Waandishi Kilimanjaro wamtaka Mh Selasini kuacha kuropoka

Dec 21, 2011
71
75
CHAMA cha waandishi wa habari mkoa wa Kilimanjaro (MECKI) kimemtaka
mbunge wa jimbo la Rombo Mh Joseph Selasini kutumia taratibu za chama
hicho kutoa malalamiko yanayo wahusu wananchama wake.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kaimu katibu mkuu wa chama hicho
Nakajumo James alisema kuwa Jan 11 mwaka huu katika kikao cha ushauri
cha mkoa wa Kilimanjaro (RCC),Mh Selasini aliwarushia tuhuma waandishi
wa habari watatu ambao hata hivyo hakuwataja majina kuwa wanafanya
kazi zao kinyume na maadili ya uandishi wa habari ..

“Mh Selasini alipaswa kuwasilisha tuhuma zake hizo kwenye klabu ya
waandishi wa habari kimaandishi kwa ajili ya taratibu nyingine
kuchukuliwa dhidi ya watuhumiwa lakini ama kwa bahati mbaya ama
makusudi akaamua kwenda kulisemea suala hili kwenye kikao cha RCC
jambo ambalo kwetu sisi linatucahua”alisema James.

James alisema kuwa tuhuma zilizotajwa si tu zinawagusa watuhumiwa,
bali zinamgusa na kumchafua kila mwanahabari Kilimanjaro pamoja na
Klabu kwa ujumla,tuhuma zinazoweza kuleta madhara makubwa katika
maendeleo ya klabu,tasnia na nchi kwa ujumla.

“Hatukutegemea mh Selasini angeweza kwenda kusemea jambo hili katika
kikao ambacho anatambua wazi kuwa waandishi wa habari hawatapata
nafasi katika kikao hicho kulitolea ufafanuzi hata hivyo hatuwezi
kukaa na kulifumbia macho jambo hili. Kukaa kimya ni kukubali
kuchafuliwa waandishi”alisema James.

Hata hivyo James alisema kufuatia tuhuma hizo klabu imechukua hatua za
awali za kumtaka mh Selasin kuwasilisha tuhuma hizo kimaandishi dhidi
ya watuhumiwa ili MECKI kama taasisi inayotambulika kisheria iwe
imethaminiwa na kupewa nafasi ya kutenda na kushughulikia masuala kwa
mujibu wa taratibu zake zilizopo.

Alisema suala hilo litakapofikishwa katika uongozi kwa mujibu wa
taratibu,litashughulikiwa ili kuhakikisha haki inatendeka lakini pia
kuboresha mahusiano baina ya pande hizo mbili, kwa maana ya wanahabari
na Mbunge kwani klabu inalenga kuimarisha mahusiano ya kikazi .

Aidha James alisema Klabu itaendelea kutetetea kwa nguvu zake zote
maadili ya uandishi wa habari kwa mujibu wa katiba yake na sheria
zingine za nchi zinazolinda maadili ya uandishi wa habari.

Alisema MECKI inakemea vikali uvunjifu wowote wa maadili ya uandishi
wa habari na kutoa wito kwa wanachama wake na waandishi wa habari kwa
ujumla kufanya kazi kwa misingi ya taaluma, bila kuvunja maadili na
sheria za nchi.

“Klabu haitafumbia macho mtu yeyote anayejaribu kuvunja maadili ya
taaluma ya uandishi wa habari na kama kuna taasisi au wadau wowote
watakuwa na lalamiko dhidi ya vitendo vya baadhi ya wanahabari ni
vyema wakawasilisha masuala hayo kwa viongozi wa klabu kwa maandishi
na ushahidi ili kuhakikisha haki inatendeka badala ya kulaumiana
pekee”alisema James.

MWISHO.

Source:press release toka MECKI
 
Kama tuhuma ni za kweli jibu na chukua hatua za muhimu.haya mambo ya ccm kwamba kuna tuhuma unataka kuandikiwa ili iweje?nchi hii ipo hapo ilipo kwa sababu tu za kuficha mambo,kwani kama ni ukweli ukisema au kuawaandikia inapunguza nini?pia maadili ya waandishi ni kwa ajili ya waandishi wa habari si kwa kila mtu!
 
Uthibitisho mwingine wa wa uandishi usio na taaluma wa magazeti ya Tanzania:

Soma hiyo habari halafu nambie umeelewa wanasema Selasini alituhumu nini kimefanywa na waandishi, akilenga chombo gani, nani, na kilifanywa kwa nini. Yani unasoma habari unatoka kama ulivyokuja, huja learn any substantive details from it.

Selasini alisema nini? Hakuna! Hawasemi.


Huwezi kusoma news article ya gazeti la nchi iliyoendelea ukakuta information gaps kama hizo halafu editor apitishe lichapishwe. Yagudu! Upupu mtupu. Hakuna fani inayotuangusha Tanzania kwa kunyima habari umma kama hawa waandishi feki wa vyombo vyetu hivi. Vilaza wa kutupwa.
 
Waandishi wetu na kozi zao za mimba ndo hao gazeti ukinunua dakika chache baadaye unatupa. anagalia daily papers zetu ni ipi unaweza fananisha na The nation au standard za kenya. Wanatakiwa kujifunza
 
lakini kusema kweli me mh selasini simwelewi elewi vile,naona kama ka mzigo flani ivi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom