Mjukuu wa bibi Pili.
Member
- Dec 21, 2011
- 71
- 75
CHAMA cha waandishi wa habari mkoa wa Kilimanjaro (MECKI) kimemtaka
mbunge wa jimbo la Rombo Mh Joseph Selasini kutumia taratibu za chama
hicho kutoa malalamiko yanayo wahusu wananchama wake.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kaimu katibu mkuu wa chama hicho
Nakajumo James alisema kuwa Jan 11 mwaka huu katika kikao cha ushauri
cha mkoa wa Kilimanjaro (RCC),Mh Selasini aliwarushia tuhuma waandishi
wa habari watatu ambao hata hivyo hakuwataja majina kuwa wanafanya
kazi zao kinyume na maadili ya uandishi wa habari ..
Mh Selasini alipaswa kuwasilisha tuhuma zake hizo kwenye klabu ya
waandishi wa habari kimaandishi kwa ajili ya taratibu nyingine
kuchukuliwa dhidi ya watuhumiwa lakini ama kwa bahati mbaya ama
makusudi akaamua kwenda kulisemea suala hili kwenye kikao cha RCC
jambo ambalo kwetu sisi linatucahuaalisema James.
James alisema kuwa tuhuma zilizotajwa si tu zinawagusa watuhumiwa,
bali zinamgusa na kumchafua kila mwanahabari Kilimanjaro pamoja na
Klabu kwa ujumla,tuhuma zinazoweza kuleta madhara makubwa katika
maendeleo ya klabu,tasnia na nchi kwa ujumla.
Hatukutegemea mh Selasini angeweza kwenda kusemea jambo hili katika
kikao ambacho anatambua wazi kuwa waandishi wa habari hawatapata
nafasi katika kikao hicho kulitolea ufafanuzi hata hivyo hatuwezi
kukaa na kulifumbia macho jambo hili. Kukaa kimya ni kukubali
kuchafuliwa waandishialisema James.
Hata hivyo James alisema kufuatia tuhuma hizo klabu imechukua hatua za
awali za kumtaka mh Selasin kuwasilisha tuhuma hizo kimaandishi dhidi
ya watuhumiwa ili MECKI kama taasisi inayotambulika kisheria iwe
imethaminiwa na kupewa nafasi ya kutenda na kushughulikia masuala kwa
mujibu wa taratibu zake zilizopo.
Alisema suala hilo litakapofikishwa katika uongozi kwa mujibu wa
taratibu,litashughulikiwa ili kuhakikisha haki inatendeka lakini pia
kuboresha mahusiano baina ya pande hizo mbili, kwa maana ya wanahabari
na Mbunge kwani klabu inalenga kuimarisha mahusiano ya kikazi .
Aidha James alisema Klabu itaendelea kutetetea kwa nguvu zake zote
maadili ya uandishi wa habari kwa mujibu wa katiba yake na sheria
zingine za nchi zinazolinda maadili ya uandishi wa habari.
Alisema MECKI inakemea vikali uvunjifu wowote wa maadili ya uandishi
wa habari na kutoa wito kwa wanachama wake na waandishi wa habari kwa
ujumla kufanya kazi kwa misingi ya taaluma, bila kuvunja maadili na
sheria za nchi.
Klabu haitafumbia macho mtu yeyote anayejaribu kuvunja maadili ya
taaluma ya uandishi wa habari na kama kuna taasisi au wadau wowote
watakuwa na lalamiko dhidi ya vitendo vya baadhi ya wanahabari ni
vyema wakawasilisha masuala hayo kwa viongozi wa klabu kwa maandishi
na ushahidi ili kuhakikisha haki inatendeka badala ya kulaumiana
pekeealisema James.
MWISHO.
Sourceress release toka MECKI