Wabeba mabox vs wala vumbi: Chuki ya nini??

Vipi kundi la nne ambalo hamjalijadili, la wala vumbi wanaenda nje kupumzika na kujionea dunia nyingine?.

Home ni home hata kama ni shambani au pangoni, ukiwa home popote unapoenda unapata heshima yako. Majuu hata ukiwa na pesa na kama hujulikani ukienda viwanja vya juu bado hupati heshima au kuthaminiwa kama mtu mweupe.

Wabeba mabox wapo na wala vumbi wapo na waliobeba mabox na sasa wanakula mavumbi pia wapo, pia kuna wala mavumbi wanaokwenda kuwatazama wabeba mabox kila mara.

Swala la exposure ni suala la hela tu. Kama umepitia elimu ya kizungu na kupata vi senti exposure inakuja tu....una jipeleka mwenyewe mamtoni kutembea.

Sidhani kama ni chuki kama mnavyoi brand hapa, nadhani ni ukweli kuwa walio majuu wanafikiri waliopo TZ hawaelewi kitu wala hawana exposure. Sasa tatizo inakuja pale unaeongea naye juzi juzi tu alikuwepo huko kupumzika. Ndipo dharau inaanza.

Ila ukibeba mabox vizuri na ukiwa na chenji na ukatuliza boli hakuna dharau utakayokutana nayo
 
Home ni home hata kama ni shambani au pangoni, ukiwa home popote unapoenda unapata heshima yako. Majuu hata ukiwa na pesa na kama hujulikani ukienda viwanja vya juu bado hupati heshima au kuthaminiwa kama mtu mweupe.

Hapana. Hiyo siyo absolute. Hapa Tanzania unapata heshima ukiwa fisadi. Ukiwa mwizi mwizi, tapeli tapeli. Ndio watu watakuona wa maana na kujipendekeza pendekeza kwako na kukusikiliza. Kama unafuata taratibu na sheria utaonekana mjinga tu, huna akili, siyo mjanja, au siyo hustler. Ni akili fupi sana.

Vitapeli tapeli na vijizi jizi vya hapa bongo ndio vinaheshimika. Sisi upstanding, law abiding citizens hatupewi heshima kama wanayopewa hawa wezi na matapeli.
 
Last edited:
Hapana. Hiyo siyo absolute. Hapa Tanzania unapata heshima ukiwa fisadi. Ukiwa mwizi mwizi, tapeli tapeli. Ndio watu watakuona wa maana na kujipendekeza pendekeza kwako na kukusiliza. Kama unafuata taratibu na sheria utaonekana mjinga tu, huna akili, siyo mjanja, au siyo hustler. Ni akili fupi sana.

Vitapeli tapeli na vijizi jizi vya hapa bongo ndio vinaheshimika. Sisi upstanding, law abiding citizens hatupewi heshima kama wanayopewa hawa wezi na matapeli.

Partly true, ila kumbuka hao mafisadi hawapo wengi..
 
Partly true, ila kumbuka hao mafisadi hawapo wengi..
what?au na wewe mmojawapo bro?mafisadi bongo kila kona utayoenda wapo na dili zao za kuumizana tu,utake leseni,pasport,ukiumwa,ukiibiwa yaani ndo utalia maana unaenda polisi kuripoti na kutaka msaada polisi nao wanataka uwahonge tena hapo ndio nnapochoka,acha niitwe majina yote lakini maisha ya bongo mmmh hapana mtanisamehe sana ntajibanza hukuhuku
 
Mi nakujaga tu likizo kutembelea watu kama wewe. Nitaendela kukaa bongo kwa kweli. Rushwa mpaka upende mwenyewe huku, wa TZ wanaendekeza rushwa kutoka kwa mtoaji mpaka mpokeaji. Mimi nilishasema NOOOO to rushwa na ninaishi fresh tu
 
Hapana. Hiyo siyo absolute. Hapa Tanzania unapata heshima ukiwa fisadi. Ukiwa mwizi mwizi, tapeli tapeli. Ndio watu watakuona wa maana na kujipendekeza pendekeza kwako na kukusiliza. Kama unafuata taratibu na sheria utaonekana mjinga tu, huna akili, siyo mjanja, au siyo hustler. Ni akili fupi sana.

Kaka na wewe umerudi Bongo? Naona unazungumza kana kwamba tupo wote 'hapa'! Karibu sana tule hivi viyoyozi asilia wanavyoviita vumbi.
 
Hilo la vitu feki bongo usiseme,wizi mtupu.Mfano hai energy saving bulbs bongo life yake haizidi miezi 3 hadi minne.Nilibahatika kupata free sample energy saving bulbs( British Gas switch to Green Promo )leo miaka bado zinadunda,labelled 10 years life based on 10,000 hours
kukatika katika kwa umeme na kupanda na kushuka lazima hizo bulb zitakuwa chali tuuu
 
Wabeba mabox wapo na wala vumbi wapo na waliobeba mabox na sasa wanakula mavumbi pia wapo, pia kuna wala mavumbi wanaokwenda kuwatazama wabeba mabox kila mara.

wala vumbi wanaenda kuwatazama wabebabox kila mara???????? labda mafisadi, wacha uongo.........
 
wala vumbi wanaenda kuwatazama wabebabox kila mara???????? labda mafisadi, wacha uongo.........

Semilong;

Nadhani umekuja TZ miaka ya zamani sana au haupo connected. Miaka ileee kulikuwa hakuna makampuni ya kigeni. Kulikuwa na kampuni na mashirika ya umma.

Baada ya makampuni ya kigeni kuingia tumeona kwa sasa kuna vijana below 40 years ambao ni ma CEOs, kuna wa UBA (sijui wamebadili jina?) na kuna Kenya commercial bank na wengineo (barcklays bank pia ni kijana).

Haya makampuni ya kigeni yanazingatia uchapa kazi wako sio kitu kingine, matokeo yake wabongo kibao wana nafasi nzuri na salaries za above 5000 Usd kwa mwezi kwenda mpaka 12,000 Usd (may be zaidi ila sina mfano wa above that)bila marupurupu kama nyumba , gari etc.

Sasa kama wewe unaona hizo salaries hazitoshi kuja kuwaangalia wabeba mabox basi una matatizo au umeamua tu kuwa mmbishi.

Uliza jamaa zako wa bongo watakwambia..
 
wabeba boksi BLAH BLAH MINGI!fimbo za mbali hizo.kelele nyiiingiiiiiiiiiii,implementation F
 
Kwa maoni yangu kuishi nchi za watu na kuyamudu maisha, bila 'kupiga' mahali ni kuonesha una akili nyingi. Mazoba hawawezi kuishi nchi za watu maanake inabidi uwe na kila kitu proper in order. Bongo kila kitu slow na ujanja wa kubomoa nchi, na hata hao wanaojiita wana pesa sijui wana-enjoy nini..

Kila kitu kwa misele tu..huduma za jamii ovyoovyo, watu wamenunanuna tu..hata sehemu za 'kujinyoosha' zenyewe mgogoro, achilia mbali vitu katalogi wanakubambikizia feki au wanakuwekea bei za kupiga. Ahh ukiwa nchi za watu salala...wala vitu online, huduma za jamii fresh bin murua, hata kama unaishi maisha ya kati naamini unajichanua kuliko milionea fisadi wa bongo.

Kwanini usiwekeze nyumbani kama Mwakalinga kuliko kusifia sifia nchi za wenzenu...rudi home uwekeze mliopo majuu mkiwekeza home bonda bongo itakuwa tambarare.
 
Kwanini usiwekeze nyumbani kama Mwakalinga kuliko kusifia sifia nchi za wenzenu...rudi home uwekeze mliopo majuu mkiwekeza home bonda bongo itakuwa tambarare.

Mzee mbona unaleta assumption juu ya assumption? Umejuaje kuwa sipo bongo? Vitu vizuri lazima visifiwe kiwe chako au sio chako, kibaya na kizuri ni kama usiku na mchana na ukweli lazima usemwe.

Halafu kama nimekuelewa unataka kuonesha kuwa eti watu waliopo nje eti wawekeze ili kuinua hali ya huduma za kijamii. Hoja yako sio mbaya, lakini nadhani uhalisia wa mambo ni kuwa kuwatwisha hawa watu kwenye diaspora na jukumu zito kama hilo lililoishinda serikali yetu kwa tangu uhuru ni kuwaonea. Binafsi naamini huduma bora kwa wananchi zinakuwa championed na kuwa spear-headed na serikali, kama serikali imeshindwa ikae pembeni..Unaposhindwa kitu sio kung'ang'ania inabidi kuwaachia watu wanaoweza.
 
Mzee mbona unaleta assumption juu ya assumption? Umejuaje kuwa sipo bongo? Vitu vizuri lazima visifiwe kiwe chako au sio chako, kibaya na kizuri ni kama usiku na mchana na ukweli lazima usemwe.

Taifa linateketea kwa kupoteza nguvu kazi kama wewe rudi ujenge nchi yako using'ang'anie kwenye nchi walizo jenga wenzio rudi uwe mfano wa kuigwa kama Mwakalinga alivyo fanya.
 
Uelewa wangu finyu ni kuwa kuwepo au kutokuwepo kwa dharau huwa kunategemea na mtendewa au mdharauliwa. Mtu akikudharau halafu kwa bahati nzuri au mbaya wewe usi-ifeel ile dharau, then dharau inakuwa haipo kwa sababu inakuwa haijawakilisha kile ambacho kilikuwa intended. Ni pale tu mdharauliwa atakapoi-feel ndiyo itakuwa imefanya kazi. HIVYO HAWEZI KUKUDHARAU MTU MPAKA PALE TU WEWE MWENYEWE UTAKAPOFEEL KUWA UMEDHARAULIWA.

Katika hii mada, watu wanajaribu kujihami juu ya dharau, ila mimi naamini kuwa MTU YEYOTE MWENYE TENDENCY YA DHARAU, AU TENDENCE YA KU-FEEL KUDHARAULIWA WANAKUWA WAKO SCREW-LOOSED SOMEWHERE KWENYE VICHWA VYAO. MBAYA ZAIDI NA BILA KUJALI HADI YA MAISHA YAKE, WHETHER ANA PESA NYINGI OR NOT , NK, MWENYE DHARAU HUWA ANAITUMIA KAMA NGAO YA KUFICHA UDHAIFU WAKE MKUBWA ALIONAO.
TUSIWE NA DHARAU NA VILEVILE TUSIWE TUNAJISIKIA KUDHARAULIWA HATA KM NI MASKINI KIASI GANI, AU MATAJIRI
 
Chuki ya nini wakati wote ni waTZ. Tupendane tu na tusaidiane. Tuachane na ubishi usiokuwa wa maendeleo. Tuungane kupiga vita ufisadi.Tukae pamoja tuijenge Tanzania yetu.

Yes Flycather!! Umewakamata wangapi?? Au ni group ya mtuy???

Waambie kuwa mmeba box ndiye ana uchungu wa hiyo nchi na anajua akifanyacho. Mmeba box anajinyima then anapiga kitabu na pia mngojee ahuke sometimes hiyo elimu aliyonanyo utamkoma.

MMbeba box anamhudumia mama yake hapa kilimatembo na community yake kwa kuiuza Tanzania kwa majirani zake anaoishi nao.
 
Taifa linateketea kwa kupoteza nguvu kazi kama wewe rudi ujenge nchi yako using'ang'anie kwenye nchi walizo jenga wenzio rudi uwe mfano wa kuigwa kama Mwakalinga alivyo fanya.

Kwani kujenga taifa wewe una ku-define vipi? Nachukia sana mijadala isiyosogea!
 
Kwani kujenga taifa wewe una ku-define vipi? Nachukia sana mijadala isiyosogea!
wekezeni makwenu bana!taifa linajengwa na vijana,wataalamu wa nyanja mbali mbali!sio unaenda kusoma ki mastaz chako ukimaliza unaamua kubaki hukohuko UBEBE BOKSI,kisa bongo kuna njaa!.........
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom