Si kweli kwamba Wabunge wameongezewa mshahara

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,703
36,143
Naungana na bunge kukanusha taarifa za Mh. Mbowe kuwa wabunge wameongezewa mshahara kutoka sh. Milioni 13 mpaka milioni 18.

Kwanza tangu tupate uhuru wa nchi hii serikali haijawahi kumlipa mbunge yeyote mshahara wa milioni 13.
turudi kweli mada.

Jamaa wajanja wamejiongezea posho na sasa kufanya jumla ya sh. Milioni 18 (posho +mshahara).

Kwahiyo bunge limekanusha kimehesabu. Mshahara hawajaongeza ila posho wamefanya kitu juu ya kitu.

Posho
Posho
Posho
Posho.
 
SALARY SLIP YA MBUNGE : TAX FREE?

Mshahara wa mbunge wa zaidi ya bilioni moja kila mwaka (miezi 12) ktk kikokotoo:


Mchanganuo wa mshahara wa miaka mitano wa mbunge ni Bilioni 1 na milioni themanini :

Shilingi 18,000,000 x miezi 12 = 216,000,000

Shilingi 216,000,000 × miaka 5 =1,080,000,000
  • Bado hapo pia anapokea allowance za vikao vya bajeti
  • Ziara za mafunzo Dubai, India n.k
  • Vikao vya Kamati za Kudumu za Bunge PAC, LAAC, Mambo ya Nje na ulinzi usalama n.k
  • Marupurupu ya mkopo wa gari n.k
  • Bima ya Afya kwa mbunge hospitali VIP Class n.k
  • Pensheni ya mkupuo akimaliza ubunge miaka
 
Kama vile tunavyoshauriwa kama wenye ajira pesa haitoshi wafungue vimiradi vya hapa na pale na hawa tuwapunguzie mishahara / marupurupu mpaka ngazi ya waalimu / vikao waanze kufanyia zoom wakiwa majimboni kwao na kama pesa haitoshi wafungue magenge ya nyanya kama wengine wanavyofanya kama vipi waulize wanaowawakilisha wanaishi vipi kwa mwaka mzima kwa pesa ambayo hawa ni kama posho ya Kikao kimoja....

Tunawapenda sana ila kwa hali yetu ya kimaisha we can not afford them....
 
Back
Top Bottom