Wabunge wakomaa: Ngeleja, Jairo watakiwa kuondoka; Pinda ataka mjadala uahirishwe kwa siku 21

Status
Not open for further replies.

Maxence Melo

JF Founder
Feb 10, 2006
4,230
13,415
Wakuu,

Taarifa niliyoipata toka kwa source wetu ndani ya kikao cha CCM huko Dodoma zinashtua kidogo.

Wabunge wa CCM wamepandisha mori wakitaka Jairo (Katibu Mkuu wa Wizara) atimuliwe na wakaendelea kutishia kuwa hata Ngeleja naye anatakiwa kuachia ngazi.

Wabunge wa CCM wamemtaka Jairo ajiuzulu kutokana na kashfa ambayo imeletwa na Shelukindo juu ya Barua aliyoandika kuzitaka taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati na Madini zitoe 50mil kila moja ili kupata pesa ya ku-lobby ili bajeti ipite.

Wameitaka serikali kupunguza 20% ya bajeti za 'Other Charges' na pesa zote za kujenga majengo ya Wizara ili ziende kwenye UMEME ama vinginevyo bajeti haipiti na Ngeleja atatakiwa kujiuzulu mara moja.

UPDATES:

Waziri Mkuu Mizengo Pinda kaomba mjadala uahirishwe mpaka baada ya wiki tatu ili waweze kujipanga upya. Kaonyesha kusikitishwa na kitendo cha Jairo na kasema ingekuwa ni kwa hiari yake (bila kumsubiri rais) angechukua maamuzi haraka sana
 
Tupo pamoja mkuu. hawa jamaa hawawezi kutuchezea akili kiasi hiki. wakipitisha bajeti hii tu tunaiingia street. Enough is enough. Ikulu pamekuwa pango la walanguzi na wanyanganyi.
 
Wabunge wa CCM wamemtaka Jairo ajiuzulu kutokana na kashfa ambayo imeletwa na Shelukindo juu ya Barua aliyoandika kuzitaka taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati na Madini zitoe 50mil kila moja ili kupata pesa ya ku-lobby ili bajeti ipite.

Wameitaka serikali kupunguza 20% ya bajeti za 'Other Charges' na pesa zote za kujenga majengo ya Wizara ili ziende kwenye UMEME ama vinginevyo bajeti haipiti na Ngeleja atatakiwa kujiuzulu mara moja
 
Naskia kuna wabunge wametumia maneno makali hadi wakaambiwa wanatoa faida kwa upinzani....ila ishu ya Jairo umekuwa msumari wa Moto kwa ngeleja
 
Nitaaondoa kauli yangu ' akili kama za wabunge wa ccm' jioni wakikaa kama kamati, asante kwa taarifa
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom