Wabunge Vijana Wa CCM: Tafadhalini Sana!

Wakuu wote JF, heshima mbele sana!

- Ninashangazwa sana na Wabunge wengi vijana wa CCM kuuogopa huu mtandao wa JF, I mean tena wengi wao wasomi wa ajabu, nimeongea nao sana kwa vipindi mbali mbali wengi wanaonyesha kuogopa sana hapa, hilo limenishitua sana. Wabunge Vijana wasomi, nilifikiri huu ndio uwanja pekee wa kuwasafisha na kuweka misimamo yao wazi of what they stand for!

- Majuzi nilikuwa na Mheshimiwa Hamis Kingwalallah proud of him, we talked a lot about Thread yake ya kwanini hakusaini karatasi ya Zitto, I mean I am again proud of him. He was very openminded and Zitto himself came we talked about it, unaona ni very positive regardless ya kejeli na matusi za hapa, lakini muhimu ni KUJA HAPA NA kuweka msimamo kama a politician tena kijana msomi, na ukaeleweka vizuri kuliko kuogopa matusi na kejeli. Leo tena nimeongea na Wabunge wengi sana pale Diamond Jubilee on JF, please njooni hapa!

- JAMANI WABUNGE VIJANA WA CCM MPO KWENYE SIASA SAWA NA BIASHARA YA UTUMBO SASA MSIOGOPE HARUFU, NJOONI HAPA TUMKOME NYANI, HUU SIO UWANJA WA CHADEMA NI UWANJA HURU WA KILA MWANANCHI KUSEMA MAONI YAKE NA NYINYI NI VIONGOZI WA HAWA HAWA WANANCHI, NJOONI HAPA KAMA MLIVYO MJIBU HOJA NA MUWEKE HOJA, MCHAMBULIWE TUONE KAMA KWELI MNA HOJA!


- MUNGU AIBARIKI TANZANIA!


William.

tunadanyana CCM HAINA WABUNGE VIJANA!maanisha nini?Sio umri tu bali fikra zao zimepitwa wakati then ni nzee.
 
Hapa ni mahali pa kupoteza wakati si pa wanasiasa na viongozi kukaa na kuwa mateja ya JF.

Wewe William ni Potato coach hata mwili wako unaonesha ni mtu uunaeweza kukaa kwenye lap top yako kutwa nzima.

Hoja na shughuli wazijibu hukohuko, hapa wawaachie magwanda na sisi tunatosha kuwa kong'oli.

Ndugu yangu bila shaka wewe ndiye unayepoteza muda.

Hapa watu wapo makini katika kujadili mada muhimu kwa mustakabali wa Taifa letu. Kukosoa maovu katika Jamii.

Sasa kama wewe unaona kuwa unapoteza muda nenda kijiweni ukanywe kahawa. na pia kama umekosa cha kuchangia katika Thread hii, ni heri unyamaze tu. Hautaadhibiwa kwa kunyamaza.

Nampongeza muanzisha wa hii Thread kwani ametoa yanayomkera na pia amefuailia kabla ya kutoa hii Thread. HONGERA SANA WILLIAM.


NILIENDA KUTEMBELEA WAGONJWA MUHIMBILI WODI YA ICU, NIKAIKUTA CCM INAPUMUA KWA MIPIRA YA OKSIJENI.
HALI YAKE NI MBAYA SANA HIVYO SIDHANI KAMA ITAFIKA MWAKA 2015!!!!!



MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
Wapo wengi lakini hawatumii majina yao. We hukumbuki Pius Msekwa aliishitumu JF hadharani? We unadhani aliwezaje kusoma thread nyingine bila kujiunga? Je ushakutana na jina la Msekwa humu ndani? Mi mwenyewe sijawai kuona jina la Malechela jukwaa la kikubwa, what if una id nyingine makskusi kwa jukwaa hilo? Au inawezekana hulifahamu kabisa mkuu?
 
@W.J. Malicela

Wanaweza kuanzia jukwaa la "Great thinkers" kule angalau kuna utaratibu mzuri wa mjadala.Lakini pia suala si tu kuingia JF lakini wataweza kujenga hoja.........wana uwezo huo kweli?......wajiandae kwa sababu watakuwa wanapopolewa pia na maadui zao wa kweli kisiasa na ki-maslahi.

Hata wewe pamoja na kuwa member wa muda mrefu hapa JF lakini hoja zako wakati mwingine zinakuwa shallow sana.....rahisi kuzivunja.Lakini una bahati hujaishi Tz muda mrefu kwa hiyo mengine ya uraiani hayaji hapa.....Kwa hao je? Siwatishi lakini wajiandae bila munkari..............
 
Hahahaaaaaa ww ni kiboko!
You know how to Critique ideas by describing what could be done to make said "ideas" more useful.But in other hand you should learn to acknowledge what was done right.
Le Baharia did well although he should not attempt to profile those guys as you mentioned.Na labda alitakiwa kuchukua ushauri wako na kusema atahamasisha wote ila kwa sasa imekuwa rahisi kufanya initiate hiyo kwa vijana kwa kuwa ana network nao zaidi;Le baharia jifunze kuchukuwa ushauri positively

Classic.

It's not that I do not appreciate the half measure, after all half a bread is better than none. Truth be told William's serendipity - the lack of a comprehensive outlook renders this nothing but- can be thanked for stirring this conversation. I am merely attempting a comprehensive look at the issue.

What is the real issue? There is a disconnect between leaders and the TZ netizen populace.Young MPs have no monopoly on this practice, in fact as I have pointed above, they are the ones who provide a much needed relief (thanks to Zitto, Mnyika and Kigwangwallah to mention the few I have seen here personally). I have yet to see an "old" MP in here this year.

So, you will see that, out of the several hundreds, we hardly have 2% coming here sporadically. The issue is across the board. If one is looking at the issue comprehensively, and has no hidden agenda, there is no sense to concentrate on the youthful MPs.

For William, someone with an MP in his immediate family, this business of concentrating on youngish MPs smacks of deliberately excusing his very own step mother from this responsibility all MPs share.

William, I will take you more seriously on this if you start the call by asking your MP stepmother, Anne Kilango Malecela, to come here openly and expose her views and plans, and answer questions.

Charity begins at home. Until you do this, you will have no moral authority to point a finger at any other MP.

This is not to be confused with an attempt to excuse MPs for not being accessible online. What I am stressing here is that all MPs should be given the same scrutiny without cherry picking groups according to some hidden agenda.
 
Kiranga, binafsi sijaona age discrimination yeyote kwenye thread hii, ni sawa na kualika kikundi chochote au wabunge wanawake huwezi kusema ni hiyo ni gender discrimination. Tukitumia notion yako hiyo kuna siku tutaogopa kujumuika na vijana wenzetu kwa hofu ya kuambiwa wabaguzi.

Mtu ukitaka kuona discrimination kwenye jambo lolote lile basi utaiona tu. Binafsi sijaona discrimination yoyote hapa.

It's just that William is challenging the younger generation MPs (who most likely are more information superhighway savvy than their much older counterparts) not to shy away from social forums like this one and there is absolutely nothing wrong or discriminatory about it.
 
Wana-JF, inapoletwa thread hapa inabidi tujadili hiyo thread. Tukianza kupinga threads kwa kuzilinganisha na mawazo yaliyo nje na mtoa hoja hatutafika popote. Kila thread itakuwa na mapungufu tu. William yuko very right kuweka hoja hiyo. Mwingine naye siku nyingine atakuja na hiyo ya opposite side. Uhasama/chuki binafsi hazitakiwi humu ndani. Humu ni kuwekana sawa. Kukosoana ndo kwa kina. William alikuwa na nia njema ya kuwa-motivate hao walengwa wake waje tujue mawazo yao kwa mustakabali wa nchi. kama wakibaki huko mafichoni hatuwezi kuwajua vizuri. Mbunge Kingwallalah kabla hajaja humu nani alijua akili yake? Baada ya kuja hapa akajifunua ndo tukaona kumbe hamna kitu mle. Naamini hata yeye alipata somo kubwa kujua nini watanzania wanataka. Nafikiri atakuwa amejiona mdogo baada ya hapa, na pengine kujua makosa yake kwa nchi yetu.

Huyu hapa hajawahi kusikia kitu kinaitwa "thinking outside the box". Akishaambiwa mjadala ni kuhusu wabunge vijana hawezi hata kuuliza kwa nini mjadala uwe wa wabunge vijana tu wakati wajibu wa wabunge kuwa karibu na wananchi ni wa wabunge wote?

Hata kama mtu anataka kuleta unafiki wa kuchezea akili watu kwa agenda zake za siri, kiasi cha kutaka kumuacha mtu wa nyumbani kwao kwenye scrutiny hii, anaweza kumchezea huyu vilivyo.

Kwa sababu huyu haulizi maswali, anaichukua hoja kama ilivyoletwa. Mtiifu sana.

Utiifu sana ndio unaotulostisha.

Punguza ukondoo.

After all JF we are supposed to be able to dare and speak openly.

So why curb the conversation instead of enhancing it?
 
The simple logic is vijana sasa hivi ni mtaji. Kila anayehitaji kupigiwa kura anajua kwamba wapigakura wengi sasa ni vijana. Lazima wajionyeshe kwamba wanawajali vijana, and that is what every fisadi is doing.

Mazee Gagnija anaanza kunusa habari nyingine ambayo inaweza kuwa tofauti kabisa na habari hii inavyoonekana kijuu juu.

Kwamba watu wanaweza kuwa wanajipigia debe kisiasa hapa kwa kuangalia demographics, huku wakijivika joho la kutaka transparency kutoka kwa wabunge vijana.

Wakitegemea chorus ya kirahisi rahis ya "Ndiyo Mzee" kutoka JF kwa misukule ambayo ikisikia "vijana" tu inakuwa kama imepata Pavlovian stimuli, inafanya vitu bila kufikiri zaidi.

Kama lengo ni kutaka transparency kutoka kwa wabunge kwa nini mtu achague vijana tu? Kama mtu anataka wabunge wapatikane kirahisi online kwa nini achague vijana tu?

Anataka mjadala wa kisiasa au anataka kupanga nao kwenda club?
 
Mwingine naye siku nyingine atakuja na hiyo ya opposite side.

Pay attention - wengine humu ni mahodari tu wa kusubiri mada zianzishwe na wengine halafu wao waanze kuponda!

Uhasama/chuki binafsi hazitakiwi humu ndani.

When people bring up others' step mothers and ex-wives I can't help but think they feel or have some sort of an animus against the person whom they are talking about.

It's sad but such is life.
 
Hoja ni wabunge vijana kuja humu ndani. Tusimshambulie william, hoja yake imekaa vizuri kweli. mambo ya mama wa kambo na mengine yasiyoendana na hoja tuachane nayo. Chuki binafsi/wivu tuachane navyo. Tumeacha hoja tunajadili kitu kingine. Ni kwa nini wabunge vijana wanakataa kuja hapa, wengi wameishatoa sababu kuwa wanaogopa kushughulikiwa na chama. Lakini hapa ni mahali pa kupata maarifa mengi. Inawezekana mtu akashindwa kufanya maamuzi ktk eneo lake akaja hapa akaanzisha thread na akapata mawazo safi kabisa. Kama kweli mtu unataka kuwatumikia na kuwaletea maendeleo watanzania, hapa ndo mahali pa kuchuma maarifa. Wanaoogopa hapa wataishia kuwa na ufinyu wa mawazo. Watu wote wenye nafasi za kutumikia taifa, walete hoja hapa zijadiliwe. Yote wanayodhani ni vikwazo ktk utumishi wao waviweke hapa. Potelea mbali wakija na ID bandia, tunachotaka sio sura ya mtu au jina lake, ni muhimu ni yeye kutumia jina lililofichwa kupata mawazo yatakayosaidia maendeleo ya nchi yetu. Tunachotaka ni maendeleo tu. Kuficha ID zao ni muhimu kwa kwa ajili ya usalama wao na familia zao, maana serikali isiyotenda haki lazima itawaondoa radicals wake wote.

Kwa nini hoja iwe wabunge vijana wakati tuna wabunge zaidi ya wabunge vijana?

Let's face it. Hoja ni wabunge kutokuja JF. William anaona akisema hivyo atakuwa kampaka mpaka Mama yake wa kambo.

Ndiyo maana kakimbilia kwa wabunge vijana.

Anaweza kutuambia kwa nini mama yake wa kambo haji hapa kwa jina lake? Akishindwa kutuambia hili atakuwa hana "moral authority" ya kutaka mbunge mwingine yoyote aje hapa JF.
 
Kwa hiyo Kiranga is right eeh? I think ungewaita wote waje tu kama unavyoshauri si kama ulivyobagua!! Ninachojua wabunge wengi sana wa CCM wanaingia huku kama guests!! Maan ka "nizamu" ka chama kamewalemaza akili!!!:wacko:

Hahaa,

Polepole anaona makosa yake na kubadili kauli kinyemela kwa sababu ego yake ni size ya @NYC kunradhi kwake ni muhali.

Kaondoa "vijana" na sasa anawaita wabunge. Good.

William, kwa sababu umebadili kauli na sasa unawaita wabunge, na kwa sababu una mbunge katika familia yenu, ushamuita na yeye? Anasemaje kuhusu hili?

Mi ningependa kuona wabunge wote wanakuja hapa. Au angalau wengi, wa kila rika na jinsia.
 
Mimi naona Malecela hajakosea kuleta hii mada hapa, maana kasema alipata muda wa kukaa na wabunge vijana na kuwaulizia kuhusu ushiriki wao katika JF, maybe akijapata muda wa kukaa na wabunge wazee na akaulizia kuhusu ushiriki wao ataanzisha tena thread nyingine.
Ukweli ni kwamba wabunge wanapita humu kupata chochote bila kutoa/kuchangia mada yoyote, they are remaining anonymous...!

Bunge lina wazee wengi kuliko vijana, huyu mtu ana familia yenye mbunge ambaye si kijana, kwa nini yeye apate muda wa kuongea na wabunge vijana tu? Ina maana hata mbunge aliye katika familia yake hakupata muda wa kuongea naye?

Hapo ndipo changa la macho linapoonekana.
 
Hakuna age discrimination hapa mbona mnatutoa kwenye hoja ya msingi kwa nini wabunge vijana wa ccm hawaji kupambana na changamoto za vijana wenzao kisiasa jf..???

To teh contrary.

Mie siwatoi kwenye hoja ya msingi. Mie ninawapeleka kwenye hoja ya msingi.

Hoja ya msingi ni wabunge hawapatikani online kushauriana na wananchi.

Hizi habari za vijana/wazee ni distractions zenye ajenda ya siri tu.
 
Salute kwako William! You have a good point on that, watu wasiogope huu uwanja! Lakini tusiamini kuwa ni eneo stahili la chama flani... nadhani tunaweka hoja katika uwanja huu kwa maslahi ya watanzania na sio chama!

Salute Mkuu.

Unaposema "watu wasiogope huu uwanja! Lakini tusiamini kuwa ni eneo stahili la chama flani." Neno "chama" linaweza kuwa pana sana.

Linaweza kumaanisha chama cha siasa, kwa maana ya pengine CCM isione kwamba JF ni eneo stahili la CHADEMA kwa mfano.

Lakini pia chama kwa tafsiri ya kundi, kauli yako inaweza kutafsirika kama "tusiamini kuwa (JF) ni eneo stahili la "age group" fulani" yaani vijana tu.

Hii tafsiri ya pili ndio msingi wangu wa kutaka wito huu usiishie kwa wabunge vijana tu na uende kwa wabunge wote, kwani ni wito muhimu. Na kama hakuna mazingaombwe yasiyotaka kusemwa wazi, hakuna sababu ya kuwaita vijana tu.
 
- Sawa sawa Bro, ninasema waje hapa openly na majina yao wazi waulizwe maswali na wajibu maswali, binafsi will do everything in my power and influence kuona hili linafanikiwa, will talk to management kama inabidi ku-move some mountains kidogo ili kuwa-accomodate, sawa Jumapili nitakutana nao tena yaani Wabunge nitaendelea kuwaomba sana waje hapa kama walivyo!

William.

William nitakuona uko serious sana na hili kama utamleta Anne Kilango Malecela, mtu wa familia yenu kabisa ambaye una full access naye. Ukimleta huyu mie nitakuona uko serious katika hili na nitakupa support 100% katika initiative yako kwa mwingine yoyote.

Kama utaruka nyumbani kwenu na kuwashikia bango wengine mie nitakuona unafanya siasa tu na pengine una ajenda ya siri ambayo huisemi wazi.
 
Kijana wa CCM au mdau wa CCM ataongea nini hamna cha kuongea zaidi ya kukuelezea wanavyoibia nchi na kuchota hela
 
Well said William, hao waje humu jamvini ili waone na waungane na vijana wenzao, na waweze kubeba maoni ya vijana wenzao. Unapomuita mzee humu, ni wachache sana wanaoweza kubeba maneno mazito ya humu na kuyafanyia kazi. Wapo watakaopandwa na presha na kubaki kusema vijana hamna adabu. Vijana ndio size yetu...Waje waje...William nilikuona nao pale Diamond, kama ambavyo walikua wanashangilia kule tunataka sauti zao hapa as well...

Kwa nini una wa excuse wazee? Kwa nini unawasemea kabla hata wao wenyewe hawajasema? Je ni wazee wote walio hivyo? Waiteni tuone nani atachemka na nani atajibu kwa busara.

Usitake kuhukumu bila kuangalia ushahidi.
 
Back
Top Bottom