Wabunge wa CHADEMA mtawambia nini wapiga kura wenu 2015?

Nimekuwa nikifuatilia harakati za wabunge wa CHADEMA kwa muda sasa.
Walio wengi wamejikita kufanya kazi za 'kichama' zaidi kuliko kutimiza wajibu wao kama wawakilishi wa wananchi.
Hata michango yao bungeni hulenga zaidi kutafuta umaarufu wa kisiasa wa chama badala ya kutatua kero za nanchi wao majimboni kwao.
Wengi wao wakiulizwa hapa, hutoa majibu rahisi kuwa hawana dola hivyo hawewezi kutekeleza ahadi zozote za maendeleo majimboni kwa kuwa hawakusanyi kodi!
Swali ni je:
  1. Mtawambia hivyo wapiga kura wenu 2015? Kuwa hatukufanya lolote kwa kuwa hatukuwa na dola?
  2. Au mtaonesha kadi za CCM zilizorudishwa kwenu kama mafanikio yako ukiwa mbunge?

Wabunge wa CDM, Tafakari na muchukue hatua!

Sijui ndo wewe mwenyewe au mmeibiana hii hoja kule Facebook.****
 
Mlete uzi hao magamba kwa miaka 51 wameleta manufaa gani zaidi ya kusinzia bugeni huku pesa zinaliwa.tena wewe binafisi uwashukuru sana cdm kwa kuwaamsheni toka usingizi wa pono
 
Kukijenga chama kunaendana sambamba na mpango mkakati wa kuwakomboa wananchi maskini wa nchi hii.
Kama nia yao ingelikuwa kukijenga chama pekee, CDM leo wangelikuwa na miradi ya maendeleo kama Viwanja vya michezo, maduka, mahoteli, pamoja na business firms nyingi tu.
CDM wame determine kuwakomboa wananchi wa Tanzania.


Labda kama sijakuelewa.
 
Back
Top Bottom