Wachangiaji wa Katiba Tanzania ndio hawa!!!

Hawa ni mateja wamekodiwa kujaza ukumbi ili watu makini wasipate fursa ya kuingia na kutoa michango yao yenye tija kwa taifa hili. Hakika anayefadhili mchezo huu mchafu historia itamhukumu.
 
Yani nimecheka mpaka mbavu zauma ivi ccm wana akili kweli?usikute tunaongozwa na vichaaa?
 
nadhani kuna wanaodhani kuwa kuwa huu ni uzushi . ni kweli Tambwe Hiza ndio aliwakusanya hawa vijana kwa ahadi za fedha , usafiri wa kwenda na kurudi na msosi. kazi yao ilikuwa kuzomea wachangiaji ambao wangeipinga rasimu. kama huamini soma waraka wa Bashe kwa viongozi magamba mapya wa CCM ( uko hapahapa JF). kilichijitokeza ni kuwa hawakupewa maagizo vizuri au walichukia baada kuona kuwa hapaelekei kuwa na uwezekano wa kulipwa chao, wakaanza kuwazomea hao hao waliowaleta. nadhani ilikuwa wanalala wakishituka wanakumbuka wamekuja kuzomea basi wanaanza kuzomea ovyoovyo( walimzomea hata Warioba!, walipogundua ni wa kwao na weledi wengine waliopata nafasi chache za kukaa zilizobakia wanamshangilia, na wao wakaanza kumshangilia!!). Hizo ndio Siasa muflisi!!!
 
Inasikitisha, inafedhehesha na inakasirisha.Mizaha ya namna hii kwenye mambo ya msingi haikubaliki. Halafu amani ikivunjika wataisingizia chadema na wakati wao wenyewe (ccm) ndio wanawatia wananchi hasira kwa upuuzi wao.
 
Tatizo letu watanzani ni kwamba tukifanya uchaguzi huwa ni kama tumemaliza kazi niseme kwamba bado tunajukumu la kufuatili na kufanya tathmini, kutofanya hivyo ni tatizo ndio maana leo hii tunaona kumhoji kiongozi kwa baadhi ya meneo ni kosa kubwa,Ni wakati mwafaka kuwajibishana juu ya majukumu yetu kama ilivyo hako katika haki zingine.
 
Back
Top Bottom