Wabunge 3 (CCM) waisaliti Serikali

Lakini pia kuna wakati plato aliwahi kusema you can't have competent and good leaders out of foolish and roten generation.kwa sababu viongozi wanatoka katika hiyohiyo jamii.what to do first ni kuondoa huu ujinga kwa wananchi
 
Kuna mbinu nyingi katika mapambano, na kina mbinu ina advantage na disadvantage. Chadema baada ya uchaguzi walianza na kulikimbia bunge na kikwete, mbinu hiyo ilizaa matunda kwa serikali kunyong'onyea na kuanza harakati za Katiba kitu kinachoendelea hadi sasa. Mbinu nyingine waliyotumia ni mikutano ambayo ilisaidia kuelimisha umma, kama wangekubali na vitisho vya kusitisha hayo haya yanayotokea leo yasingetokea, ingebaki kama ilivyokuwa NCCR Mageuzi kilipokuwa chama cha msimu na kuibuka wakati wa uchaguzi tu.

Hawa wabunge waliotoka nje ya kikao wakati wa kupiga kura ya kupitisha bajeti, dhamiri zao ziliwasuta kutokukubaliana, na hivyo kutoka nje ya kikao ni mojawapo ya option itumikayo katika mabunge mengi duniani. Wanacho cha kuwaelewa wapiga kura wao kivitendo kwamba waligomea bajeti hiyo na kutoka isijeonekana wamshiriki kupitisha.

I think you might be Right
 
nawapenda sana kangi lugora na deo filikunjombe,hawa ndo wanaccm wa kweli,na kwa mwendo huu wameshajikatia tiketi kuingia bungen 2015,nlikuwa na nia ya kugombea mwibara sasa kupitia ccm sasa basi lugora anatosha,
 
Hawa wabunge tatizo lao wapo kwenye kuipinga serikali ya chama chao na sio kuikosoa serikali yao,kwa hiyo chama chao kinataka wasipinge wakosoe kama wanataka kupinga then wa wahame chama waungane na vyama vya upinzani ili wapinge ndiyo maana wakaitwa wapinzani!!!
 
Hivi hata wangepiga kura ya kuikataa hiyo bajeti ingekwama kwa kura zao tu? Wengine waliokuwa wnaibishiawala hawajui implications. Kwa vile fulani kabishia basi na yeye anabisha!
 
Wanakurupuka usingizini, wanagonga mabenchi, wanaunga hoja asilimia mia kaliki wanaikosoa. Weanaitwaje hawa?
 
wapi wapiganaji asilia ndani ya ccm, mbona mmeniangusha -- mama kilango, ole sendeka ....au bahasha zilifanya kazi yake?
 
[yeaa kaka, hoja ngumu zenye manufaa zatakiwa sana........uma umeshaanza kuelewa sana,huu ndo wakati muafaka,let's di it to the maximum
 
Yeeeeeesssssssss, we can. Lets join together to fight it. Ninachofurahi vijana na wasomi wengi wanafunguka akili na kuelewa kile ambacho tunapambana nacho. Ukiona hadi vijijini moto unawaka ujue kuuzima ipo kazi, na watakaposhtukia nyumba imeteketea.Tunatakiwa kuwa kitu kimoja, kujenga uvumilivu, kuelimisha umma bila kuchoka, papo kujitahidi kukosoa pale ambapo wapambanaji wanapoteleza, vinginevyo tutaendekeza yale yale. Huu ndio ukomavu, maana makamanda wakikosea step katika mapambano, wanarudi kujipanga upya na mbinu mpya baada ya kusoma mkao wa adui.[yea kaka huo ndo ukweli, kuna kila haja ya kujipanga sana.tunapeleka elimu mpaka vijijini]
 
Wanashangaza sana kutojua kwamba wao wametokana na ccm na Bajeti ndiyo determining instrument unayoitafuta kupitia kura. Ebo, kwani basi unatekelezaje ahadi ulizotamka kwenye ILANI yako? Kwani lazima iandikwe kwa urahisi wa uelewa wako tu?
Nadhani kutafuta umaarufu kumewazidi. Mwisho wao mbaya.
Hata hivyo CCM nao hawajapa seminar wabunge wao. Hili ni jambo muhimu.
 
Naomba mmnieleweshe wadau hivi inakuaje mbunge anaamka anaunga hoja mkono mia kwa mia kabla ya kuongea then anaanza kulalamika maji,umeme,barabara,nk.alichokiungia mkono mwanzo ni nini???huu ni UDHAIFU TENA MMBAYA
 
ukivuta bangi ndio unatuma thread mbona hata majina ya hao wabunge watatu wa CCM hujataja?

Ni kawaida ya wapambe wa CCM wakiishiwa hoja ni matusi na kumshambulia mtu binafsi badala ya hoja inayojadiliwa.

Hivi we mwenzetu unajadili kichwa cha habari bila kusoma habari yote? Picha za wahusika na majina yao hujaziona kwenye mada hii amayo imetoholewa kutoka vyombo vya habari pamoja na kivuli cha taswira ya gazeti?

Labda unatumia simu ambayo haina nguvu ya kufungua taswiras na body nzima ya habari la sivyo kila anayesoma comment yako anakushangaa swali ulilouliza.
 
Back
Top Bottom