Wabunge wataka Milioni 130 badala ya 90 kama mkopo wa gari

Na swala la posho nalo liangaliwe..Laki na nusu per day zinawatosha
 
wapewe mkopo wa landrover. hawa wamekuja na ari ile ile ya mchwa. magufuli inabidi awaonyeshe nini maana ya 'Magufuli for Change'
 
Wabunge wengi ni selfish siku zote huwa wanakumbuka matumbo yaooo
Nyambav zaooo
 
Na swala la posho nalo liangaliwe..Laki na nusu per day zinawatosha

Ya nini hio??Bado ni kubwaa mnoo!!Mshahara wa milion 12 per month unatoshaa saana !!sasa posho ya nn??Ina maana ile sindo kazi yao??

BUNGE NI TAASISI INAYOONGOZA KUKUMBATIA MATUMIZI MABAYA YA FEDHA
 
  • Thanks
Reactions: nao
Wabunge wa chadema kwenye posho na safari za matanuzi hawawezi kutoka nje
 
Ya nini hio??Bado ni kubwaa mnoo!!Mshahara wa milion 12 per month unatoshaa saana !!sasa posho ya nn??Ina maana ile sindo kazi yao??

BUNGE NI TAASISI INAYOONGOZA KUKUMBATIA MATUMIZI MABAYA YA FEDHA
Najua hilo mkuu..Ila sidhani kama zinaweza kufutwa..Labda kupunguzwa
 
Kati ya hizo Mil 130 wao wanalipa nusu Mil 65 na Ml 65 wanalipiwa na serikali. Mr President kata kila kitu,mishahara punguza,posho za vikao ondoa,penshen ya kila miaka mitano ondoa, ruzuku kwa vyama ondoa. Ukifanya hivi Tanzania itakuwa salama. Anayetaka kazi ya uongozi ajue ni kazi ya kujitolea/wito na yenye mshahara mdogo. Kama hukufanya hivi tegemea mauaji kila mara
 
Kwa kweli hii inasikitisha na kuhudhunisha sana.....na tena inakatisha tamaa.....ni vigumu kuamini kuwa wale waliokuwa wakijinadi kwenye kampeni kuwa ni watetezi wetu sisi wanyonge.....ambao wengi ni mafukara.....tena wengine walikuwa wanadiriki hata kushiriki milo nasi kumbe ile ilikuwa ni usanii tu wa kupata kura......na sasa ndio tunaziona ngozi zao halisi......

Siamini kwamba kweli hawa wawakilishi kwa huo mkopo wa shilingi millioni 90 wanaishindwa kupata gari ya kutembelea na kuwafikia wananchi kwa urahisi.....

Nakumbuka wao ndio waliokuwa mstari wa mbele kuishutumu serikali iliyopo MADARAKANI kwa ubadhirifu wa fedha.....kwa matumizi ya kijinga na ya kipumbavu....

Sasa na WAO wana ulazima gani wa kutembelea gari la zaidi ya milioni 130 mbele ya wananchi ambao ni mafukara na hawana UHAKIKA wa kuiona kesho wakiwa hai.....hii ni dhihaka kwa wapiga na walalahoi wote wa taifa hili masikini linalojitahidi kujitoa HUKO shimoni......

Mtaisoma namba ccm ni ile ile ,oh ni ile ile
 
Si wakakope kama haziwatoshi ebhooo kwa nini mnataka kuendekeza watu watu wanaotaka dream life??!!
Mbunge wa kiti maalumu 1kz anaenda nayo wapi????
Mbunge wa Kinondoni, Ilala, Arusha mjini, Moshi mjini hawa wanaenda wapi na Hard top au LX??!!
Ukweli ni kuwa hawahitaji magari ya aina moja, serikali iachane nao kabisa ofisi ya bunge iwe guarantor wakakope kwa mishahara yao uone kama watanunua hayo magari. . . .. .

Imetosha sasa

Kabla ya maelezo yako jiulize wanastahili kuwa na usafiri au hawastahili?
 
Wakati Serikali ikihaha kutafuta fedha
kwa ajili ya kuendeshea shughuli
zake, wabunge wameingia kwenye
mvutano na ofisi ya Bunge kuhusu
fedha ambazo wanastahili kupewa
kwa ajili ya kununulia magari yao.
Mwaka 2010, wabunge walilipwa
Sh90 milioni kwa ajili ya ununuzi wa
magari hayo aina ya Toyota Land
Cruiser (hardtop), ambayo ni vitendea
kazi vyao. Wabunge hutakiwa kulipa
nusu ya fedha hizo wkati nyingine ni
mchango wa Serikali.
Lakini wakati gharama za maisha
zikipanda huku thamani ya Shilingi
ikiporomoka kulinganisha na Dola ya
Marekani na hivyo kusababisha
bidhaa kupanda bei, wabunge
wamekataa kulipwa kiasi hicho cha
fedha mwaka huu na badala yake
wanataka walipwe kulingana na bei
ya sokoni ya magari aina hiyo.
Wabunge wanataka walipwe Sh130
milioni ambazo wanasema ni bei ya
magari hayo kwa sasa baada ya
kupanda bei. Hata hivyo ombi hilo
limegonga mwamba
Wakizungumza kwa sharti la
kutotajwa majina, baadhi ya wabunge
walisema mara baada ya kujisajili
bungeni kwa ajili ya uzinduzi wa
Bunge la Kumi na Moja, katibu wa
chombo hicho, Dk Thomas Kashililah
alifanya kikao na wabunge wote ili
kuwapa taratibu lakini pia
kuwafahamisha stahili wanazopaswa
kupata kama wabunge.
?Katibu alitujulisha kuwa hakuna
ongezeko lolote la posho, hivyo
tunapaswa kulipwa kiasi kilekile cha
Sh300,000 kwa siku .
"Lakini pia alisema tutapewa Sh90
milioni kwa ajili ya mkopo wa gari
badala ya milioni 120 ,? a lisema
mmoja wa wabunge hao.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, suala
hilo liliibua mjadala na kusababisha
wabunge kuhoji iweje kiwango hicho
kitumike katika Bunge la Kumi na
Moja, miaka mitano baada ya
wabunge wa Bunge la 10 kupewa
kiasi hicho.
?Unajua magari tunayotakiwa kununua ni
Toyota Land Cruiser Hardtop, na ukweli
sasa thamani ya magari hayo imepanda
sana huwezi kuifananisha na mwaka
2010 wakati wa Bunge la 10,? alisema
mbunge mmoja.
Wabunge hao walitaka walipwe kiasi
cha Sh130 milioni kwa madai kuwa
ndiyo bei ya sokoni ya magari aina
hiyo.
Mbunge wa viti maalumu (Chadema),
Anatropia Theonest amesema
hawajakataa fedha hizo, lakini
thamani ya Dola imepanda hivyo
kusababisha thamani ya magari hayo
kupanda pia.
?Hakuna asiyejua kwamba thamani ya
Dola imepanda na kwa kawaida kila
Bunge kunakuwa na ongezeko la Sh30
milioni. Mfano Bunge la Tisa walipewa
Sh60milioni la 10 wakapewa
Sh90milioni, hivyo ilipaswa sasa iwe Sh
120mililioni ili kuendana na soko,?
alisema mbunge huyo.
Akizungumzia sakata hilo,naibu
katibu wa Bunge, John Joel alisema
jukumu la ununuzi wa magari ya
wabunge, lipo chini ya Serikali na
siyo ofisi yake hivyo ni bora
wangeulizwa wenye jukumu hilo.
?Tunachofamu sisi mbunge anatakiwa
apewe vitendea kazi likiwemo gari, lakini
wanaohusika na hilo ni Serikali,?
alisema.
Alisema ofisi ya Bunge hushauriana
na Serikali namna ya kutoa huduma
kwa wabunge na kwamba kwa jinsi
anavyofahamu, mpaka jana watunga
sheria hao walikuwa hawajapewa
fedha yoyote ya kununua magari kwa
awamu hii, hivyo wanasubiri
utaratibu.
Wakati Joel akisema Serikali ndiyo
inahusika, Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi Ombeni Sefue aliurudisha
mpira kwenye ofisi hiyo ya Bunge,
akisema uongozi wa bunge
umekwisha pewa maelekezo yote na
serikali juu ya ununuzi wa magari
hayo, hivyo akamtaka mwandishi
akawaulize wao ( uongozi wa bunge)
Katika kukusanya fedha za
kuwezesha kutekeleza mipango ya
Serikali na ahadi alizotoa wakati wa
kampeni, Rais John Maguguli
alitangaza hatua mbalimbali za
kudhibiti matumizi, na akawaeleza
wabunge mwishoni mwa wiki kuwa
hataweza kufanikiwa iwapo hatapata
ushirikiano wao.
Katika kuonyesha kuwa anatoa kauli
thabiti, Dk Magufuli aliagiza fedha
ambazo zilichangwa na taasisi
mbalimbali za fedha kwa ajili ya hafla
za kuwapongeza wabunge,
zielekezwe kwenye ununuzi wa vifaa
tiba kwenye Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili.
Tayari Rais ameshafuta safari za nje
isipokuwa kwa kibali cha Ikulu baada
ya mtu anayetaka kusafiri kutimiza
masharti kadhaa, likiwamo
linalomtaka aeleze faida ya safari
yake na kama iwapo hatasafiri, nchi
itaathirika vipi.
 
Kama kweli hilo tinga tinga lina meno ,namsubiria kwenye hii ishu ya wabunge ,wakati kwenye speech yake alisema atahakikisha wabunge wanapata fedha zao kwa wakati ikiwa ni pamoja na fedha za majimbo yao .
Mtihani wa kwanza wamemtega na mashangingi Tinga tinga akitoboa hapo kitakachofuata ni kum impeach ,ccm ni ile oh ni ile ,mtaisoma namba
 
Mbona mnajadili ujinga wewe unaambiwa ni mkopo kwani tangu lini mtu kapangiwa achukue ngapi mkopo ni haki yao na jinsi ya kutumia wanajuwa wao hivyo kuingiza maneno ni ujinga
Sawia Mkuu tatizo watu wanashindwa kutofautisha mkopo na kupewa,ndio maana wameshupalia kinoma
 
Kama ni haki yao kupewa vitendea kazi ikiwemo gari basi ningeshauri serikali ikanunue magari yawe ya aina moja kwa wabunge wote halafu iwakopeshe nadhani watakua wamesolve tatizo la usafiri
 
Back
Top Bottom