Wabunge wakomaa: Ngeleja, Jairo watakiwa kuondoka; Pinda ataka mjadala uahirishwe kwa siku 21

Status
Not open for further replies.
HAIJAPITA MKUU SOMA HAPA

Wabunge wa CCM wamepandisha mori wakitaka Jairo (Katibu Mkuu wa Wizara) atimuliwe na wakaendelea kutishia kuwa hata Ngeleja naye anatakiwa kuachia ngazi.

Wabunge wa CCM wamemtaka Jairo ajiuzulu kutokana na kashfa ambayo imeletwa na Shelukindo juu ya Barua aliyoandika kuzitaka taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati na Madini zitoe 50mil kila moja ili kupata pesa ya ku-lobby ili bajeti ipite.

Wameitaka serikali kupunguza 20% ya bajeti za 'Other Charges' na pesa zote za kujenga majengo ya Wizara ili ziende kwenye UMEME ama vinginevyo bajeti haipiti na Ngeleja atatakiwa kujiuzulu mara moja.

UPDATES:

Waziri Mkuu Mizengo Pinda kaomba mjadala uahirishwe mpaka baada ya wiki tatu ili waweze kujipanga upya. Kaonyesha kusikitishwa na kitendo cha Jairo na kasema ingekuwa ni kwa hiari yake (bila kumsubiri rais) angechukua maamuzi haraka sana
 
Sasa sijuhi hizo ela huyu katibu mkuu alifanikiwa kuzikusanya? Na kama alifanikiwa sijuhi amemgawia nani?? Ahh. Ingekuwa kwa wenzetu mbona tungejua cheni ya wabunge wote waliopewa huo mshiko budget ipite asilimia mia kwa mia.
Nina wasiwasi na Mh Mkapa wa Nanyumbu alipewa. Aliongea upupu upupu tu.
 
CCM - Chama Cha Mapacha lakini watatu watatu !

Attachments

  • umemejamani(1).jpg
    umemejamani(1).jpg
    43.3 KB · Views: 36
Siku,miezi na hatimaye mwaka sasa toka sakata maarufu kama sakata la Jairo limepita bila kujua hatima yake nini.Bunge lilielezwa kila kitu,waliohongwa nao walitajwa lakini hatuoni hatua madhubuti za kisheria zikichukuliwa.Sipendi kuamini kulikuwa na mapango maalumuuliondaliwa kuwang'oa watu fulani kwa maslahi fulani.

Pia sipendi kuamini kilichofanyika ni funika kombe mwanaharamu apite.Ikiwa dhana nzima ilikuwa ni kusafisha serikali kwanini basi watuhumiwa wa sakata la Tanesco kupitia wizara ya nishati na madini na wenzao walioadabishwa wasichanganywe pamoja kutoa dhana inayotaka kujenga miongoni mwetu kuwa ule ulikuwa mchezo wa kuigiza.

Mbaya zaidi mpaka mawaziri wetu na wabunge wetu nao pia walihongwa,kiasi cha waziri mkuu naye kupata chake kwa staili ya posho ya kikao.Kama kweli ule msemo wa kisheria unao sema sheria ni msumeno basi sasa ndiyo wakati wake kuutumia vizuri ili kujenga imani kwa wananchi.

Hatuwezi kuwaacha hivi hivi viongozi wetu ambao wamegueka wasaliti na kujifanya kupe kwa kuinyonya nchi yetu bila aibu.utawala ule tulioaminishwa kuwa ni wa sheria uonekane sasa ukifanya kazi yake,tusisubiri mpaka wafadhili watishie kutokutupa misaada ndipo tukurupuke na kuchukua sheria.

Maamuzi mengi ndani ya nchi yetu yamekuwa ya kizimamoto zaidi tena yasiyo na tija kwa mustakabali wa maendeleo ya nchi.Bunge linatunga sheria inayo toa nafasi kwa mafisadi kuzidi kujimilikisha rasilimali zetu,kwa kuwa tu adhabu zake hazikidhi haja ya kumudabisha mkosaji.Ndiyo maana matukio ya uvunjaji wa sheria na uwizi wa mali ya umma umekuwa ukiongezeka siku hadi siku.

Mwaka 1984,wahujumu uchumi walikamatwa bila kujali sheria kama ipo,lakini bunge lilikaa na kutunga sheria ya uhujumu uchumi na sheria ikachukua mkondo wake,sasa tuna shindwa nini ikiwa tuna wabunge wengi tena, nzuri zaidi wengi wao wana taaluma ya sheria.Turekebishe sheria ili adhabu zitazo tolewa na mahakama zilete tija na kuwa fundisho kwa wale watako thubutu kuigeuza nchi shamba la bibi

Wakati sasa umefika wananchi tuelezwe hatima ya sakata la Jairo na wenzake limefikia wapi.Sakata hili liliikumba hata ikulu yetu kwa katibu mkuu kiongozi kutoa maamuzi ya kishabiki na kiushindani bila kujali bunge ni chombo cha kuisimamia serikali.Mapendekezo ya bunge yalimtaka aliyekuwa katibu mkuu kiongozi bwana Philipo Luhanjo awajibishwe lakini ajabu na kweli mheshimiwa huyu ameachwa apumzike na kulipwa mafao yake bila kujali kuwa ni miognoni mwa watuhumiwa kwa namna moja au nyingine.

Wapo wengi tu ambao wana stahili kufikishwa kwenye mkono wa sheria lakini wapo mitaani wanapeta bila kuchukuliwa hatua,diyo maana napata shaka kuwa mchezo huu unaoendelea ndani ya bunge yawezekana ukawa ni the comedy.Nina liasa bunge letu kama mhimili mkuu wa kuisimamia serikali ujitambue na kujua wajibu wake nini,ikibidi liihoji serikali ni kwanini haitekelezi maazimio yaliyokusudiwa na bunge hilo linalotumia pesa za walipa kodi.

Kuna haja gani ya kuwa na bunge kiboyo,ambalo haliwezi kutafuna nyama kiasi cha kupelekea wananchi kukata tamaa na serikali ,bunge pamoja na mahakama.Ifike wakati kulindana kwa staili ya mwenzetu ikome kabisa ndani ya nchi yetu na kila mhimili uheshimu madaraka na utendaji wa mhimili mwingine bila kuingiliwa.Kamwe hatuwezi kuwa na bunge linaloongoza kuvunja sheria nasi tukakaa kimya kama mbuzi wa kafara anaye subiri kuchinjwa.
 
Bofya hapa: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...taka-mjadala-uahirishwe-kwa-siku-21-a-23.html

Naona hii link ina utata. Hii nimeichukua kutoka hiyo link hao juu iliandikwa na Maxence

Wakuu,

Taarifa niliyoipata toka kwa source wetu ndani ya kikao cha CCM huko Dodoma zinashtua kidogo.

Wabunge wa CCM wamepandisha mori wakitaka Jairo (Katibu Mkuu wa Wizara) atimuliwe na wakaendelea kutishia kuwa hata Ngeleja naye anatakiwa kuachia ngazi.

Wabunge wa CCM wamemtaka Jairo ajiuzulu kutokana na kashfa ambayo imeletwa na Shelukindo juu ya Barua aliyoandika kuzitaka taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati na Madini zitoe 50mil kila moja ili kupata pesa ya ku-lobby ili bajeti ipite.

Wameitaka serikali kupunguza 20% ya bajeti za 'Other Charges' na pesa zote za kujenga majengo ya Wizara ili ziende kwenye UMEME ama vinginevyo bajeti haipiti na Ngeleja atatakiwa kujiuzulu mara moja.

UPDATES:

Waziri Mkuu Mizengo Pinda kaomba mjadala uahirishwe mpaka baada ya wiki tatu ili waweze kujipanga upya. Kaonyesha kusikitishwa na kitendo cha Jairo na kasema ingekuwa ni kwa hiari yake (bila kumsubiri rais) angechukua maamuzi haraka sana

Suala hapa, nini hatima yake pamoja na wote wale waliopewa posho ambazo hazikubaliki kisheria.Kuwa nje ya uwaziri hiyo ni kesi nyingine lakini kuwa huru ili hali umefanya madudu kwa kutumia madaraka vibaya kisheria haikubaliki ndo maana nnina hoji.Shaka kubwa isiwe tu ndo picha ya kihindi sterling kauwa na ndo mwisho wa picha.
 
Mkuu sisi hatuna bunge linalojua wajibu wake.Ukitafakari vizuri utagundua kuwa bunge na serikali wanashirikiana kutuhujumu na ndio maana hata maazimio yao hawayasimamii.Zili kele kele ni unafiki na kithibitisho ni kuunga hoja mkono kwa asilimia miamoja kila bajeti na kila mwaka wa fedha.
 
Ni ukweli usio pingika lakini isiishia hapa tu wakija kwenye majimbo yetu,tuwaulize ni kwanini wamekubali kuwa rubber stamp na kutumika kama chombo cha kupitishia madudu ya serikali na kusahau wajibu wao kama chombo cha kuisimamia serikali.

Pia,kwanini tusiwawajibishe kwa kuligeuza bunge sleeping hall,ilihali si kazi tuliyowatuma huko bungeni
 
Suala hapa, nini hatima yake pamoja na wote wale waliopewa posho ambazo hazikubaliki kisheria.Kuwa nje ya uwaziri hiyo ni kesi nyingine lakini kuwa huru ili hali umefanya madudu kwa kutumia madaraka vibaya kisheria haikubaliki ndo maana nnina hoji.Shaka kubwa isiwe tu ndo picha ya kihindi sterling kauwa na ndo mwisho wa picha.
Hakitaeleweka mpaka tufumue system nzima ya kiutawala hapa nchini I mean tupige chini CCM tuwajaribishe na CHADEMA.
Coz sijui nani wakumwamini 100%.
 
Hakitaeleweka mpaka tufumue system nzima ya kiutawala hapa nchini I mean tupige chini CCM tuwajaribishe na CHADEMA.
Coz sijui nani wakumwamini 100%.

Nakubaliana nawe,lazima tuweke mfumo ndani ya mioyo yetu sisi wapiga kura utakaopingana na mfumo dume uliopandikizwa na watawala.Tuwe na maamuzi ya kuwapima wakishindwa watoke tuwape wengine.Lakini si kutoka tu bali kama walitumia madaraka vibaya lazima tuwapeleke gerezani.Pia kwa haya yanayo tokea CCM wana hitaji likizo ya miaka hamsini kama walivyoitumia miaka 50,hapo ndipo uwanja wa siasa utakuwa fair ground.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom