Wabunge waliokataa "kutoka" wafukuzwe/waonywe na Chadema kwa msimamo wake?

Samahani wanaJF Heading imebadilishwa ambayo haiendani na maudhui niliyokusudia sitaki kuonekana mbabaishaji post nimeifuta.

Good, Tunataka hapa ukweli na habari kamilifu tujadili mustakabali wa taifa letu.
 
...... Muhimu hapa ni kuheshimu maamuzi ya chama kupitia vikao vyake halali. Hata kama wanachama kadhaa wanapinga suala fulani lakini kura zikipigwa na kuonekana wengi wanaunga mkono, basi huo unachukuliwa kuwa ndiyo msimamo wa chama na ndiyo unaopaswa kuheshimiwa na wanachama wote.

Na huo ndio msingi wa Criticism kwa kauli ya Zito!
 
Mods kubadilisha Heading ni udikteta.
Na mbaya zaidi mwanzisha mada mwenyewe hakubaliani na heading uliyoiweka.
Kama vp Mod si ungeanzisha thread yako yenye heading unayoitaka wewe!

Sioni maana ya ile slogan "...we are dare to talk openly"
Unajua Ndibalema MODS sometimes wamekuwa na maamuzi yao ya kulazimisha kwa vile hii ni blog yao lakini kama wanafikiri hivyo si sahihi.

Heading yangu ilikuwa inamlenga mtu mmoja Zitto kwa makusudi kabisa si wabunge waliokataa kutoka, hata hivyo ukiangalia hakuna mbunge wa CDM aliyekataa kutoka wabunge wote waliokuwemo bungeni walitoka. Sasa sikuelewa MODS walikuwa na maana gani kuweka heading hiyo ambayo inapotosha wanaJF, ndiyo maana nikawaomba kama ndivyo waifute thread hii haina maana.

Ieleweke ugomvi wangu au lengo la thread hii si wabunge waliokataa kutoka(kwanza hawapo) wafukuzwe wala si kitendo cha Zitto kupingana na wenzake, ugomvi wangu uko wazi kabisa si Zitto kukataa kwenda bungeni ni yeye kuendelea kutoa siri za chama hadharani kwa kisingizio cha uhuru wa mawazo, huo sio uhuru tunaouhitaji kwa sasa hiyo ni FUJO.
 
Hakuna ulazima wa haya jamani; Zitto anajua anachofanya na kukoleza demokrasia ndani ya CHADEMA. Hatutaki kurudi kwenye chama ambacho wote wanafikiri vile vile, wanazungumza lugha ile ile na wanamwelekeo ule ule.. demokrasia ya kweli nipamoja na kuruhusu dissent. Haiwezekani kila kiongozi akiwa na mawazo tofauti basi atimuliwe. Tunaweza tusikubaliane na sababu alizozitoa Zitto kwanini hajakubaliana na wenzake, lakini ni lazima tutetee na kuilinda haki yake kutoa mawazo hayo bila hofu ya kutishiwa rungu la "nidhamu ya chama".

MKJJ what about "Collective Responsibility" au "Uwajibikaji wa Pamoja"? Kama yale yalikuwa ni maamuzi ya chama katika kikao halali na kura zikapigwa, ilikuwa ni jukumu la wote kutenda hata kama hutaki. Ndiyo maana ya Demokrasia ya kweli. Kutoka nje na kuelezea tofauti zilizojitokeza ndani ya chama ni upuuzi uliotukuka.

Hoja ya kuwa na Spika mwanamke kutoka CCM bila ya shaka iliwagawa. Lakini baada ya maamuzi yale umemsikia yeyote including Sitta akilalamika katika media?

No matter how good Mr. Zitto Kabwe might be, lazima aelewe kuwa ukomavu wa kiuongozi ni pamoja na kulinda maslahi ya chama hasa katika suala nyeti kama hili ambalo ni hot debate kwa taifa zima sasa hivi.
 
Back
Top Bottom