lakini bahati mbaya Benchikha hataingia uwanjani kuzuia Simba isifungwe wala kuifanya simba kufunga magoli. Ukiwasikia mashabiki wa simba wengi wao hawasifii wachezaji wao tegemeo bali wanamsifia kocha Benchikha kuwa anajua kuzicheza hizi mechi. Wanasimba wana imani kubwa kuwa timu yao ni dhaifu lakini Al-Ahly nayo sasa hivi ni unga (dhaifu). Hii ni tofauti kabisa na wenzao Yanga.
Yanga mara zote kuelekea mechi yao na Mamelodi huwa wanasifia na kutegemea ubora wa wachezaji wao zaidi kuliko kocha wao gamondi. Ni rahisi kuwasikia mashabiki wa yanga kuelekea mechi yao na Mamelodi wakiwasifia sana wachezaji wao akina Pacome, yao, Aucho, Aziz, Mudathir, Nzengeli, Musonda, Mzize na wengine kuliko ubora na uzoefu wa Gamondi. Yanga wanaamini kuwa Mamelodi ni timu imara na tajiri lakini wachezaji wao wana uwezo wa kuifunga Mamelodi.
Wanamwamini zaidi mwalimu wao na wale wanawaamini zaidi wachezaji wao. wacha tusubiri.
Tofauti Yao nyingine ni Simba kuwaamisha wafuasi wao kuwa kulipiwa viingolio kuona mechi live bila malipo ni vibaya sana na Yanga wanawaaminisha wafuasi wao kuingia bila malipo kutawqfanya waende wengi uwanjani usiku na kushangilia timu yao..
Hapo ukweli ni upi? Je mashabiki wa Simba ni kweli hawataki kusaidiwa au viongozi wa Simba wanawasemea tu? Je, ni kweli Yanga kuondoa viingolio kwa mashabiki wao wa mzunguuko kunashusha thamani Yao? Kweli wako watanzani wasiopenda msaada?
Mwisho wa juma sio mbali, panapo majaliwa simba, yanga na Tanzania tutapata darsa jipya kuhusu namna ya kuutazama, kuucheza, kuuchambua na kuushabikia mchezo wa mpira nchini.