Wabunge Vijana Wa CCM: Tafadhalini Sana!

Apr 27, 2006
26,588
10,364
Wakuu wote JF, heshima mbele sana!

- Ninashangazwa sana na Wabunge wengi vijana wa CCM kuuogopa huu mtandao wa JF, I mean tena wengi wao wasomi wa ajabu, nimeongea nao sana kwa vipindi mbali mbali wengi wanaonyesha kuogopa sana hapa, hilo limenishitua sana. Wabunge Vijana wasomi, nilifikiri huu ndio uwanja pekee wa kuwasafisha na kuweka misimamo yao wazi of what they stand for!

- Majuzi nilikuwa na Mheshimiwa Hamis Kingwalallah proud of him, we talked a lot about Thread yake ya kwanini hakusaini karatasi ya Zitto, I mean I am again proud of him. He was very openminded and Zitto himself came we talked about it, unaona ni very positive regardless ya kejeli na matusi za hapa, lakini muhimu ni KUJA HAPA NA kuweka msimamo kama a politician tena kijana msomi, na ukaeleweka vizuri kuliko kuogopa matusi na kejeli. Leo tena nimeongea na Wabunge wengi sana pale Diamond Jubilee on JF, please njooni hapa!

- JAMANI WABUNGE VIJANA WA CCM MPO KWENYE SIASA SAWA NA BIASHARA YA UTUMBO SASA MSIOGOPE HARUFU, NJOONI HAPA TUMKOME NYANI, HUU SIO UWANJA WA CHADEMA NI UWANJA HURU WA KILA MWANANCHI KUSEMA MAONI YAKE NA NYINYI NI VIONGOZI WA HAWA HAWA WANANCHI, NJOONI HAPA KAMA MLIVYO MJIBU HOJA NA MUWEKE HOJA, MCHAMBULIWE TUONE KAMA KWELI MNA HOJA!

- MUNGU AIBARIKI TANZANIA!

William.
 
Wanaogopa nidhamu ya chama. Ukisema umkome nyani hapa JF, kesho yake utashangaa Mukama anakupigia simu na kukukoromea huku akikutishia kukushughulikia. Labda kama ni "kumkoma nyani giladi" kwa kujipendekeza kwa chama na serikali kushabikia hata uozo ulio wazi.

Kigwangala alipokwenda kuwaunga mkono madaktari wenzake kwenye mgomo wa mwezi March ilikuwa ni kama vile ametenda kosa la jinai au uhaini. Alipoenda Dodoma bungeni, wabunge wenzake wa CCM kwenye caucus yao walimshukia kama mwewe na wengine wakitaka ashughulikiwe. Sasa kwenye mazingira kama hayo, hakuna mbunge atakuwa na ujasiri wa kuja hapa na kuweka misimamo yake wazi, unless hiyo misimamo iwe ni kukilamba miguu chama na kuilamba miguu serikali. Ukienda kinyume na hapo hawachelewi kukushughulikia ki-chama.

CCM inataka watu wanafiki wa kutetea uozo wa chama na serikali. Ndio maana kwenye mijadala ya hoja nzito bungeni ni nadra kuwasikia hao wabunge vijana wakiweka misimamo yao wazi. Misimamo yako iko facebook ambako hakuna mijadala ya maana, hata akifuka pumba hakuna atakayehoji kama jinsi watu wanavyohoji hapa, sana sana akiona unamkera na hoja ngumu anaamua kukutoa kwenye orodha yake ya marafiki.

CCM haitaki watu ambao wako na open mind na wana ujasiri wa ku-speak their mind. CCM inatakiwa kuelewa kwamba kuna msimamo wa chama na kuna msimamo wa mtu binafsi. Mbunge anawakilisha wananchi, hawakilishi CCM huko Bungeni. Kinachomuunganisha na msimamo wa chama ni Itikadi tu, ambayo kwa sasa ndani ya CCM haipo.

Nidhamu ya Chama ndio ambayo inaua fikra za wabunge wengi wa CCM, kabla hawajasema kitu, anajiuliza kwamba hivi chama kitanielewa kweli? Hata kama hoja yake ina maslahi kwa umma, lakini bado atakuwa anagwaya kusema kwa kuogopa rungu la chama na hiyo ndio inawafanya wabunge wa upinzani wapande chat unnecessarily. Sometimes wabunge wa upinzani wanajizolea "maujiko" ya bure bila jasho. Ndio maana mara kwa mara utawasikia wabunge wa CCM wanalalama kwamba upinzani wameiba hoja yao, sasa kama ni hoja yenu mlikuwa mnangoja nini kuiweka wazi kwenye mjadala Bungeni?

Pamoja na hiyo nidhamu ya chama, lakini pia wabunge vijana wengi wa CCM ni "opportunists" wanavizia kupewa ulaji na hivyo ili waonekane kuwa ni "good boys", wanakuwa ni wanafiki ambao ukikutana nao pembeni kukata issues anaonekana yuko critical na mambo yanavyokwenda ndani ya chama na serikalini lakini akiwa kwenye official jukwaa la kutema sumu "bungeni" au kwenye vikao vya NEC, unashangaa anamwaga pumba tupu! Then unaanza kujiuliza, hivi huyu ndiye yule niliyekuwa naongea naye few days ago au ni mwingine? Ulaji dot com at work!
 
Age discrimination.

Kwa nini unafikiri JF ni uwanja wa vijana tu?

Mtu mwenye ndoto za kuwa kiongozi hatakiwi kuwagawa watu, anatakiwa kuwaunganisha. Habari za wabunge vijana/ wazee ni kuwagawa wabunge. Ongea ideas, sio kuwagawa wabunge kama mafungu ya dagaa.

Chukua somo la bure la leo, kama ego yako itakuruhusu kujifunza.
 
- Nimetoa somo kwa Wabunge vijana na wewe unaweza kuanzisha thread ya Wabunge wazee, mimi nia na madhumuni yangu kwenye hii thread ilikuwa ni Wabunge Vijana tu, ambao ninashirikiana nao sana kila siku ya Mungu, leo nilikuwa nao na Jumapili nitakuwa nao tena, I mean kama huna uhakika na ishu ni kuuliza kwanza, kuliko kukurupuka kama ulivyofanya, tizama heading kwanza kabla ya kukurupuka next time! ha1 ha! ha!

William.
 
Hapa ni mahali pa kupoteza wakati si pa wanasiasa na viongozi kukaa na kuwa mateja ya JF.

Wewe William ni Potato coach hata mwili wako unaonesha ni mtu uunaeweza kukaa kwenye lap top yako kutwa nzima.

Hoja na shughuli wazijibu hukohuko, hapa wawaachie magwanda na sisi tunatosha kuwa kong'oli.
 
Hapana,

Ulichofanya hapa ni kitu kinaitwa "age discrimination". Ume discriminate wazee ambao wengine tunawaheshimu sana. Habari ya wajibu wa wabunge kuwa karibu na wananchi wao, na kuja kutoa vipande hapa JF, ni ya wabunge wote. Sasa kwa nini wewe ufanye hii ni habari inayowahusu wabunge vijana tu? Unamaanisha kwamba hutegemei wazee waweze kuja hapa, na wala huwashikii bango. Una wa discriminate. Unatuonyesha kwamba akilini mwako unafikiri kwamba wazee hawawezi na hata hawafai kufuatiliwa kwa hili.

Hii age discrimination haina tofauti na gender discrimination au racial discrimination.

Ungesema hapa "wabunge wanawake hamji hapa JF" tungeona mlipuko wa watu kusema kwamba unaleta gender discrimination.

Sasa umesema vijana, watu hawako sensitive sana na age discrimination lakini mii naiona.

Acha kubagua wabunge kwa dini, kabila, jinsia au umri. Hizi zote ni discrimination tu.
 
Age discrimination.

Kwa nini unafikiri JF ni uwanja wa vijana tu?

Mtu mwenye ndoto za kuwa kiongozi hatakiwi kuwagawa watu, anatakiwa kuwaunganisha. Habari za wabunge vijana/ wazee ni kuwagawa wabunge. Ongea ideas, sio kuwagawa wabunge kama mafungu ya dagaa.

Chukua somo la bure la leo, kama ego yako itakuruhusu kujifunza.
Kiranga, binafsi sijaona age discrimination yeyote kwenye thread hii, ni sawa na kualika kikundi chochote au wabunge wanawake huwezi kusema ni hiyo ni gender discrimination. Tukitumia notion yako hiyo kuna siku tutaogopa kujumuika na vijana wenzetu kwa hofu ya kuambiwa wabaguzi.
 
Kisa cha ku limit swali kwa vijana ni nini?

Tungekuwa tuna wabunge wazee wengi wapo hapa, na wabunge vijana wanakosekana, William angekuwa na point.

Actually mie ningemuona ana point kubwa zaidi angesema wabunge wazee hamji JF kwa sababu angalau hao vijana tunawaona wawili watatu kina Kigwangwallah, Mnyika, Zitto wanakuja.

Wazee hatuwaoni kabisaaa.

Sasa point ya kusema vijana hawaji ni nini?

Anaonekana kama mtu aliyewatoa wazee katika stahiki ya kuja hapa, anafanya JF kuwa ni ukumbi stahiki wa vijana tu, ndiyo maana anawashikia bango vijana.

Ndiyo maana ninamwambia aache age discrimination.

Kama anataka kusema wabunge hawaji hapa kutoa maoni, aseme hivyo.

Kuanza kuweka mafungu yasiyokuwa reflected na reality ni noma kwa sababu wabunge vijana wanakuja kuliko wazee, kwa hiyo kusema wabunge vijana hawaji bila kusema wabunge wazee hawaji does not make sense, unless you do not expect at all wazee waje.

Kawabagua wazee. Hajawapa haki yao ya stahiki ya kuja kwa wananchi/ JF inayoambatana na scrutiny kama hawaji.

Wengine tunaweza kusema kwamba anawaonea vijana na kuwaogopa wazee, kama anavyosema vijana wanaogopa kuja JF.

Muoga anakemea uoga.
 
unaposema 'tumkome nyani' unamaanisha nini? Kwa status unadhani linafaa?

Anyway,

ni vyema ulivyowashawishi kujiunga, wasiogope mitandao....
 
Hapana,

Ulichofanya hapa ni kitu kinaitwa "age discrimination". Ume discriminate wazee ambao wengine tunawaheshimu sana. Habari ya wajibu wa wabunge kuwa karibu na wananchi wao, na kuja kutoa vipande hapa JF, ni ya wabunge wote. Sasa kwa nini wewe ufanye hii ni habari inayowahusu wabunge vijana tu? Unamaanisha kwamba hutegemei wazee waweze kuja hapa, na wala huwashikii bango. Una wa discriminate. Unatuonyesha kwamba akilini mwako unafikiri kwamba wazee hawawezi na hata hawafai kufuatiliwa kwa hili.

Hii age discrimination haina tofauti na gender discrimination au racial discrimination.

Ungesema hapa "wabunge wanawake hamji hapa JF" tungeona mlipuko wa watu kusema kwamba unaleta gender discrimination.

Sasa umesema vijana, watu hawako sensitive sana na age discrimination lakini mii naiona.

Acha kubagua wabunge kwa dini, kabila, jinsia au umri. Hizi zote ni discrimination tu.

- Haya ni maneno yako, siwezi kuwaa-address wabunge ambao sijajadili nao ishu ya JF, so far nimekwua nikijadili JF na wabunge Vijana tu, hayo mengine ni yako ila for me nia na madhumuni ilikuwa ni kuwalenga Wabunge Vijana na wewe unaweza kufungua Thread ya Wabunge wazee iwapo utapata nafasi ya kujaidli nao JF kama ninavyofanya kila wakati na Wabunge vijana!

- I mean na will not answer tena maana nitatoka kwenye focus ya this subject, lakini hope somo limeleweka!

William.
 
Hapa ni mahali pa kupoteza wakati si pa wanasiasa na viongozi kukaa na kuwa mateja ya JF.

Wewe William ni Potato coach hata mwili wako unaonesha ni mtu uunaeweza kukaa kwenye lap top yako kutwa nzima.

Hoja na shughuli wazijibu hukohuko, hapa wawaachie magwanda na sisi tunatosha kuwa kong'oli.

- Siku zote nina heshima sana na hoja zako, ni muhimu sana wakaja hapa na kupangua hoja maana zingine ni jibu moja tu na thread inakwisha, kuhusu mwili wangu dont worry Mungu hatoi mzigo bila kukupa mabega ya kuubeba! ha! ha! ha! ha! I mean bado nina-enjoy Organic to the fullest, maana kule majuu ilikuwa frozen food kama magazeti tasteless, mambo hapa kikuku cha kienyeji super sana, ha! ha! ha! halafu sambusa na maandazi, na vitumbuwa saafi sana so haina shida bro!

- Wabunge waje hapa wajibu hoja, itasaidia sana kupunguza kelele hapa!

William.
 
Kisa cha ku limit swali kwa vijana ni nini?

Tungekuwa tuna wabunge wazee wengi wapo hapa, na wabunge vijana wanakosekana, William angekuwa na point.

Actually mie ningemuona ana point kubwa zaidi angesema wabunge wazee hamji JF kwa sababu angalau hao vijana tunawaona wawili watatu kina Kigwangwallah, Mnyika, Zitto wanakuja.

Wazee hatuwaoni kabisaaa.

Sasa point ya kusema vijana hawaji ni nini?
Kiranga, sioni kama una point yeyote kwa kusema kwanini vijana na siyo wazee, hata unaposema angealika wazee huoini pia na wewe unaingia kwenye kitu kile kile unachokipinga?, tofauti yake ni sababu tu mnazotumia. Mimi sioni ubaya na kama Willy alivyokushauri wewe unaweza kuanzisha thread ya wazee au ya wabunge wote kabisa, ili hii uache watu waendelee na mada iliyopo.

Discrimination is a very broad term halina mipaka hata kama angeanzisha thread ya wabunge wote ungesema kwa nini asianzishe ya watanzania wote?
 
Hapa ni mahali pa kupoteza wakati si pa wanasiasa na viongozi kukaa na kuwa mateja ya JF.

Wewe William ni Potato coach hata mwili wako unaonesha ni mtu uunaeweza kukaa kwenye lap top yako kutwa nzima.

Hoja na shughuli wazijibu hukohuko, hapa wawaachie magwanda na sisi tunatosha kuwa kong'oli.
Kong'oli ndio nini? Hebu acha kuleta lugha za kwenye maigizo hapa jf. Bora William tunajua ni mnene kuliko wewe unayejificha na hiyo id huenda upo Kama Mzee wa gombe
 
Naunga mkono..
ingependeza zaidi kuona jinsi wanavyojitetea au jinsi wanavyotoa na kupokea maoni..
mara nyingi na majibu mengi hapa JF ni mambo ya ku "guess" ingependeza kama wao
wangetupa ukweli wa mambo. waache uogo hakuna mtu anaekula watu hapa. na huu
ni mtandao tu ... KARIBUNI JAMII FORUM.
 
Wako tayari wakose hata posho kuliko kuja hapa JF wanaona Kama ni kikaango wanataka sehemu za kusifiwa Kama FB si unakumbuka tokea kigwagallah aje hapa akachanwa hajawahi kuonekana tena!!!!!
 
Precise pangolin
hakuna mtu anae ishi kwa kusifiwa tu dunia hii..

mtu huwa anaogopa kama kweli amefanya kosa. kama huna kosa unaogopa nini?
wenyewe kama viongozi wanatakiwa wawe tayari kutetea Chama Chao "CCM" na pia
kutetea nafsi zao. haina maana ya kuwa kiongozi kama unaogopa comment za watu.
angalia Mkuu W. J. Malecela kila mara anapondwa hapa jamvini bado anarudi na kutetea
au kusimamia anacho amini... kwa hilo nampa pongezi.
 
Last edited by a moderator:
Hapana,

Ulichofanya hapa ni kitu kinaitwa "age discrimination". Ume discriminate wazee ambao wengine tunawaheshimu sana. Habari ya wajibu wa wabunge kuwa karibu na wananchi wao, na kuja kutoa vipande hapa JF, ni ya wabunge wote. Sasa kwa nini wewe ufanye hii ni habari inayowahusu wabunge vijana tu? Unamaanisha kwamba hutegemei wazee waweze kuja hapa, na wala huwashikii bango. Una wa discriminate. Unatuonyesha kwamba akilini mwako unafikiri kwamba wazee hawawezi na hata hawafai kufuatiliwa kwa hili.

Hii age discrimination haina tofauti na gender discrimination au racial discrimination.

Ungesema hapa "wabunge wanawake hamji hapa JF" tungeona mlipuko wa watu kusema kwamba unaleta gender discrimination.

Sasa umesema vijana, watu hawako sensitive sana na age discrimination lakini mii naiona.

Acha kubagua wabunge kwa dini, kabila, jinsia au umri. Hizi zote ni discrimination tu.

Divide and Rule
 
Dogo William hiyo list ya makulaji hapo mwishoni imenijaza mate mdomoni,zilikuwa zangu enzi zile pale JOJIZI Bank House.
Angalia sana hivyo vitumbua na sambusa na vichaichai kwa jinsi mwili wako ulivyo na shukrani inabidi uwe una jog 5 miles kila siku.
- Siku zote nina heshima sana na hoja zako, ni muhimu sana wakaja hapa na kupangua hoja maana zingine ni jibu moja tu na thread inakwisha, kuhusu mwili wangu dont worry Mungu hatoi mzigo bila kukupa mabega ya kuubeba! ha! ha! ha! ha! I mean bado nina-enjoy Organic to the fullest, maana kule majuu ilikuwa frozen food kama magazeti tasteless, mambo hapa kikuku cha kienyeji super sana, ha! ha! ha! halafu sambusa na maandazi, na vitumbuwa saafi sana so haina shida bro!

- Wabunge waje hapa wajibu hoja, itasaidia sana kupunguza kelele hapa!

William.
 
42 Reactions
Reply
Back
Top Bottom