Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,903
- 945
Mbunge Simon Lusengikile: Gari ya Milioni 120 Yauzwa Milioni 8
MBUNGE wa Jimbo la Busega, Simon Lusengikile ameitaka Wizara ya Fedha kuja na mpango utakaoonesha ni namna gani uthaminishaji wa magari ya Serikali unafuata bei ya soko kabla ya kuuza magari hayo.
Akichangia hoja ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Lusengikile amesema kuwa lipo tatizo kubwa katika mchakato wa kuthaminisha magari ya Serikali kabla ya kuyauza.
Ametoa mfano wa gari la Serikali aina ya V8 lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 120 lililokuwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Rorya ambalo liliuzwa shilingi milioni nane baada ya kufanya kazi miaka kumi tu na bado likiwa katika hali nzuri.
Aidha, ameongeza kuwa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa imeona kuna changamoto ya kutokuwa na uwazi wakati wa kuuza magari ya umma.
Amesema taarifa ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) inaonesha kuwa katika taasisi nane zilizokaguliwa, sita kati ya hizo hazikuwa na uwazi katika kuuziana magari.