MKJJ nakubaliana na wewe kuwa katika kujenga demokrasia lazima kuwe na uhuru wa kutofautiana kimawazo hasa ndani ya chama, lakini uhuru bila mipaka ni fujo. Sikatai Zitto kutofautiana kimawazo lakini yeye kama kiongozi hata kama si kiongozi hawezi kuwa anatoa siri za chama nje bila kuwasiliana na viongozi wenzake. Ningekuwa mimi nimesema kuwa kuliwa na kutofautiana kwenye maamuzi hata kama ni kweli uzito hauwezi kulingana wa kiongozi kama yeye hasa ukizingati swala tete kama hili.Hakuna ulazima wa haya jamani; Zitto anajua anachofanya na kukoleza demokrasia ndani ya CHADEMA. Hatutaki kurudi kwenye chama ambacho wote wanafikiri vile vile, wanazungumza lugha ile ile na wanamwelekeo ule ule.. demokrasia ya kweli nipamoja na kuruhusu dissent. Haiwezekani kila kiongozi akiwa na mawazo tofauti basi atimuliwe. Tunaweza tusikubaliane na sababu alizozitoa Zitto kwanini hajakubaliana na wenzake, lakini ni lazima tutetee na kuilinda haki yake kutoa mawazo hayo bila hofu ya kutishiwa rungu la "nidhamu ya chama".
Petition Zitto afukuzwe Chadema
Ninazo sababu;
Ingawa yeye na baadhi ya watu wanamtetea kuwa hizo ni njama za CCM lakini kuna matukio anayoyasababisha yeye mwenye ama kwa makusudi au kwa kutokujua ambayo huwezi kuisingizia CCM.
Hizi ni baadhi ya sababu zilizonifanya nifikie uamuzi huu mgumu:
Kwenye sakata la ama kununuliwa au kutonunuliwa kwa mitambo ya Dowans Zitto alitofautiana na msimamo wa viongozi wake na msimamo wa Chadema kwa ujumla.
Huku akijua kuchukua form na kugombea uenyekiti kungesababisha mgogoro mkubwa wakati wa uchaguzi wa ndani wa Mwenyekiti, Zitto alionyesha waziwazi mbele ya vyombo vya habari kutoridhishwa na uamzi wa wazee wa chama kuombwa kujitoa kiasi cha kusababisha kuzaliwa kwa makundi mawili ndani ya chama.
Kutofanyika kwa chaguzi za ndani za Baraza la vijana BAVICHA na Baraza la wanawake BAWACHA inasemekana mkono wa Zitto pia ulihusika kiasi cha kuleta makundi na chaguzi kusimamishwa.
Wakati chama kikiendelea na kampeni mwaka huu Zitto alisikika akisema uchaguzi ujao atagombea urais huku akijua kitendo hicho kingetumiwa na wapinzani kuwagombanisha na wapiga kura.
Zitto amekuwa akipinga maamuzi mengi ya chama waziwazi kiasi cha kuleta minong'ono ndani na nje ya chama. Ingawa ana uhuru na utashi wake lakini yeye kama kiongozi anatakiwa atoe ubinafsi na kuweka chama mbele, mfano kupinga uamuzi wa chama kuwasimamisha kina Kafulila na wenzake.
Zitto amekuwa akiongea habari za chama zingine za siri kwenye vyombo mbalimbali vya habari mfano kutumia FACEBOOK bila kujali utaratibu uliowekwa na chama.
Leo ameongea siri za chama kuhusu upigaji kura wa ama kususia hotuba ya rais au la bila kuangalia athari zitakazosababishwa na kitendo chake hicho.
Kwa sababu hizi na zingine ambazo ni siri ya chama; ili kukinusuru chama na mgawanyiko unaoweza kutokea naomba kupendekeza yafuatayo:
1. Chama kimuonye Mh. Zitto aache tabia yake hiyo inayokishushia heshima chama. AMA
2. Zitto anyang'anywe vyeo vyake vya juu vya chama hadi hapo atakapojirekebisha(kukomaa). AU
3. Ili kukilinda chama kisigawanyike kabla ya uchaguzi mkuu ujao chama kichukue uamuzi mgumu (mapema) wa kumsimamisha Zitto uanachama. Ni bora kupoteza jimbo moja kuliko kupoteza chama kizima kinachotegemewa kuleta mapinduzi Tanzania.
Naomba kutoa hoja.
Hakuna ulazima wa haya jamani; Zitto anajua anachofanya na kukoleza demokrasia ndani ya CHADEMA. Hatutaki kurudi kwenye chama ambacho wote wanafikiri vile vile, wanazungumza lugha ile ile na wanamwelekeo ule ule.. demokrasia ya kweli nipamoja na kuruhusu dissent. Haiwezekani kila kiongozi akiwa na mawazo tofauti basi atimuliwe. Tunaweza tusikubaliane na sababu alizozitoa Zitto kwanini hajakubaliana na wenzake, lakini ni lazima tutetee na kuilinda haki yake kutoa mawazo hayo bila hofu ya kutishiwa rungu la "nidhamu ya chama".
Kwa wasiofahamu ccm imefikia kuwa chama cha kidikteta kwa sababu ya kuzuia sauti yenye msimamo kinzani ndani ya chama. Mimi nilikuwa mwanachama wa ccm na nilikitumikia kwa moyo wangu wote. Lakini mwaka 2006 niliwarejeshea kadi yao baada ya kubaini udikteta mkubwa ndani ya chama hicho. Kwa ufupi, kwenye vikao vya ccm ukitofautiana na msimamo wa wakubwa basi wewe unatazamwa kama muasi na unaweza kuanza kuandamwa kama adui.
Bado sijajiunga na chama chochote cha siasa lakini kwa utafiti wangu binafsi naelekea kushawishika kujiunga na CDM. Ninaamini ndani ya CDM kuna demokrasia ambapo mojawapo ya ishara zake ni kuruhusu mawazo kinzani. Naamini kuwa CDM inaheshimu wanachama wenye mawazo tofauti na haiwachukulii kuwa ni maadui. Na kama haifanyi hivyo, basi nitumie fursa hii kuwashauri waanze mara moja. Kama mhe. Zitto Kabwe amekuwa akitofautiana sana na viongozi wengine kwenye vikao vya chama, basi wachukulie kuwa hiyo ndiyo demokrasia. Muhimu hapa ni kuheshimu maamuzi ya chama kupitia vikao vyake halali. Hata kama wanachama kadhaa wanapinga suala fulani lakini kura zikipigwa na kuonekana wengi wanaunga mkono, basi huo unachukuliwa kuwa ndiyo msimamo wa chama na ndiyo unaopaswa kuheshimiwa na wanachama wote.
MKJJ nakubaliana na wewe kuwa katika kujenga demokrasia lazima kuwe na uhuru wa kutofautiana kimawazo hasa ndani ya chama, lakini uhuru bila mipaka ni fujo. Sikatai Zitto kutofautiana kimawazo lakini yeye kama kiongozi hata kama si kiongozi hawezi kuwa anatoa siri za chama nje bila kuwasiliana na viongozi wenzake. Ningekuwa mimi nimesema kuwa kuliwa na kutofautiana kwenye maamuzi hata kama ni kweli uzito hauwezi kulingana wa kiongozi kama yeye hasa ukizingati swala tete kama hili.
MODS heading uliyoiweka haiendani kabisa na maudhui niliyokusudia, mtu akisoma heading na kukuta kitu tofauti wa kupuuzwa ni mimi siyo wewe MODS. Ningeshauri kama haiwezekani kurudisha heading ya mwanzo jaribu kuangalia heading nyingine iendane na maudhui yaliyopo au kama haiwezekani kabisa bora ifute thread nzima, kwa sababu lengo la heading uliyoiweka ni kunigombanisha na watu wengi wakati si lengo langu. Asante. Heading yangu ilisomeka
Nakupa big up?
Heading ya mwanzo ndiyo yenye kuwakilishwa yaliyomo kwenye hoja.Mods kabda ya kubadili heading labda ingekuwa bora kufanya consultation na mweye thread!
Yote ni yote message sent.