Waandishi wa habari waache kuidhalilisha dini safi ya Uislam. Aliyeiba nguruwe sio "Imam" kwa maana alichokifanya ni kinyume na miongozo ya dini yake

Status
Not open for further replies.

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Habari zenu jamiiforums

Kwa wale msiomfahamu vema Infantry Soldier ni kwamba, mimi ni mkristo tena mkatoliki ila ninafahamu fika ya kuwa uislamu si ugaidi na si dini ya wizi na wala waislamu si magaidi na wala sio wezi bali wahalifu wachache hujificha katika kivuli cha uislamu ili kutenda uhalifu wao.

Dini ya uislamu ni dini safi sana tena ya watu waungwana kweli inayohubiri amani na upendo kama ilivyo dini ya kikristo. I love and respect all my muslim brothers and sisters out there.

171425407_10218528559597559_2549944044859624321_n.jpg


Tanzania ililazimika kupigana vita ya Kagera mwaka 1978 kwa lengo la kuikomboa ardhi yetu na kumtoa nduli Idd Amin Dada na genge la wahuni wenzie. Uamuzi wa kuivamia ardhi ya mkoa wa ziwa Magharibi (Kagera) haukuwa na ridhaa ya waganda hata kidogo bali ni maamuzi ya kipuuzi na kichokozi yaliyofanywa utawala wa kidhalimu wa dikteta Amini dada.

Kwanini uhalifu alioufanya Salum Yusuph wa kwenda kuiba nguruwe uhusishwe na nafasi ya ungozi wa kidini (Imam) ilhali kitendo hicho (wizi) sio muongozo sahihi wa dini ya kiislam? Je, hii ni sahihi? Je, haya ndio maadili ya taaluma ya uandishi wa habari?

aaaaaaaasdfvfgtre.jpg


Je, mnafahamu kuwa vyombo vya habari visipotumika ipasavyo vinaweza kuleta vurugu za kidini au hata kikabila ndani ya jamii ya watanzania? Mmesahau yaliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994? Leo hii mmesahau yaliyotokea nchini Kenya mwaka 2007? Ni njia zipi zilitumika katika kusambaza chuki kama sio vyombo vya habari?

Kulingana na Quran Tukufu, wizi umekatazwa katika Uislamu na ni dhambi kubwa sana. Inachukuliwa pia kuwa ni Haraam kulingana na maneno ya mtume Muhammad (SAW - peace be upon him). Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema amelaani wizi na ameamuru adhabu ya kisheria kupitia sheria ya Kiislam (Sharee’ah) kwa mwizi ni kukata mkono wa wake.

Mimi Infantry Soldier kabila langu ni mjaluo. Endapo itakuja siku moja kuonekana nimetoka msalani pasipo kunawa kabisa na kwenda moja kwa moja kwenye meza ya chakula kwa ajili ya kujiandaa na kula, Je itakuwa ni sahihi kusema kwamba, wajaluo wana tabia ya kula pasipo kunawa wakitoka msalani? Je, ni sahihi kutumia uovu wa mmtu mmoja katika kuhukumu wengine wa jamii yake?

Kabla ya mtu kufanya uhalifu, huwa anapanga kwanza mikakati kichwani mwake. Kitendo cha kupanga mikakati ovu kichwani tayari kinatosha kumvua mtu nafasi aliyonayo katika dini hata kabla hajatenda uovu husika.

Kitendo cha Imam mstaafu kupanga kuiba nguruwe kinamvua wadhifa ule hata kabla hajatenda tukio hilo la wizi. Alitenda tukio la wizi akiwa sio Imam tena kwa maana dini inakataza mtu wa hadhi yake kuwaza kutenda uovu wa namna ile.

asasdddddddfdedcv.jpg


Ninatambua na kuheshimu mchango wa wanataaluma wa tasnia ya habari katika kujenga jamii yenye umoja na mshikamano, lakini katika hili la uchochezi wa kidini ni lazima tulikemee sote kwa pamoja.

Maoni ya wadau;
==========
mjibu hoja nakupongeza , hii ni taabu ya kuwa na waandishi wasio waandishi. TAALUMA HII IMEVAMIWA . na biashara ya magazeti imekuwa ngumu kwa sasa kutokana na teknolojia. huyo muandishi uchara anatakiwa kujua KUNA UISLAMU , NA MUISLAMU.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Kwa wale msiomfahamu vema Infantry Soldier ni kwamba, mimi ni mkristo tena mkatoliki. Dini ya uislamu ni dini safi sana tena ya watu waungwana kweli inayohubiri amani na upendo kama ilivyo dini ya kikristo. I love and respect all my muslim brothers and sisters out there.
Ochie nade omera!!
 
Taarifa siku zote huwa haina nguvu ila kile kitakacho ng'amuliwa au tambuliwa kutokana na hiyo taarifa ndo kitu muhimu sana..

Tunaweza kuwa na taarifa ya kawaida tu na isilete taharuki.. Ila taarifa hiyo kwa namna fulani ikatambuliwa au ikawa imetafsiriwa kwa mlengo fulani inaweza kuleta madhara makubwa..

Katika Mass Journalism Perception ndo kila kitu, ndo maana nchi zilizoendelea kiuchumi zinatumia Propaganda kujaribu ku Control Perception ya watu baada ya habari au taarifa kutoka.

Wenzetu hawazuii taarifa zao kuwa public ila wanajitahidi sana kubadili Perceptions za watu kutokana na taarifa zilizotolewa.

Ulichofanya wewe ni kutusaidia sisi, tu-perceive uimamu wa muhalifu una uhusiano na Uislamu wake.. Ila inawezekana katika habari hiyo lengo la kuweka Uimamu ni kumtambua muhalifu kwa cheo chake katika jamii.

Uimamu wake ni Uislamu au Uimamu wake ni cheo chake katika jamii yake..

Inawezekana lengo la habari ni kuwapa watu taarifa kwamba haijalishi cheo cha mtu ila yeyote anaweza kufanya uhalifu katika jamii yetu..
 
Uislamu umetuhumiwa kila aina ya uhalifu tangu enzi hizo !! Na bado wataendelea huchafua jina na taswira... ili hali hakuna shida wala kutikisa unywele wa Musislamu...waendelee tu Imani za waislam zinakomaa!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom