Wabunge waigeuka TANESCO

Nadhani umefika wakati sasa kwa wananchi kufikiri jinsi ya kuwawajibisha wabunge wao. Sioni sababu kwa nini mwanakijiji anaeishi maeneo ya karibu na mtera akose umeme wakati umeme unazalishwa maenea hayo. Sio sababu ya mwananchi anayeishi along or jirani na gridline kuelekea dar es salaam kuendelea kutegemea kibatari. Hawa wabunge wasitudanganye hapa, wanaongea tuuu ilimradi wasikike radio tanzania au magazetini.

Wabunge hebu kuweni wakweli kwa wananchi wenu na msijikombe sana kwa chama chenu, muogopeni Mungu kwa kutokubali kuwa wanafiki na rubber stamps.
 
Wanaofanya maamuzi kuhusiana na TANESCO na kusaini mikataba hewa akina fisadi Mkapa na wengineo mikataba ya IPTL, RICHMOND, Songa na Net group ambayo imekuwa na athari kubwa katika utendaji wa shirika hilo, halafu wa kulaumiwa ni watendaji wakuu wa TANESCO eti kwa kuwapeleka watoto wao kusoma nje! :confused:

Juzi juzi wafanyakazi wa TANESCO waliandamana na kusema hadharani kwamba utendaji ndani ya shirika hilo unaathiriwa zaidi na mikataba mibovu. Hawakuzungumzia kabisa watendaji wa juu wa shirika hilo, je wana nasaba nao gani mpaka wasiwataje kwamba nao wanahusika katika kulegalega kwa shirika hilo?. Na hawa wafanyakazi wamo ndani ya TANESCO wanajua kwa undani zaidi yanayoendelea ndani ya shirika hilo kuliko wabunge wanaosema bila kujua wasemalo. GET REAL!

Sasa hawa ulitegemea waseme nini? Kuwa wao ndio wenye matatizo? Kama walivyouliza wengine, umewahi kuomba kuunganishiwa umeme na Tanesco? Wote tunajua kuwa the buck stops kwenye menejimenti! Hauwezi wewe bosi uliyepewa dhamana ukawatupia lawama mafundi mchundo kuwa wanahujumu shirika bila kuonyesha hatua gani unazowachukulia. Kwa taarifa yako ni hawa hawa wanaojifanya kuandamana leo ndio mwanzo mkuu wa matatizo katika mashirika yetu! Ni hao hao ambao wanashiba katika hali hiyo ya uzembe uliokuwepo kwenye mashirika yetu. Narudia matatizo katika mashirika yetu hayakuanza na Net Group, IPTL, Richmond na wengine. Tulikuwa nayo kabla hawa hawajaja na tunayo baada ya wao kufika. Ninachokataa mimi ni kutumia hii mikataba mibovu kama fig leaf ya uzembe na matatizo yetu. Badala ya kuyatupitilia nje madai ya hao wabunge, tudai watoe uthibitisho. Wakishindwa ndiyo mtoe hizo shutuma mnazotaka kutoa. Lakini kuhusu utendaji wa shirika hili, hakuna haja ya uthibitisho. Ni wazembe na inabidi tuwavalie njuga wajirekebishe. Kwa kuachia haya mashirika yafikie mahali yanapofika ndiyo maana tukitaka mtu wa maana wa kuwekeza wanajitokeza matapeli tu.Huu ndiyo ukweli wenyewe hata kama haupendezi.
 
Yule fundi pale Magomeni au Ubungo na meneja wake walikuwa wachapa kazi wa kawaida. Wakaanza ingiliwa na vimemo vya katibu kata, Mjumbe wa shina, Mbunge, DDD, DC, RDD, RC, Katibu Mkuu, Mkurugenzi, Waziri na kila mtu ambaye ana madaraka au nguvu za madaraka na kushurutishwa kufanya kazi zao kwa matakwa ya vi-memo.

Hali halisi ya maisha ya fundi na meneja huyu bado ni za kusitasita. Tawi la OTTU la kampuni yao linashindwa kupata suluhisho la vipato vyao kuongezwa, lakini kila siku wanaona jinsi Shirika linavuyoongiza mapato kwa kuongeza viwango vya matumizi kwa Watumiaji umeme, wanaona na kusoma pesa zinavyotumika kiholela hata kwa menejmenti yao, wizara na Serikali yao, na mikataba ya kijinga ambalo inapunguza gawio la mapato ya kampuni kwa wao kama wafanyakazi.

Sasa mchungaji unataka kusema hao menejimenti wao walikuwa conduits tu za vimemo? Hawa mara nyingi walikuwa wanashirikiana na hao wa ngazi ya chini kujiongezea kipato. Ndivyo ilivyo kote. Si traffic, si kazitamu. ubovu chini unaendekezwa na wale wanaosimamia.

Ninachokisema hapa ni kuwa na sisi technocrats tumechangia kwa kiasi kikubwa haya matatizo. Badala ya kutoa ushauri wakitaalamu tunawaeleza wanachotaka kusikia. Wanapotuingilia tunachelekea na wakati mwingine ni sisi tunaowaendea kuwaomba ushauri hata katika mambo tuliyo na utaalamu. Kwenye hayo mazungumzo ya hiyo mikataba mnayosema mibovu bila shaka wataalamu kutoka tanesco walikuwepo. Kama kweli wao waliiona bomu mbona hatujasikia hata mmoja wao akijiuzuru. Badala yake hao hao ndio tunasikia walioenda kuajiriwa na haya mashirika tunayoyaita uchwara! Hapana, Mkuu, penye menejimenti makini hao wachini hawatafurukuta. Mbona leo hatusikii madereva wamashirika ya bia wakiuza bia kimagham? wanalipwa vizuri na wanawajibishwa. Sisi hata pale tunapowalipa vizuri hatutaki kuwawajibisha. Hilo ndio tatizo letu.
 
Sasa hawa ulitegemea waseme nini?

huh?:confused:

Kuwa wao ndio wenye matatizo? Kama walivyouliza wengine, umewahi kuomba kuunganishiwa umeme na Tanesco?[/font]

Tunachojadili hapa ni lawama zilizotolewa na Wabunge siyo mimi kama nimewahi kuomba kuunganishiwa umeme!!!!! Usibadili mjadala!

Wote tunajua kuwa the buck stops kwenye menejimenti!?[/font]

Geeee!! Kwa hiyo hata mikataba ya akina fisadi Mkapa, Mramba, Karamagi, Msabaha, Lowassa ya IPTL, Richmond, Net group, Songas wa kulaumiwa ni management ya TANESCO!!!!


Hauwezi wewe bosi uliyepewa dhamana ukawatupia lawama mafundi mchundo kuwa wanahujumu shirika bila kuonyesha hatua gani unazowachukulia.
[/font]

Hivi umesoma hizo lawama kwa watendaji wakuu wa TANESCO kama zilivyotolewa na wabunge zinahusiana na nini ? :confused:
Mbona unaongelea vitu ambavyo havikugusiwa kabisa na wabunge hao katika lawama zao!? :confused: Kama huwezi kusoma hiyo article ili uone hawa wabunge uchwara wametoa lawama zipi ili tuzijadili lawama hizo hapa kama zinastahili au la, then I AM OUT OF THIS DISCUSSION.
 
Hebu angalia hapa uone jinsi wabunge hawa walivyokuwa uchwara na kuweka maslahi ya chama chao cha mafisadi mbele badala ya nchi. Kipi kilochotokea katika siku chache na kuwafanya wageuke 180 degrees!? Wananchi tungependa kukifahamu. Kigumu chama cha mafisadi! Kigumu!

]
Aidha, wabunge waliendelea na msimamo huo hata katika semina ya pili kuhusu miswada hiyo, iliyofanyika wiki chache zilizopita jijini Dar es Salaam.

Walikuwa wakiupinga muswada wa umeme kwa maelezo kuwa sheria hiyo itasababisha kifo kwa Tanesco, kwa kukaribisha wawekezaji binafsi wakati shirika hilo liko taabani kifedha.

Wabunge walibainisha kuwa, serikali inapaswa kwanza kuiwezesha Tanesco kuwa imara kifedha kwa sababu yenyewe (serikali) ndiyo imechangia shirika hilo kuporomoka.

Lakini kwa mshangao, tofauti na ilivyokuwa siku za nyuma wakati wa semina kuhusu muswada huo ambapo wabunge wengi walitamka maneno makali kuupinga, na kuapa kutoupitisha kwa madai una lengo la kuiua Tanesco, jana wengi walionekana kuukubali na kuliponda Shirika la Tanesco.
Kabuzi Rwilomba (Busanda-CCM) ndiye aliyekuwa wa kwanza kuelekeza mashambulizi kwa Tanesco na kuusifia muswada huo, akisema kuwa awali aliupinga kwa sababu hakuuelewa vema.

 
Ulitegemea wafanyakazi watanesco waseme nini kama sio kutupa lawama zote kwenye mikataba?

Menejimenti wanahusika katika hiyo mikataba maana walihusika katika kutoa ushauri. Wakati umefika wakuwaambia technocrats wetu kuwa kisingizio cha kuwa niliburuzwa hakitoshi.



KATIKA hali isiyotarajiwa, baadhi ya wabunge wameligeuka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na kudai kuwa matumizi mabovu ya fedha yanayofanywa na watendaji wake, ndiyo yaliyolifikisha shirika hilo hapo lilipo kiasi cha kushindwa kuzalisha umeme wa kutosha, hivyo kutegemea ruzuku ya serikali.

Aidha, wabunge hao walisema watendaji wa Tanesco walipopata nafasi za kuliendesha shirika hilo, walifikiria zaidi kuwapeleka watoto wao shule nje ya nchi na mambo mengine, badala ya kufikiria zaidi maendeleo ya shirika.

Waungwana, hawa wabunge wa CCM wanaonyesha upumbavu wao wa hali ya juu na kutaka kuwatumia lawama watendaji wa TANESCO ambao hawahusiki kabisa na matatizo ya shirika hilo.-ulivyosema mwenyewe[/
QUOTE]

Wewe umeleta topic na mimi naichangia ninavyoiona. Hii habari iliyoletwa katika gazeti haitoi picha kamili. Kwa mfano, hayo mambo mengine ni yapi? Wewe kwa mtizamo wako ni kuwa matatizo yote ya Tanesco yametokana na mikataba mibovu na kwamba watendaji hawahusiki KABISA na matatizo ya shirika hilo! Dhana hii mimi ndiyo naipinga. Ndiyo maana nikakutolea mfano ya ubovu wa utendaji kupinga usemi wako wa kutaka kuwaosha kabisa watendaji kama unavyotaka kufanya wewe.

Ninachowaunga mkono hao wabunge ni wao kudai kuwa pengine kuna matatizo ya kiuendeshaji Tanesco. Hayo ya kupeleka watoto nje siyajui lakini yakiuendeshaji naHISI yapo.

With all due respect,mkuu, kuileta kwako mada hakukufanyi kuwa kiranja wa mada hii. Hii ni open forum na unapoleta jambo lazima ujue kuna wapuuzi wengine watakaokataa kukuunga mkono.
 
Ulitegemea wafanyakazi watanesco waseme nini kama sio kutupa lawama zote kwenye mikataba?

Menejimenti wanahusika katika hiyo mikataba maana walihusika katika kutoa ushauri. Wakati umefika wakuwaambia technocrats wetu kuwa kisingizio cha kuwa niliburuzwa hakitoshi.





[/B][/COLOR]QUOTE]

Wewe umeleta topic na mimi naichangia ninavyoiona. Hii habari iliyoletwa katika gazeti haitoi picha kamili. Kwa mfano, hayo mambo mengine ni yapi? Wewe kwa mtizamo wako ni kuwa matatizo yote ya Tanesco yametokana na mikataba mibovu na kwamba watendaji hawahusiki KABISA na matatizo ya shirika hilo! Dhana hii mimi ndiyo naipinga. Ndiyo maana nikakutolea mfano ya ubovu wa utendaji kupinga usemi wako wa kutaka kuwaosha kabisa watendaji kama unavyotaka kufanya wewe.

Ninachowaunga mkono hao wabunge ni wao kudai kuwa pengine kuna matatizo ya kiuendeshaji Tanesco. Hayo ya kupeleka watoto nje siyajui lakini yakiuendeshaji naHISI yapo.

With all due respect,mkuu, kuileta kwako mada hakukufanyi kuwa kiranja wa mada hii. Hii ni open forum na unapoleta jambo lazima ujue kuna wapuuzi wengine watakaokataa kukuunga mkono.

Watendaji ambao wanaingiliwa na sirikali kila kukicha katika maamuzi yao. Wataalamu wa TANESCO hawakutaka kuingia mkataba na Richmond lakini walilazimishwa kufanya hivyo na mafisadi. Wataalamu wa TANESCO na Watanzania kwa ujumla hawakutaka kuingia mkataba na makaburu, lakini fisadi Mkapa akalazimisha mkataba huo kwa mtutu wa bunduki na kuwaingiza makaburu wale TANESCO huku wakilindwa na FFU. Wataalamu wa TANESCO waliona kasoro kubwa katika mkataba na IPTL kama wangesikilizwa na wizara na kuhusishwa katika maamuzi muhimu ya mkataba huo kabla haujasainiwa basi labda tungeuepuka.

Je unakubaliana na wabunge hao uchwara kwamba matatizo ya TANESCO yanatokana na watendaji wa shirika hilo kusomesha watoto wao nje? Mimi sikubaliani nao. Tanesco kama shirika lolote duniani lilikuwa na matatizo, lakini kasi ya matatizo hayo imeongezeka kwa kasi sana kwa sababu ya mikataba ya kifisadi.

Kwa mwaka TANESCO inalipa shilingi 102.7 bilioni kutokana na mikataba ya kifisadi ya IPTL na Richmond. Hebu imagine kama hela hii ingetumika kuboresha huduma za TANESCO na pia kuongeza idadi ya wateja wao katika kila kona ya Tanzania, shirika hilo lingeongeza mapato yake na pia lisingekuwa katika hali mbaya kifedha kama ilivyo.

Wabunge wa CCM tunawajua siku zote ni uchwara. Kule bungeni hawazungumzi chochote chenye maslahi ya nchi yetu bali chenye maslahi ya chama chao cha kifisadi. Kidogo kidogo Watanzania wanafungua macho na kuijua CCM vizuri. Kama hakitagawanyika basi kitakuwa history very soon. Kigumu cha cha mafisadi, kigumu!
 

Bubu Atakaye Kusema!

Pamoja na admirable efforts zako za kutaka kuwaosha tanesco na maovu yote yanayolikumba shirika hilo hebu soma hapo chini jinsi Tume ya Mwakyemba ilichoandika kuhusu insider trading kutoka kwenye hilo shirika!


Aidha, Kamati Teule ilipata tetesi na baadaye ushahidi kuwa Richmond Development Company LLC ilikuwa na wapambe ndani ya Wizara ya Nishati na Madini na TANESCO waliokuwa wanaipa taarifa (insider dealing). Mfano mdogo tu ni wa Ndugu Mohamed Saleh, aliyekuwa Mkurugenzi wa Usambazaji wa TANESCO na rafiki wa karibu wa wamiliki wa Richmond Development Company LLC. Alishiriki kwenye Kamati ya Wataalam na Kamati ya Serikali ya Majadiliano. Alipostaafu tu TANESCO, akawa mmoja wa wahandisi waandamizi wa DOWANS HOLDINGS S.A iliyochukua majukumu ya Richmond Development Company LLC.

Ripoti nzima iko hapa : http://kenyananalyst.wordpress.com/2008/02/page/2/

Tofauti na unavyotaka tuamini hao watendaji wa Tanesco walihusika katika mzungumzo yote na baadhi yao bila shaka walikaa katika mkao wa kula! Naam, mikataba mibovu imechangia matatizo ya tanesco lakini hauwezi kuwa absolve na wao wenyewe.

Hauwezi kuchukua statement ya wabunge wachache wa chama kimoja kuhukumu chama chote. Mbona kuna wabunge wengine makini tu kama huyo Mke wa Malecela! Mimi hiyo statement ya kwamba matatizo ya shirika hili yamesababishwa na watendaji kuwapeleka watoto wao nje sina siiamini for the simple reason hata wapeleke mpaka wajukuu hii haiwezi kuwa sababu PEKEE ya kulifikisha shirika hapo lilipo! Lakini kama mheshimiwa ana ushahidi kuwa kuna watendaji ambao wanatumia pesa au rasilimali za shirika kusomesha watoto wao nje angewataja na kutoa ushahidi ili hatua za kisheria zichukuliwe. After saying this, bado nasimamia pale pale kwamba menejimenti ( pamoja na bodi) wamechangia kwa kiasi kikubwa tu kulifikisha shirika hapa lilipo. Kama mheshimiwa Mwakyembe alivyohoji, hapo walipoona wanaburuzwa kwa nini hawakufanya the honourable thing na ku'resign'?

Mbona unajichanganya Mkuu? Hao makaburu walioingizwa kwa mtutu wa bunduki unavyodai, ndiyo waliokatia umeme zanzibar kutokana na deni. Ndio waliotishia (sijui kama walifanya) kukatia umeme ikulu kutokana na hilo hilo. ndiyo waliopinga kuendelea kuzalisha umeme Mtera maji yalipokuwa chini ya kiwango kinachoruhusu. Na, naam, ndiyo waliopinga huu mradi wa Richmond! Leo unadai walihusika? Kwani hiyo menejimenti unayoitetea ya Tanesco wakati wa mradi wa Richmond ilikuwa chini ya wakina nani?

Hizo pesa wangepewa kwa jinsi walivyo sasa hivi wala wasingefanyia lolote la maana. Ewura ilipowakatalia kupandisha bei ya umeme, moja ya sababu ilikuwa ni kutokuonyesha juhudi zozote katika kupunguza gharama za uendashaji na kutokua na mipango makini!

Hapana, Mkuu. Sehemu nyingine za dunia shirika halitakiwa kuwa na matatizo. Linatakiwa ku'deliver' na likishindwa menejimenti inatoswa. Steve Jobs pamoja na kuwa ndiye aliyeanzisha Apple lakini alishawahi kutoswa baada ya kuonekana anaipeleka kampuni kusikotakiwa. hii ya kuwatafutia visingizio watendaji wabovu ndio kwa kiasi kikubwa imetufikisha hapa. We can't afford this luxury, we are too poor to do so. Kukosekana umeme sehemu nyingi za nchi yetu kuna impact kubwa sana katika ubora wa maisha wa ndugu zetu. Watu kulazika kuunganisha umeme kiujanjajanja kutokana na umangi meza, uzembe na ndiyo mara nyingi tamaa ya rushwa ya watendaji wa Tanesco kumechangia kuungua nyumba nyingi na watu kupoteza maisha yao. Hili sio suala la mzaha hata kidogo.

Wabunge uchwara wako kutoka kila upande. Cha muhimu ni kumpima kila mbunge kwa vitendo vyake na si kuingia katika huu mtego wa ushabiki.
 
Chadema ina wabunge wachache bungeni lakini wao wamekuwa mstari wa mbele kutetea maslahi ya Tanzania kuliko mbunge yeyote yule wa CCM. Kulikuwa na jitihada kidogo za Anna Kilango (mke wa Malecela) na Seleli, lakini kila mara wakionywa kutohoji chochote kile bungeni basi wananyamaza kimya. Wabunge wa CCM kama kundi wameliangusha bunge letu, wingi wao ndani ya bunge wanautumia ili kulinda maslahi ya CCM badala ya yale ya nchi, kwa hiyo lazima wote tuwaone kama wabunge uchwara. Mimi naamini kabisa kama wangeweka maslahi ya nchi na ya wapiga kura waliowachagua basi hali ya Tanzania isingefikia hapa ilipo leo, wangekuwa wakali kuikemea serikali kwa uchafu chungu nzima ambao unaendelea kila kukicha, lakini si hivyo wao wameweka mbele maslahi yao na ya CCM ufisadi ukawa unaota mizizi kila kona, wao wako kimya tu. Mikataba ya kifisadi inasainiwa na hata waliponyimwa kuiona mikataba ya uchimbaji wa dhahabu wao hawakusema lolote ili kuishinikiza serikali. Matokeo yao ya kuunyamazia ufisadi wote tunayajua.

Sijui kama ulipata bahati ya kuisoma hii article hapa chini ambayo inafanana sana na mengi niliyoyaandika jana katika thread hii. Huyu aliyeandika ripoti hii ni mkaguzi mkuu wa serikali ambaye ana haki ya kuona documents zote za TANESCO kuhusiana na mambo mbali mbali. Angeweza kabisa kuwalaumu watendaji wakuu wa TANESCO kwamba ndio wanaohusika na kuzorota kwa shirika hilo, lakini amesema matatizo mengi yamesababishwa na wizara ambayo kwa maoni yangu ilikuwa inawasikiliza watu kama fisadi Mkapa katika maamuzi yao. Kama huwezi kuamini ripoti aliyoiandika Mkaguzi Mkuu wa serikali na kutaka kuendelea kuwaunga mkono wabunge uchwara wa CCM ambaohawajui wanachoongea, basi utajiju

Hawa Wabunge wa CCM kama wangekuwa si uchwara basi wangeishinikiza serikali kufuta umiliki wa Kiwira Coal Mining ambayo fisadi Mkapa na Yona wameimiliki katika mazingira ya kifisadi na hivyo basi kuutengua mkataba wa KCM na TANESCO ambao viongozi wa TANESCO walishinikizwa wausaini. Mkataba huo ni wa shilingi 340 bilioni, lakini wamekaa kimyaaaa!!!! Kikao cha bunge kitafikia ukingoni na maamuzi yao mengi yatakuwa ni yale yale ya kisanii ili kulinda maslahi ya CCM, na wakati huo mafisadi wakiendelea kupeta uraiani!

Kwa kumalizia mimi siji hapa JF kujadili matatizo ndani ya nchi yetu kwa ushabiki. Kuangamia kwa Tanzania kamwe usifananishe na ushabiki kama wa Yanga na Simba. We're talking about the current events in our beloved country, if not rectified the future of our country will be very bleak. Yanayotokea ndani ya nchi yetu nikiwa kama Mtanzania yananikosesha raha sana kama ambavyo yanavyowakosesha raha Watanzania wengine.


CAG confirms ministry hand in Tanesco plight: Also notes delay in payment of Dowans` own debt to the government

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

THE Controller and Auditor General (CAG) has blamed the Ministry of Energy and Minerals for TANESCO's current doldrums, saying officials from that ministry literally forced the state-run power utility to enter into dubious power generation deals with several private companies.

The latest CAG report released this week confirms that the Tanzania Electric Supply Company's severe financial crisis was occasioned by high-level meddling from the parent ministry.

''In our audit, we discovered that the Ministry of Energy and Minerals has contributed in trapping TANESCO in contracts entered without the company's own assessment and vetting process by its board of directors and management,'' says the report signed by the CAG, Ludovic Utuoh.

The report cites such dubious contracts forced on TANESCO by the parent ministry as including the Independent Power Tanzania Limited (IPTL), Songosongo gas-to-electricity (Songas) and Kiwira Coal and Power Company Limited projects.

Government auditors say they have not been able to find any records showing that the deals with the stated independent power producers were duly approved by relevant tender boards.

The report notes in particular that the $271.8m (approx. 340bn/-) Kiwira contract was 'prematurely' signed while key aspects on the power purchase agreement were not even complete.

Investigations by THISDAY have long established that the formerly state-owned Kiwira coal mine was bought by a company formed by ex-president Benjamin Mkapa, his energy and minerals minister Daniel Yona, and their close family members.

Mkapa and Yona are understood to have used their powerful positions in government to fast-track the sale of the coal mine to their own company, which subsequently signed the controversial power purchase agreement with TANESCO.

''Another example is the Richmond Development Co. Ltd project,'' says the CAG report, echoing widely published findings of the Public Procurement Regulatory Authority (PPRA) and the parliamentary committee on the Richmond deal, all of which highlighted apparent interference by high-level government officials in the tender process.

The CAG report notes that while the tender documents clearly specified that TANESCO would enter into a 12-month contract, Richmond was given a two-year contract despite the company's bid being earlier rejected.

The report also confirms that thanks to such contracts, the cash-strapped TANESCO is now understood to be paying a staggering $7m (approx. 8.4bn/- each month) to independent power producers, equivalent to 30 per cent of the public utility's total revenues.

It furthermore uncovered various operational problems also causing huge losses to the company.

In 2005, TANESCO was losing a third of its generated power through technical and non-technical causes.

''A significant amount of the electricity generated by TANESCO during 2006 was lost through the power distribution network, which was caused by the overloading of power lines and transformers,'' says the CAG report.

A former prime minister and two senior cabinet ministers have been forced to resign after being implicated by a parliamentary probe team in what is now regarded as the Richmond corruption scandal.

On the other hand, the report notes that while the government continues to pay Dowans Holdings SA a staggering 152m/- per day in capacity charges, the United Arab Emirates-based company that inherited the controversial Richmond power generation deal had by September last year still to pay delay penalty dues to the state.

The CAG report shows that by that month, the delay penalty had reached $2.1m (approx. 2.7bn/-).

''This amount was yet to be paid to TANESCO for no apparent reasons,'' said the report, which in general covered audited accounts of parastatals for the year ended June 30, 2007.

It said a special audit on TANESCO was done at the request of the government and the state-run company's own board of directors.

Dowans Holdings SA inherited the highly-dubious, 172.5bn/- government contract to supply emergency turbine-charged power from Richmond Development Company in the closing weeks of 2006.

Still, back in October last year, TANESCO Managing Director Dr Idris Rashidi told THISDAY in a statement that there would be no problem in recovering the delay penalty debt from Dowans Holdings.

''The government will recover what is owed to it by the contractor (Dowans Holdings) by deducting the amounts from their monthly payments invoiced to TANESCO,'' said the TANESCO boss in the statement.

Earlier last year, the government's procurement watchdog - Public Procurement Regulatory Authority (PPRA) � noted in a scathing report on the whole Richmond deal that there was no formal agreement between the parties in the original contract (the government and Richmond Development Company) as to how this penalty would be claimed from Dowans Holdings (the inheritor).
 
Nimeisoma lakini ninachopingana na wewe ni hii kusisitiza kuwa watendaji wa TANESCO hawahusiki na hali ambayo hilo shirika limo sasa hivi. Sipingi kuwa mzigo wa malipo ya hii mikataba ni mkubwa lakini si huo tu kilichoifikisha Tanesco ICU.

Kwa bahati mbaya mimi siangalii mbunge anayetoa hoja kama ni wa CCM au chama cha upinzani. Binafsi ningetegemea zaidi kutoka vyama vya upinzani katika masuala yanayonigusa mimi hususan mazingira na jamii. Ninachosiikia kutoka pande zote ni zile siasa za sound bites au kama alivyosema Obama za Gotcha! Hizi naamini haziaddress mzizi wa matatizo yetu.
 
The CAG report shows that by that month, the delay penalty had reached $2.1m (approx. 2.7bn/-).

’’This amount was yet to be paid to TANESCO for no apparent reasons,’’ said the report, which in general covered audited accounts of parastatals for the year ended June 30, 2007.

It said a special audit on TANESCO was done at the request of the government and the state-run company’s own board of directors.

Dowans Holdings SA inherited the highly-dubious, 172.5bn/- government contract to supply emergency turbine-charged power from Richmond Development Company in the closing weeks of 2006.

Still, back in October last year, TANESCO Managing Director Dr Idris Rashidi told THISDAY in a statement that there would be no problem in recovering the delay penalty debt from Dowans Holdings.

’’The government will recover what is owed to it by the contractor (Dowans Holdings) by deducting the amounts from their monthly payments invoiced to TANESCO,’’ said the TANESCO boss in the statement.


Bubu Atakaye kusema.
Mfano wa hayo ninayoyazungumzia ni huo hapo nilioutoa kwenye posting yako kuhusu ripoti ya CAG. Kwa nini menejimenti haijaeleza sababu za kutokusanya hizi delay penalties wakati wao wenyewe walisema kuwa si tatizo kukusanya? Wao wanalalamikia deni lakini haki yao mbona hawaifuatilii? Huu mimi, unfortunately, naona ni uzembe tu.
 
Wewe sasa naona unabisha for sake ya kubisha tu. Hiyo kampuni ni matapeli si ajabu hata capital walikuwa hawana halafu unategemea waweze kulipa. Kama wizara ingewasikiliza management na Board of Directors basi huo mkataba wa kifisadi wala usingesainiwa. Sasa kama wanashindwa kulipa management ya TANESCO iende ikawadai na bunduki? :confused:

Hilo la kushindwa kulipa hao Dowans, Mkaguzi Mkuu wa Serikali kaliona lakini hakuliweka katika ripoti kama ni uzembe wa management ya TANESCO kwa kuwa kama management hiyo na board yao ya directors wangesikilizwa pale walipotoa tahadhari katika mikataba hiyo isingesainiwa, lakini wewe umeng'ang'ana tu kutaka kuwatupia lawama magament hata ambazo hazistahili, kwa maana nyingine unambishia hata mkaguzi mkuu wa serikali ambaye ameangalia documents mbali mbali za TANESCO katika ukaguzi wake kabla ya kuandika ripoti hiyo.
 
Wabunge Dodoma wautupia madongo muswada wa umeme
Na Muhibu Said, Dodoma

MJADALA kuhusu Muswada wa Sheria ya Umeme wa Mwaka 2007, umechukua sura mpya bungeni, baada ya baadhi ya wabunge kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutilia shaka baadhi ya vipengele vyake na wengine kutoka kambi ya upinzani kuupinga kabisa.

Wabunge ambao wameonyesha kutilia shaka vipengele vya muswada huo uliowasilishwa bungeni wiki chache zilizopita na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja ni pamoja na Mbunge wa Siha (CCM), Aggrey Mwanry, hasa kipengele kinachowakaribisha wawekezaji kuwekeza katika umeme, huku Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP), John Cheyo, akipinga kabisa suala hilo.

Akichangia mjadala huo, Cheyo alisema hakubaliani na muswada huo kwa kuwa kabla ya kufikishwa bungeni, haukufanyiwa utafiti wa kutosha ili kubaini mapungufu yake ambapo iwapo utapitishwa na kutungwa sheria, taifa linaweza kujikuta likiingia upya katika hasara.

Kutokana na hali hiyo, alisema kupitishwa kwa muswada huo, kutawakosesha wananchi wa vijijini kupata huduma ya nishati hiyo, kinyume na inavyoaminiwa na baadhi ya watu.

Cheyo alisema hakubaliani kabisa kama muswada huo iwapo utasaidia umeme kufika vijijini ambako wananchi wengi hawawezi kumudu gharama kubwa za kujiunganishia nishati hiyo.

Alisema muswada huo utalinyima Shirika la Umeme nchini (Tanesco) ukiritimba ilionao wa kutumia raslimali zilizopo nchini kufikisha nishati hiyo vijijini kwa gharama nafuu.

Alisema kosa la kuwafungulia wawekezaji binafsi kuwekeza katika umeme, ndilo lililofanyika huko nyuma kwenye sekta ya madini ambako lilisababisha wananchi kutonufaika na raslimali hiyo muhimu kiuchumi wa nchi, badala yake likabaki kuwanufaisha wawekezaji pekee.

Alisema kama muswada huo umetungwa kwa shinikizo kutoka kwa wafadhili, ni heri kuachana kabisa na mapesa yao (wafadhili), badala yake yaangaliwe maslahi ya

taifa.

Pia alionyesha wasiwasi wake kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Madini nchini (Ewura) ambayo haina uwezo kifedha kama itaweza kuwabana wawekezaji.

Naye Mwanri alisema pamoja na kuunga mkono muswada huo, angependa Tanesco ndio isimamie huduma ya usambazaji umeme vijijini na kwamba wapewe watu wenye moyo wa uzalendo kuendesha shirika hilo.

�Mheshimiwa Ngeleja, waambie Tanesco kazi ya kupeleka umeme vijijini ni yao.Private Sector (sekta binafsi) watakuyumbisha,� alisema Mwanry.
 
Menejimenti ya TANESCO haiwezi kukwepa lawama, mikataba mibovu waliiona na kila dhambi waliion ikiendelea, kwa kukaa kimya ina maana walishirikiana na ufisadi kwa njia moja au nyingine. Kama wangekua wasafi wangeachia ngazi. Wabunge nao walikua wapi siku zote kusema? mpaka maji yamwagike ndo wahangaike kuyazoa? IPTL ni ya lini? wangekemea sawasawa tungepata Richmond kweli?
 
Menejimenti ya TANESCO haiwezi kukwepa lawama, mikataba mibovu waliiona na kila dhambi waliion ikiendelea, kwa kukaa kimya ina maana walishirikiana na ufisadi kwa njia moja au nyingine. Kama wangekua wasafi wangeachia ngazi. Wabunge nao walikua wapi siku zote kusema? mpaka maji yamwagike ndo wahangaike kuyazoa? IPTL ni ya lini? wangekemea sawasawa tungepata Richmond kweli?

Kweli TANESCO wanalo. Na katika hili nadhani Mkapa na Netgroup yake alilikoroga. Bwana Mkapa soon utalinywa kwa kuzembea wakati wa utawala wako.
 
Wewe sasa naona unabisha for sake ya kubisha tu. Hiyo kampuni ni matapeli si ajabu hata capital walikuwa hawana halafu unategemea waweze kulipa. Kama wizara ingewasikiliza management na Board of Directors basi huo mkataba wa kifisadi wala usingesainiwa. Sasa kama wanashindwa kulipa management ya TANESCO iende ikawadai na bunduki? :confused:

Hilo la kushindwa kulipa hao Dowans, Mkaguzi Mkuu wa Serikali kaliona lakini hakuliweka katika ripoti kama ni uzembe wa management ya TANESCO kwa kuwa kama management hiyo na board yao ya directors wangesikilizwa pale walipotoa tahadhari katika mikataba hiyo isingesainiwa, lakini wewe umeng'ang'ana tu kutaka kuwatupia lawama magament hata ambazo hazistahili, kwa maana nyingine unambishia hata mkaguzi mkuu wa serikali ambaye Smeangalia documents mbali mbali za TANESCO katika ukaguzi wake kabla ya kuandika ripoti hiyo.


Mkuu, naona unaamini mno magazeti. Naona kweli uko confused kama ulivyosema mwenyewe maana naona hata mimi unataka kunipeleka huko. Kampuni ipi hiyo ya kitapeli unayozungumzia? Richmond, Net Group au Dowans?

Tanesco ni shirika na lina njia chungu mzima za kudai haki yao. Wewe leo chelewa kulipa bill utaona makali yao. Si lazima washike bunduki. Kuna arbitration, kuna mahakama n.k. Zote hizi wameshindwa kuzitumia ? kwa hiyo basi kwa sababu wamekataa kulipa , menejimenti na bodi yao wakunje mikono na kumwomba mwenyezi Mungu awasaidie? Are you serious?

CAG alichosema ni kuwa hakuna sababu zilizotolewa kueleza kwa nini hizo Delay penalties hazijakusanywa. Hizo hizo penalties ambazo mtendaji mkuu aliishasema kuwa si kazi kubwa kuzikusanya. Kama Tanesco ingekuwa imefanya jitihada na kuzuiliwa na wasioitakia mema, wangesema. Hawakusema na ndio maana CAG ameshtuka. Haya ameyaandika CAG mwenyewe. Mkuu acha kung'ang'ania vichwa vya habari vinavyoandikwa na waandishi wetu uchwara. Penye ripoti soma na ujaribu kumuelewa aliyeandika na sio kungoja kutafuniwa. Pengine ni neno delay penalties hukuliewa. Haya ni yale malipo ambayo sisi mafundi mchundo tunaita liquidated damages. Mkandarasi akishindwa kukamilisha mradi katika muda anaotakiwa kukamilsha anatozwa LD. Kwa vile Richmond na mrithi wake Dowans walishindwa kukamilisha mradi katika muda uliokubalika basi walipaswa kulipa Tanesco LD kwa kila siku waliyochelewa. Haya ni malipo ambayo shirika lililo ICU kama Tanesco wangelivalia njuga kikamilifu. Hawakufanya hivyo. Na hii ndiyo CAG anayozungumzia. Sasa mwenzangu ulitaka mpaka CAG awaite Tanesco kuwa walikuwa wazembe ndiyo umuelewe?

Nimekuwekea nakala ya ripoti ya Mwakyembe anapozungumzia suala la inside trading ambao unaelekea ulifanywa na mtendaji mmoja wa Tanesco, bado nayo unakataa kuiona. Leo wanazungumzia malipo yaliyotoka Jersey kwenda kwa boss mmoja wa Tanesco, bado unadai Tanesco walikuwa wasafi katika hili jambo! Ama kweli mpenda chongo huona kengeza!

Pamoja na kwamba sijapingana nae kwenye hili bali sitasita kumpinga pale nitakapoona amekosea. Yeye ni binadamu kama wewe na mimi.

Bado nashikilia palepale kuwa kuna haja ya kuliangalia vizuri hili shirika letu ili tusije tukajuta baadae.
 
Kuliangalia shirika wakati mikataba ya kifisadi ikiendelea kusainiwa na mafisadi! Nazungumzia management ya TANESCO na Board of directors ambao wanafanya maamuzi kama timu na walikataa kusaini mikataba yote hiyo ya kifisadi na kulazimishwa kufanya hivyo na wizara, lakini bado hutaki kuelewa hili. Duhhhh! :confused:

Maamuzi ya kuzorotesha TANESCO wafanye wengine kama alivyosema CAG, lawama tuwabebeshe wengine!!!!
 
Kuliangalia shirika wakati mikataba ya kifisadi ikiendelea kusainiwa na mafisadi! Nazungumzia management ya TANESCO na Board of directors ambao wanafanya maamuzi kama timu na walikataa kusaini mikataba yote hiyo ya kifisadi na kulazimishwa kufanya hivyo na wizara, lakini bado hutaki kuelewa hili. Duhhhh! :confused:

Maamuzi ya kuzorotesha TANESCO wafanye wengine kama alivyosema CAG, lawama tuwabebeshe wengine!!!!

Kweli kabisa Bubu,

kazi yao kuhamisha lawama tu hao Tanesco wakati wanajulikana kwa ufisadi na vikao vya bodi vyenye kutumia mamilioni ya pesa.
 
Mswada wa umeme ni njia za Mafisadi kuwekeza fedha zao katika Makampuni ya Umeme., na si kazi Hizo hizo Richmond na Agreko, na IPTL baada ya kupata mtaji kutoka Serekali (kwa wadanganyika) ndio hizo hizo zitakapotoka upya.
Na Hela walizo weka Jersey etc ndio zitazowekezwa kwenye umeme.
Hivyo hatuna budi kujua hao Share holders wa hayo makampuni yatakayo kuja kuwekeza, isije ikawa kama Richmond mwenyewe hajulikani.
 
Kuliangalia shirika wakati mikataba ya kifisadi ikiendelea kusainiwa na mafisadi! Nazungumzia management ya TANESCO na Board of directors ambao wanafanya maamuzi kama timu na walikataa kusaini mikataba yote hiyo ya kifisadi na kulazimishwa kufanya hivyo na wizara, lakini bado hutaki kuelewa hili. Duhhhh! :confused:

Maamuzi ya kuzorotesha TANESCO wafanye wengine kama alivyosema CAG, lawama tuwabebeshe wengine!!!!

Nakiri mimi ni mzito wa kuelewa. Nimesoma ripoti ya Mwakyembe na maelezo ya CAG na sijaona mahali ambapo wame'exonerate' Tanesco kutokana na mikataba hiyo. Mwakyembe alifikia hatua ya kushangaa kwa nini bodi haiku'resign' kama waliona mikataba ina matatizo! Mwakyembe amezungumzia kuwepo kwa inside trading kwa upande wa Tanesco.CAG ameshangaa kwa nini Tanesco hawajachangamkia malipo ya Delay penalties! Yote haya si kuisifia Tanesco bali ni kuwakosoa. Kisingizio na kilio cha kila siku cha technocrats kuwa walilazimishwa na wanasiasa does not wash anymore. Wewe kama mtaalamu hauwezi kuepuka lawama kama ulicapitulate mara mkubwa anapokukazia macho. Tanesco ilikuwa ICU hata kabla ya hii mikataba. Dawasa ilikuwa ICU hata kabla ya City Waters. ATC ilikuwa ICU hata kabla ya makaburu. Leo tumesahau yote haya na kutupia lawama zote makaburu, mafisadi na wengine wote isipokuwa wale waliopewa dhamana ya kuendesha hivyo vyombo! Nimeishiwa nguvu.
 
Back
Top Bottom