Wabunge wa CCM waliopanga kumuona Lema gerezani waonywa, waitwa wasaliti

Rais haupendi upinzani toka moyoni.,.

Na hii ni hatari kwa kiongozi wa nchi kuwa na chuki na baadhi ya wananchi wake.
Apunguze kufanya/kuongea mambo kwa hisia. Ndio maana viongozi wa ngazi yake huwa na washauri ili wamsaidie kuepuka fedheha kama hii.
 
masikin i Tanzania, mwenyekiti wa CCM anatangaza chuki za wazi kabisa alafu kutwa kuwaomba wananchi wamuombee,

wabunge wa CCM wanapelekeshwa kama watoto wa shule ya msingi.


Namuonea huruma mrembo Halima Bulembo ndiyo anaandamwa na mwenyekiti wake eti yeye anavujisha siri kwa wapinzani
 
Jamani naomba msaada wa mawazo,

mke wangu ni CCM damu nani SIMBA damu, ni Man U damu.

mimi ni UKAWA damu nani YANGA damu, pia ni Arsenal damu,

kwa rais anavyotaka kutugawa nifanyaje?

Kwani nn hujaelewa hapo? Ngoja nikusaidie:

1. Mkeo akiumwa hupaswi kumpeleka wala kwenda kumuona hospitali
2. Hupaswi kumpelekea uji wala kwenda kumuona akiswekwa Central au kwingine kokote
3. Mengine kama hayo ongeza mwenyewe.
 
Nimeshangaa sana kusikia kuna wabunge wasaliti,,nikajiuliza mbona kafukuzwa mmoja tuu,hao wasaliti wabunge aliwasahau?
 
Amesema anasikia kuna wabunge wanataka kupiga kura ya kutokuwa na Imani na Waziri Mkuu hawatofanikiwa na akawaambia tena kwa kiburi kuwa yeye ndio alietoa amri bunge lisiwe live kwa kuwa hamna wanachofanya zaidi ya kupiga soga tu akaenda mbali zaidi akasema jaribio lolote la kutaka kumwajibisha PM litasababisha hatorudisha jina la wabunge watakotaka kugombea kipindi kijacho pale litakapopelekwa kwenye Kikao husika kwa ajili ya kupitisha nadhani hapa alimanisha kwa kuwa yeye ni mwenyekiti wa Ccm na Majina yote baada ya kura za maoni yeye ndio ataongoza kikao cha kuyapitisha MBAYA zaidi mwishoni akasema wakijaribu atalivunja Bunge!!! Nimejiuliza maswali manne, mosi Ndugai na Mwenzake walikuwepo kwenye hicho kikao? Pili siku hizi Bunge ni sehemu ya Ikulu? Tatu je wabunge waliochaguliwa na wananchi kuna mtu anawapangia nini cha kufanya au kutokufannya? Nne je ni kweli tumekuwa na wabunge wa ovyo kiasi hichi? Hapa namalizia kwa yafuatayo Endapo wabunge wa CCM hawatoungana kwa hili naona dalili ya nchi kuingia gizani!! Na baada ya kufanikiwa hapo wabunge wote wa ccm wategemee kuendelea kudhalilishwa Mno!!! Kama haoni faida yenu atawahitaji kwa lipi? Hiyo ni kumlinda tu Bashite katoa maneno hayo je akiwa anajilinda mwenyewe dhidi yenu atayatoa yapi? WABUNGE WA CCM hiyo ni wake up call mkilala tu mmeisha!!! MWAFAA AAAAAAA.
 
Wewe ndo unatakiwa usitumike kijinga...hao wanamenyana wenyew baba yao mmoja sasa sis tusio wafuasi wa siasa hatuoni shida...na kaa ukijua wajinga sio viongoz wajinga ni mim na wew tunaotumiwa vibaya...over
Una cheti?
 
Tishio la Nchi yetu kwa sasa ni Kiongozi mkuu wa CCM wale wanaodhani ni baa la Njaa nawaambia wamekosea sana!!
 
Wewe huwezi amini mh raisi akiwa kwenye hafla ya nmb aliwaasa wa tz wasiweke pesa benki nyingine zote ila nmb maana serikali ina hisa asilimia 31 so hela zoote tuweke nmb na benki nyingine tuweke 0.001% ya hela zetu ili hela zikienda nmb serikali itapata gawio la hisa na hisa zitasaidia wananchi. Je is that a presidential speech? Je anaona raha bank nyingine zikifa?, na je nn madhara kwa bank nyingine kufa , kwa taifa na kwa serikali? Je huyu ni raisi wa nmb tu? Bank nyongine wanajisikiaje wanaposikia mkuu wa nchi anelekeza taasisi zoooote za serikali zisiweke pesa au kufanya biashara na bank za biashara wanajisikiaje? ukizingatia mchango wao mkubwa sana wa kimaendeleo ktk uchumu wa nchi yetu? HUYO NDO RAISI. LIKE FATHER LIKE SON. Asanteni
Wakati huo huo yeye anasisitiza watanzania bila kujali imani zetu tumuombee.....Nafikiri kuanzia sasa kila mtu ajiombee mwenyewe tu....mtu unapoteza mda kumwombea yeye alafu ndo kwanza yeye anatugawaa sasa hivi akitaka kuombewa amtafute Gwajima na Pengo wamuobee
 
Rais Magufuli amewatisha wabunge CCM kwa kuwaonya vikali, amewashutumu wabunge hao kwa kutoa siri za CCM kwa upinzani na hata kuwagawia wabunge wa upinzani muda wa maongezi bungeni.

Magufuli amewaonya wabunge wa CCM waliokuwa wamepanga kumtembelea mbunge mwenzao Godbless Lema gerezani na ameita kitendo hicho kama usaliti mkubwa kwa CCM.

Na mwisho JPM amewapa somo, kwamba anajua kuna njama za kumwondoa Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa kwa kutokuwa na imani naye,wakishiriki kwenye mipango hiyo atalirejesha jina la Majaliwa kwa mara ya pili na bunge likilikataa atalivunja na nchi irudi kwenye uchaguzi wa nafasi zote.

CHANZO: Gazeti la Mwananchi.

======================

Hii ni dalili ya Taifa linalojengwa katikati ya chuki ma uhasama.Taifa la visasi na kukomoana.Unaposikia Rais anawalaumu wabunge wa chama chake kumtembelea mbunge mwenzao wa chama kingine gerezani,unapata picha ya nini na nani anaweza kuwa nyuma ya mbunge husika kuwa gerezani.

Hii inakatisha tamaa,inaondoa moyo wa uaminifu hata kwa sie wachache ambao tulikuwa upande wa Rais ktk baadhi ya mambo anayoyasimamia.Kwa kauli hizi,Rais na mkuu wetu anatukatisha tamaa sana sana.

Unaposikia kauli za chuki kiasi hiki,unajiuliza pale mtu anapokuwa anataka aombewe,aombewe kwa minajili ya kuzidisha chuki na mtangamano au?

Rais mara nyingi husema yeye ni wa wote;maendeleo hayana chama,tudumishe amani na upendo maana Tanzania ni moja,lakini Tanzania itakuwa moja kwa mtindo huu wa kupandikiziana chuki na kutishana??

Tuzidi kuliombea Taifa.Na wengine tunazidi kukata tamaa.Mungu saidia.
Hii hatariii
 
Rais wetu ni msomi lakini mambo mengine anayozungumza hasa kwa nafasi yake yanaleta shida sana badala ya kukusanya anatawanya
Kabisa. Inatakiwa alete umoja, sio utengano. Siasa sio uadui, ila iwe ni mgongano wa mawazo
 
Hivi kweli ndo tumefika huku?

Naomba niwe wa mwisho kuamini maana hii inaleta mpasuko.

Kama kiongozi analeta mpasuko sisi raia wa kawaida itakuaje? Mungu tusaidie
 
masikin i Tanzania, mwenyekiti wa CCM anatangaza chuki za wazi kabisa alafu kutwa kuwaomba wananchi wamuombee,

wabunge wa CCM wanapelekeshwa kama watoto wa shule ya msingi.


Namuonea huruma mrembo Halima Bulembo ndiyo anaandamwa na mwenyekiti wake eti yeye anavujisha siri kwa wapinzani
 
Back
Top Bottom