Wabunge wakomaa: Ngeleja, Jairo watakiwa kuondoka; Pinda ataka mjadala uahirishwe kwa siku 21

Status
Not open for further replies.
sijui ntakuta umeme leo home.....maana hata nguo ya kazini sijanyoosha, sina umeme siku ya nne sasa halafu walivyo wajinga mwisho wa mwezi wanakuletea bonge la bill yaani mwezi huu ntamkata mtu biology yake...........
 
Ngeleja anahojiwa na Rahel Mhando wa TBC sasa..

Anasema kaichukulia hoja kichanya zaidi,anashukuru michango ya wabunge na msimamo wa serikali...Anasema fedha zilizotengwa ni kidogo,kunahitajika jhudi za ziada(fedha za ziada).....Hoja ya msingi ilikuwa ni kuongeza fedha ili kutatua tatizo,wanakwenda kujipanga kuangalia fedha zitatoka wapi,watahusisha wizara/taasisi zingine ili kufanikisha upatikanaji wa fedha hizo'

Kuhusu taarifa za uongo kwenye kitabu/hotuba za bajeti amesema kwamba ni makosa ya kibinadamu(aisee),makosa ya kiuchapaji,kasoro za kitakwimu,na kufanya rejea ya baadhi ya miradi(anazungumzia la mbunge wa Nkasi)....

Anasema angepewa fursa ya kuzungumzia bungeni ingeonekana tofauti..

Kuhusu Jairo...Anasema hawezi kusema chochote,anasubiri uamuzi wa Rais,kusema chochote atakuwa anazungumzia madaraka ya mkubwa wake....Anaulizwa kama alikuwa analijua hili kabla...anababaika,mtangazaji wa TBC anaondoka.......Inasikitisha sana
 
jairo nae chizi tu...unaandika baria kienyeji namna hii ?! barua ya dili kaandika kijinga abisa hana maana hata kidogo....
 
Ni habari njema wabunge wa vyama vyote wameungana kukataa makadirio ya wizara. Ni furaha sasa maswala ya kitaifa yanapewa kipaumbele bila kujali chama
 
Hii ni rushwa na kwa kweli huu ndiyo wakati ambao Rais wetu mpendwa anatakiwa kuchukua hatua za haraka kuwatia adabu watu hawa ambao wanatumia fedha za umma kuhonga na kupitisha mambo amabyo si ya maslahi ya umma.
Unfortunately, hao watu unaowasema wachukuliwe hatua ni marafiki zake rais wenu mpendwa.
 
Mnyika anasema pamoja na swala la umeme pia kuna mambo ya madini ambayo serikali inatakiwa kutoa ufafanuzi vinginevyo watahamasisha wananchi kuandamana nje ya bunge.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom