Wabeba mabox vs wala vumbi: Chuki ya nini??

Semilong

JF-Expert Member
Mar 5, 2009
1,712
219
Siku hizi kumekuwa kuna tabia ya mtu ukitoka nje ukimuambia mtu kitu hata kama ni cha ukweli yeye ananga'ng'ania kubisha na kukuita mbeba box
unakuta unamuambia mtu kutokana na wewe umeona upande mwingine wa dunia lakini hataki kukusikiliza sio kama yeye anahoja hapana bali ni kutaka kukuletea zarau...
Na wengi wanakua wanaongea kwa chuki sana huku wakikuita mmbeba box

cha kujiuliza kwa nini kumekuwa na chuki kati ya wabeba mabox(watz wa nje) na wala vumbi(watz walioko tz)????
 
Chuki ya nini wakati wote ni waTZ. Tupendane tu na tusaidiane. Tuachane na ubishi usiokuwa wa maendeleo. Tuungane kupiga vita ufisadi.Tukae pamoja tuijenge Tanzania yetu.
 
Hao wenye chuki ni wale wasioelewa chochote kuhusu wenzao.Siyo kila aliye nje ni mbeba box..na pia siyo kila aliye TZ ni mla vumbi!
kama anabeba box au ha bebi sidhani anastahili chuki yeyote
tuondoe matabaka
neno mla vumbi ni responce ya mmbeba box
 
The truth is a majority of Africans who immigrate to the U.S. do manual labor na wana kua kwenye welfare ukilinganisha na immigrants toka nchi nyingine say za Asia ambao wao ni 1% ya immigrants but they are the biggest tax contributors of all immigrant groups. Hizi stereotype za ubeba mabox ina tokana na ukweli usio fichika kwamba majority of Africans in the U.S. and Europe are not blue collar workers(siyo wote). So hata kwa Tanzania the more Tanzanians who are seen to make something of themselves nje the more the "mbaba mabox" label will disappear. Maana kuna watanzania wanakaa nje miaka bila kurudi na wanapo rudi Tanzania they have nothing to show for it sasa watu wata draw conclusion gani?

With that said, naamini hizi kauli za mbeba mabox ni stereotypes na ina vunjia wengi heshima. Siyo vizuri kumlabel mtu in an offensive way. Iwe changamoto kwa watanzania nje kusaidiana na kumake something of themselves ili siyo kila Mtanzania aliepo nje aonekane ana beba mabox. Mnaweza msikubaliane na maneno yangu but I think it's the truth.
 
Siyo kweli kwamba Waafrica wengi wanao-immigrate in the US wanaishia kwenye welfare labda kwa wale wanakuja kama political asylee. Kama ulikuwa na maana ya kusema Wasomali hapo ni sawa kabisa kwani hao ndio wanaishia kwenye Public housing na food stamp. Ni vigumu kwa Mtanzania kumuunganisha kwenye hiyo group kwani walio wengi wanakuja kwa student visa, na wachache wanakuja kwa green card kitu ambacho hawa-qualify kupata hivo vitu.
 
Siku hizi kumekuwa kuna tabia ya mtu ukitoka nje ukimuambia mtu kitu hata kama ni cha ukweli yeye ananga'ng'ania kubisha na kukuita mbeba box
unakuta unamuambia mtu kutokana na wewe umeona upande mwingine wa dunia lakini hataki kukusikiliza sio kama yeye anahoja hapana bali ni kutaka kukuletea zarau...
Na wengi wanakua wanaongea kwa chuki sana huku wakikuita mmbeba box

cha kujiuliza kwa nini kumekuwa na chuki kati ya wabeba mabox(watz wa nje) na wala vumbi(watz walioko tz)????

Sioni ubaya wowote kwa mtu akiitwa mbeba box. Hata kama ubebi box; hii ni kauli nzuri na lugha nzuri kutumiwa na mtu yoyote au mwanasiasa yoyote. Hii ni changamoto nzuri kwa WTZ waliopo bongo. Kwanza, inamfanya MTZ aliepo TZ kuipenda nchi yake bila ya kuwa na tamaa ya kwenda nje ya nchi. Kwa sababu, atakuwa hapendi kwenda Ulaya kubeba box. Pili, itawasaidia WTZ wengi kisaikologia, WTZ wengi wataaamini kwamba zile kazi wanazozifanya ni bora kuliko kubeba box Ulaya. Kwa hiyo, itasaidia kuwapa hope WTZ wengi waliopo home, kujenga Taifa bila ya kuwa na mawazo ya kwenda Ulaya tu. Hii ni theory.
 
Bahati nzuri nimetembelea ulaya na amerika na nimekulia kijijini na kuishi dsm. Hapo zamni kidogo mpaka mwishoni mwa miaka ya 90 ulikuwa ukienda nje unaonekana mtu wa maana sana kwani watu walio kuwa nje ya nchi waliweza kurudi na magari na kujenga nyumba nk. Na wakaanza kuwaita walioko Bongo washamba na pia kuwa bongo ni nchi ya vumbi na anayeishi huko ni mla vumbi.

Baadaye vijana wengi wakaforge vyeti waonekane walifaulu F.VI wakaingia mtoni kwa students VISA halafu hawakusoma wakaingia kupiga kazi warudi na pesa. Matokeo yake hata dola nayo ikawa ngumu sana kuchanga. hasa baada ya september 11 maisha yalibadirika ghafla kwa wabeba box.

waliporudi Bongo wakatukuta wenzao tulioenda DSA, SUA, IFM, IDM, UD nk tume-make. Kwani Ufisadi ukawa nao umepamba moto bongo, deal zikawa nje nje tu, walioko mtoni wanarudi wanshangaa walioko bongo wanaendesha magari makali, wana nyumba nzuri, wanajirusha every weekend.

Tukaanza kuwaazima magari waliotoka mtoni wakasalimie mikoani, tukaanza kuwapa accomodation hata kuwaazima simu maana simu zao za subscription hazikuweza kuroam bongo. Ndipo sisi wala Vumbi tulipo anza kuwadharau hawa washikaji wa kutoka mtoni na ndipo tulipolipiza kisasi cha kutuambia twala vumbi na kuwaambia kuwa wanabeba box.

UFISADI ukiisha pesa za deal deal zikiisha, hakuna vijisecond hand vya japan, tutaanza kuwaheshimu tena wabeba box. Kwasasa mutuache tu, samahani sana, Heshima hailazimishwi.
 
Shame on you. Unakuja hapa kusifia UFISADI? Unajua WTZ wangapi wanakufa kwa njaa kila siku kwa sababu ya watu kama nyinyi mnaondekeza UFISADI? Shame on you.
 
Last edited:
Kwanza inabidi tujiulize mbeba box ni kazi za jinsi gani? Je hizi kazi bongo zipo au hazipo. Kwa mtazamo wangu wa sehemu zote mbili ughaibuni na bongo hizi kazi za kubeba box watu wote wanazifanya uwe bongo au ughaibuni, lazima hizi kazi zipo na zinawafanyakazi. Maana hata hapa bongo sio kwamba kila mtu kasoma ili afanye kazi hizo za ofisini.
Vile vile kama Ughaibuni sio kila mtanzania anafanya kazi za kubeba box , wapo watu wanafanya kazi za maana tu.Wapo kwenye vitengo vya maana tu huko ughaibuni, hapa inategemea ughaibuni ulienda kivipi. Kama ulienda kama mtembezi halafu ukazamia hapo kweli unaweza kubeba box. Ila kama ulienda kusoma na baada ya kumaliza skul wakapenda utendaji wako na kukupatia Visa vya kufanyia kazi hapo wala hutalijua box.
hivyo uwe bongo au ughaibuni kazi za box zipo tu, isitoshe huko ughaibuni hata hao wazawa wenyewe wanazichapa hizi kazi za box, sembuse mtu wa kuja!!!
Vile mbeba box wa Ulaya/USA usimfananishe na mbeba box wa Tanzania ni vitu viwili tofauti. Mbeba box wa ughaibuni pato lake kubwa tofauti na wa Tanzania. Utakuta mshahara anaoupata mbeba box wa Ulaya/USA kwa wiki au kwa mwezi na akitoa zile expenses za life bado atakuwa sawa au atamzidi yule mfanyakazi wa serikali ya Kikwete.
Hivyo chuki hazitakiwi baina ya watu hawa wawili, kila mtu inabidi awe na respect kwenye kazi ya mwenzie. Maana hiyo kazi anayofanya mwenzio ndio inamuweka mjini.
 
Tupo tuliobeba maboksi. Na sasa tunakula hilo mnaloliita vumbi. Sisi mnatuweka wapi?
 
Pretty uchambuzi wako ni mzuri. Kwa kuongezea inabidi uangalie kama hii ni chuki kati ya mbeba maboxi wa Ulaya/Marekani na mbeba maboxi wa Afrika/Tanzania au ni kati ya wabeba maboxi wa ughaibuni na watu wa daraja la kati kiasi hapa bongo. Mimi nadhani ni chuki kati ya hilo kundi la pili. Na maadam nimekuwa kwenye makundi hayo yote mawili na kuyasoma kwa undani naamini chuki hiyo inatokana na wivu na uchungu. Wabeba maboxi wana uchungu na wivu kuwa wenzao waliokuwa sawa nao au waliosoma nao sasa wanatesa kinoma bongo tena kwa hela ya mkononi (cash economy). Pia kuna walioko bongo ambao wana uchungu na wivu kuwa kuna wabeba maboxi wanaotumia vizuri uchumi wa mikopo (credit economy) ambao wanafanya vitu vikubwa huku nyumbani na kuwapiga bao. Kwa ufupi, kila kundi linatamani na kudharau cha kundi lingine.

Angalizo: Pia lipo kundi ambalo linaamini kwa dhati kabisa kuwa wabeba maboxi wengi waliodanganywa wamelosti huko majuu na halitaki wala vumbi wetu wakalosti huko hivyo linawapa tahadhari wasifuata mkumbo!
 
Bahati nzuri nimetembelea ulaya na amerika na nimekulia kijijini na kuishi dsm. Hapo zamni kidogo mpaka mwishoni mwa miaka ya 90 ulikuwa ukienda nje unaonekana mtu wa maana sana kwani watu walio kuwa nje ya nchi waliweza kurudi na magari na kujenga nyumba nk. Na wakaanza kuwaita walioko Bongo washamba na pia kuwa bongo ni nchi ya vumbi na anayeishi huko ni mla vumbi.

Baadaye vijana wengi wakaforge vyeti waonekane walifaulu F.VI wakaingia mtoni kwa students VISA halafu hawakusoma wakaingia kupiga kazi warudi na pesa. Matokeo yake hata dola nayo ikawa ngumu sana kuchanga. hasa baada ya september 11 maisha yalibadirika ghafla kwa wabeba box.

waliporudi Bongo wakatukuta wenzao tulioenda DSA, SUA, IFM, IDM, UD nk tume-make. Kwani Ufisadi ukawa nao umepamba moto bongo, deal zikawa nje nje tu, walioko mtoni wanarudi wanshangaa walioko bongo wanaendesha magari makali, wana nyumba nzuri, wanajirusha every weekend.

Tukaanza kuwaazima magari waliotoka mtoni wakasalimie mikoani, tukaanza kuwapa accomodation hata kuwaazima simu maana simu zao za subscription hazikuweza kuroam bongo. Ndipo sisi wala Vumbi tulipo anza kuwadharau hawa washikaji wa kutoka mtoni na ndipo tulipolipiza kisasi cha kutuambia twala vumbi na kuwaambia kuwa wanabeba box.

UFISADI ukiisha pesa za deal deal zikiisha, hakuna vijisecond hand vya japan, tutaanza kuwaheshimu tena wabeba box. Kwasasa mutuache tu, samahani sana, Heshima hailazimishwi.

**************************************************************
Je mmeacha kuchambia kopo???
 
Kwa maoni yangu kuishi nchi za watu na kuyamudu maisha, bila 'kupiga' mahali ni kuonesha una akili nyingi. Mazoba hawawezi kuishi nchi za watu maanake inabidi uwe na kila kitu proper in order. Bongo kila kitu slow na ujanja wa kubomoa nchi, na hata hao wanaojiita wana pesa sijui wana-enjoy nini..

Kila kitu kwa misele tu..huduma za jamii ovyoovyo, watu wamenunanuna tu..hata sehemu za 'kujinyoosha' zenyewe mgogoro, achilia mbali vitu katalogi wanakubambikizia feki au wanakuwekea bei za kupiga. Ahh ukiwa nchi za watu salala...wala vitu online, huduma za jamii fresh bin murua, hata kama unaishi maisha ya kati naamini unajichanua kuliko milionea fisadi wa bongo.
 
Pretty uchambuzi wako ni mzuri. Kwa kuongezea inabidi uangalie kama hii ni chuki kati ya mbeba maboxi wa Ulaya/Marekani na mbeba maboxi wa Afrika/Tanzania au ni kati ya wabeba maboxi wa ughaibuni na watu wa daraja la kati kiasi hapa bongo. Mimi nadhani ni chuki kati ya hilo kundi la pili. Na maadam nimekuwa kwenye makundi hayo yote mawili na kuyasoma kwa undani naamini chuki hiyo inatokana na wivu na uchungu. Wabeba maboxi wana uchungu na wivu kuwa wenzao waliokuwa sawa nao au waliosoma nao sasa wanatesa kinoma bongo tena kwa hela ya mkononi (cash economy). Pia kuna walioko bongo ambao wana uchungu na wivu kuwa kuna wabeba maboxi wanaotumia vizuri uchumi wa mikopo (credit economy) ambao wanafanya vitu vikubwa huku nyumbani na kuwapiga bao. Kwa ufupi, kila kundi linatamani na kudharau cha kundi lingine.

Angalizo: Pia lipo kundi ambalo linaamini kwa dhati kabisa kuwa wabeba maboxi wengi waliodanganywa wamelosti huko majuu na halitaki wala vumbi wetu wakalosti huko hivyo linawapa tahadhari wasifuata mkumbo!

Nadhani uchambuzi wako ndugu umetoa elimu tosha kwa makundi yote mawili.Asante.
 
Kwa maoni yangu kuishi nchi za watu na kuyamudu maisha, bila 'kupiga' mahali ni kuonesha una akili nyingi. Mazoba hawawezi kuishi nchi za watu maanake inabidi uwe na kila kitu proper in order. Bongo kila kitu slow na ujanja wa kubomoa nchi, na hata hao wanaojiita wana pesa sijui wana-enjoy nini..

Kila kitu kwa misele tu..huduma za jamii ovyoovyo, watu wamenunanuna tu..hata sehemu za 'kujinyoosha' zenyewe mgogoro, achilia mbali vitu katalogi wanakubambikizia feki au wanakuwekea bei za kupiga. Ahh ukiwa nchi za watu salala...wala vitu online, huduma za jamii fresh bin murua, hata kama unaishi maisha ya kati naamini unajichanua kuliko milionea fisadi wa bongo.

Ukweli mtupu!
 
Unajua maisha hayana formula na mwisho wa siku ni jinsi gani mtu anaweza kumudu mahitaji yake ya kila siku, kuweka akiba, na ku'invest' (rejea somo la uchumi). Hii haijalishi unafanya kazi gani au unaishi wapi. Kwa wale waliosoma kitabu cha "think like a millionaire" kuna usemi kuwa "...you can be right or you can be rich but you cant be both...". kuwa right inamaanisha kuwa mtu amekuwa katika comfort zone fulani na hataki kutafuta challenge za maisha. yeye uamini kuwa chote anachofanya ni sahihi. na kwa upande mwingine wale wanaojaribu mambo ambayo ni ya ziada ndio hufanikiwa (being rich). Inawezekana wengi ambao wako bongo walipenda kwenda "majuu" lakini kwa sababu moja au nyingine walishindwa na wakawa hapo walipo. Na inawezekana kuwa wale walio "majuu" siku moja hapo nyuma walifikiria kwenda ughaibuni kuna mahusiano na mafanikio katika maisha. Na si aliye ughaibuni anabeba mabox na siye kila aliye tanzania anakula vumbi. Hakuna cha kujutia wala kutupiana maneno kwamba ni mbeba mabox au mla vumbi kwani ni njia ya kusaka shillingi ili kumudu maisha! kwani si kweli kuwa kuna wengi walio hapa bongo na al-maarufu kwa kupiga mizinga! unapoamua kumsaidia rafiki yako unayemuita mbeba mabox ni utashi wako na haitii akilini unatoka mlango wa nyuma unamsanifu! Kuwa na nyumba na magari makali si kipimo cha mafanikio ya maisha, na ukweli usiopingika kuwa ngozi nyeusi inapopata visenti kidogo basi hukimbilia kwenye matanuzi zaidi na kujionyesha kuwa wao ni top in town! Kila mtu ana mipango yake na kila kitu hufanyika kwa wakati muafaka.
 
Kwa maoni yangu kuishi nchi za watu na kuyamudu maisha, bila 'kupiga' mahali ni kuonesha una akili nyingi. Mazoba hawawezi kuishi nchi za watu maanake inabidi uwe na kila kitu proper in order. Bongo kila kitu slow na ujanja wa kubomoa nchi, na hata hao wanaojiita wana pesa sijui wana-enjoy nini..

Kila kitu kwa misele tu..huduma za jamii ovyoovyo, watu wamenunanuna tu..hata sehemu za 'kujinyoosha' zenyewe mgogoro, achilia mbali vitu katalogi wanakubambikizia feki au wanakuwekea bei za kupiga. Ahh ukiwa nchi za watu salala...wala vitu online, huduma za jamii fresh bin murua, hata kama unaishi maisha ya kati naamini unajichanua kuliko milionea fisadi wa bongo.

Kwenye huduma za jamii hapo wengi huomba Mungu sana wanapokuwa Bongo wasifikwe na lolote maana hizo huduma zinatisha sana. Mfano Mke, Mume na watoto walikuwa Bongo siku yakuondoka na kurudi makazi mapya ndiyo wako kwenye pipa Mume anamwambia Mke namshukuru Mungu sana....Mke anajibu najua unashukuru nini mpenzi. Mume anauliza niambie ninashukuru nini....Mke anajibu kwamba tumejaliwa muda wote tuliokaa Tanzania wote hatukuugua...Mume anajibu hukukosea kabisa mpenzi maana hospitali zetu zinatisha! unaweza kuambulia gonjwa lingine huko.
 
Last edited:
Kwa maoni yangu kuishi nchi za watu na kuyamudu maisha, bila 'kupiga' mahali ni kuonesha una akili nyingi. Mazoba hawawezi kuishi nchi za watu maanake inabidi uwe na kila kitu proper in order. Bongo kila kitu slow na ujanja wa kubomoa nchi, na hata hao wanaojiita wana pesa sijui wana-enjoy nini..

Kila kitu kwa misele tu..huduma za jamii ovyoovyo, watu wamenunanuna tu..hata sehemu za 'kujinyoosha' zenyewe mgogoro, achilia mbali vitu katalogi wanakubambikizia feki au wanakuwekea bei za kupiga. Ahh ukiwa nchi za watu salala...wala vitu online, huduma za jamii fresh bin murua, hata kama unaishi maisha ya kati naamini unajichanua kuliko milionea fisadi wa bongo.

Hilo la vitu feki bongo usiseme,wizi mtupu.Mfano hai energy saving bulbs bongo life yake haizidi miezi 3 hadi minne.Nilibahatika kupata free sample energy saving bulbs( British Gas switch to Green Promo )leo miaka bado zinadunda,labelled 10 years life based on 10,000 hours
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom